Trump ataka walinzi wa Clinton wapokonywe silaha

Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump

Wafuasi wa Bi Hillary Clinton, wamelaani vikali matamshi ya leo ya kejeli aliyotoa Donald Trump, dhidi ya Bi Clinton.

Mgombea huyo wa kiti cha urais wa chama cha Republican, amesema walinzi wa Bi Clinton wapokonywe silaha walizo nazo ndipo watu waone kitakachomtokea Bi Hillary Clinton

Bwana Trump alikuwa akizungumza na wafuasi wake katika mkutano wa kampeni huko Miami ,akitetea hoja yake kwamba raia wa marekani zaidi wana haki ya kumiliki bunduki.

Anadai kuwa Bi Hillary Clinton anataka kuwaondolea sheria inayowapa haki hiyo.

Hillary Clinton

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hillary Clinton

Wafuasi wa Bi Clinton wanasema kauli hizo za Trump hazikubaliki kwani ni za kuchochea ghaisia.

Mwezi jana Trump aliwahimiza wafuasi wake wafanye kila kinachowezekana kumzuia Bi Clinton kuiondoa sheria hiyo matamshi ambayo wana Democratic waliyatafsiri kama uchochezi na vitisho vya kumtishia maisha mgombea wao Bi Clinton .