Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mugabe afuta ziara yake nchini Ghana
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefuta ziara yake kwenda nchini Ghana kupokea tuzo la Millennium Lifetime Achievement award, kwa kuliongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika kupata uhuru wake mwaka 1980.
Rais wa Ghana John Mahama alitarajiwa kumpa Mugabe tuzo hilo, wakati wa warsha ambayo ingefanyika katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ameingoza Zimabawe tangu ipate uhuru na ameapa kusalia madarakani hadi kifo na kukataa wito wa kumtaka ang'atuke.
Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa safari hiyo, lakini mtandao mmoja nchini Ghana unawanukuu wanadiplomasia nchini Zimbabwe wakisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana masuala ya kisiasa nchini Zimbabwe.
Mabango makubwa yalikuwa yamewekwa mjini Accra kumkaribisha Rais Mugabe na pia hotuba yake ilikuwa imesubiriwa kwa hamu.