Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda afurushwa Marekani
Marekani imemrudisha nyumbani msomi mmoja wa Rwanda anayetuhumiwa kuwa mtu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Kufurushwa kwa Leopold Munyakazi kunajiri baada ya kupoteza kesi ya kupata uhifadhi nchini Marekani.
Anatuhumiwa kwa kuvaa majani ya mgomba wakati wa mauaji hayo ya kimbari ili kujitambulisha kuwa raia wa kabila la Hutu,mbali na kupanga mashambulio ya usiku katika nyumba za familia za watu wa kabila la Tutsi .
Bwana Munyakazi ,aliyewahi kuhudumu kama profesa wa chuo kikuu amekana madai hayo.
Takriban Watutsi 800,000 na watu wa kablila la Hutu wenye ustani waliuawa na wapiganaji wa Kihutu katika kipindi cha siku 100 pekee mwaka 1994.