Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Al-Shabab lamuua jenerali wa jeshi Somalia
Mlipuaji wa kujitolea muhanga katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu amemuaa kamanda mmoja wa jeshi pamoja na walinzi wake sita.
Mshambuliaji huyo aliligonga gari lake lililojaa vilipuzi na msafara wa jenerali Mohamed Jimale Goobaale karibu na makao makuu ya jeshi .
Jimale alikuwa amenusurika majaribio mengi ya kumuua .
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab walikiri kutekeleza shambulio hilo wakisema kuwa jenerali huyo alikuwa kipanga mashambulizi mengi dhidi yao.