Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa kwa mapigano Syria

Chanzo cha picha, Getty Images
Umoja wa mataifa umetaka kusitishwa kwa haraka mapigano yanayoendelea katika mji wa Alleppo nchini Syria.
Pia tahadhari kuhusu usambazwaji wa chakula na dawa upo katika hatari kufuatia kutengwa na wakazi wa maeneo hayo.

Katika siku za karibuni waasi walifukuzwa na majeshi ya serikali yaliyopo mjini Aleppo.
Shirika la habari la serikali la Syria limeripoti kuwa majeshi ya serikali yamefanikiwa kurudisha majimbo yaliyokuwa mikononi mwa waasi katika mji wa kusini magharibi mwa mji iliyokaliwa na waasi.








