Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Video ya droni ya IDF 'yaonyesha Sinwar katika dakika za mwisho'
Muda wa kusoma: Dakika 1
Picha ya video ya droni iliyotolewa na jeshi la Israel siku ya Alhamisi inasemekana kuonyesha dakika za mwisho za kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kabla ya kuuawa.
Video inaonekana kupigwa kutoka kwa droni ambayo inapita dirisha lililo wazi la jengo lililoharibiwa zaidi.
Inamkaribia mtu aliyeketi bila kusonga kwenye kiti kwenye ghorofa ya kwanza ya nyumba ambayo imejaa uchafu.
Mtu huyo ambaye anaonekana kujeruhiwa, kisha anarusha kile kinachoonekana kuwa fimbo kwenye droni na video inaisha.