Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waasi wasema watu 100, wauawa DRC, wakati wa maandamano
Waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kiasi cha watu mia moja wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali, katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Vyanzo vingine vya habari vinasema watu waliouawa ni 40.
Ofisi ya Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila imepinga taarifa hizo, huku ikiwalaaumu viongozi wa maandamano hayo kwa kuchochea ghasia hizo za umwagaji damu.
Upinzani nchini humo wamevilaumu vyombo vya usalama kwa kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakiandamana kwa amani juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo.
Wanaamini kuwa Rais Kabila anajaribu kung'ang'ania madaraka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake.