'Kutuma pesa Korea Kaskazini ni kama filamu ya ujasusi'

Na Jungmin Choi,

BBC Idhaa ya Korea

h

Chanzo cha picha, Jungmin Choi / BBC Korean

Maelezo ya picha, Dalali Hwang Ji-sung alikimbilia Korea Kusini mwaka 2009

"Ni kama filamu ya ujasusi na watu huweka maisha yao hatarini ," anasema Hwang Ji-sung, dalali wa Korea Kusini ambaye amekuwa akiwasaidia waasi wa Korea Kaskazini kutuma pesa zinazohitajika sana nyumbani kwa zaidi ya muongo mmoja.

Miaka kadhaa iliyopita, raia wa Korea Kaskazini walibuni neno "Hallasan stem" kwa watu wanaopokea msaada kutoka kwa waasi wa Korea Kusini, anasema Hwang.

Hallasan ni jina la Mlima Halla, volkano maarufu uliopo katika kisiwa cha Jeju cha Korea Kusini.

"Mtu kutoka familia ya shina ya Hallasan anachukuliwa kuwa mke anayehitajika zaidi, hata bora kuliko wanachama wa Chama cha Kikomunisti," anasema.

Utafiti wa mwaka 2023 uliofanywa na Kituo cha hifadhi ya data kuhusu Haki za Binadamu cha Korea Kaskazini ambacho kiliwahoji takriban watu 400 walioasi Korea Kaskazini, ulibaini kuwa karibu asilimia 63 kati yao walikuwa wametuma pesa kwa familia zao Kaskazini.

Lakini sasa kutokana na kuongezeka kwa ukandamizaji kutoka Kaskazini na Kusini, usafirisha ya fedha kutoka kusini hadi kaskazini linekuwa ni jambo la hatari kubwa.

Tayari ni kazi ngumu inayohitaji mtandao wa siri wa madalali na wasafirishaji ambao wameenea kote Korea Kusini, China na Korea Kaskazini.

Mawasiliano ya siri kwa kutumia simu za Kichina zilizoingizwa yanatumika katika maeneo ya mbali. Majina ya msimbo hutumiwa.

Gharama ni ya juu sana kwani pesa hizi zimepigwa marufuku katika Korea Kusini na Kaskazini.

Tangu mwaka 2020, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameimarisha msako dhidi ya madalali ili kuzuia usafirishaji wa fedha na maingiliano ya "tabia na utamaduni" kutoka Korea Kusini.

Wanakabiliwa na hatari ya kupelekwa katika kambi za kisiasa za nchi hiyo, zinazojulikana kama kwan-li-so, ambako mamia kwa maelfu wanaaminika kufariki.

f

Chanzo cha picha, Jungmin Choi / BBC

Maelezo ya picha, Wanandoa hao wamekuwa katika biashara ya kuhamisha pesa kwa zaidi ya muongo mmoja
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Idadi ya madalali nchini Korea Kaskazini imepungua kwa zaidi ya asilimia 70 ikilinganishwa na miaka michache iliyopita," anasema Joo So-yeon, mke wa Bw Hwang. Yeye pia ni dalali.

Korea Kusini pia imeweka marufuku ya usafirishaji huo wa pesa, lakini katika siku za nyuma mamlaka zimeangalia njia nyingine. Sasa hali hii inabadilika.

Aprili mwaka jana, nyumba ya Bw Hwang na Bi Joo katika jimbo la Gyeonggi - ambalo liko karibu na Seoul - ilivamiwa na maafisa wanne wa polisi, ambao walimshutumu kwa kukiuka sheria ya miamala ya fedha za kigeni.

Washukiwa wengine saba pia wanachunguzwa.

Polisi hawajajibu uchunguzi wa BBC kuhusu kesi ya Bi Joo.

Maafisa wa Korea Kusini walimuambia Bw Hwang kwamba utumaji wowote wa fedha kwenda Korea Kaskazini unapaswa kufanywa kupitia "benki halali".

"Kama kuna moja, nijulishe!" alisema, akiongeza kuwa hakuna taasisi ambayo inaweza kupokea fedha kisheria nchini Korea Kaskazini kwa kuwa Korea hizo mbili bado ziko vitani.

Uhusiano kati ya Korea mbili umekuwa ukizidi kuwa mbaya tangu Korea Kaskazini ilipolipua ofisi ya uhusiano na Korea Kusini mwaka 2020. Mapema mwezi huu, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema haiwezekani kuungana tena na Korea Kusini - lengo

Simu za siri

Shughuli hii nzima huanza kwa mawasiliano ya simu kati ya waasi wa Kusini na familia zao huko Kaskazini - iliyowezeshwa na uingizwaji wa simu za Kichina zilizoingizwa katika majimbo ya mpakani ambayo yanaweza kunasa mitandao ya mawasiliano ya China.

Mawasiliano haya huwezeshwa na madalali nchini Korea Kaskazini ambao hulazimika kusafiri umbali mrefu na wakati mwingine hata kupanda milima kupanga mawasiliano ya aina hii.

Baada ya kusubiri kwa saa kadhaa, simu huunganishwa, na muasi hukubaliana na dalala kuhusu malipo na familia atakazo zungumza nazo. Lakini mazungumzo yanapaswa kuwa ya siri ili kuepuka kufuatiliwa na Wizara ya Usalama wa Taifa.

Muasi kisha hufanya amana katika akaunti ya Kichina kupitia mawakala nchini Korea Kusini. Hii pia inakumbwa na hatari kwani China pia inafuatilia kwa karibu mtiririko wa fedha za kigeni nchini humo.

Ni jukumu la madalali wa China kuleta pesa hizo Korea Kaskazini.

Mipaka hiyo ni muhimu sana kwasababu China ni mshirika muhimu wa Korea Kaskazini. Malipo kutoka kwa waasi wakati mwingine hufichwa kama shughuli kati ya makampuni ya kibiashara ya China na Korea Kaskazini.

Wanaajiri wafanyakazi kadhaa nchini Korea Kaskazini ili kupeleka fedha hizo kwa familia.

w

Chanzo cha picha, Jungmin Choi / BBC

Maelezo ya picha, Kim Jin-seok alikuwa dalali wa Korea Kaskazini kabla ya kuikimbia nchi hiyo mwaka 2013

"Watu wanaotoa pesa hawajuani, na hawapaswi kujuana kwasababu maisha yao yako hatarini," anasema Kim Jin-seok, ambaye alikuwa akifanya kazi kama dalali nchini Korea Kaskazini kabla ya kuikimbia nchi hiyo mwaka 2013.

Madalali hulazimika kutumia nambari na alama za siri kuashiria ni wakati gani utakaokuwa salama kwa familia kupokea pesa.

Bwana Hwang, ambaye ana wateja 800, anasema hata amekutana na familia ambazo zilikataa pesa hizo.

"Waliogopa kwamba inaweza kuwa mtego uliowekwa na polisi wa usalama na walisema, 'Hatutakubali pesa kutoka kwa wasaliti.'"

Mara baada ya fedha kutolewa, mawakala huchukua karibu 50% ya pesa zilizotumwa kama malipo yao.

"Mawakala wa Korea Kaskazini huhatarisha maisha yao kupata kati ya 500,000 na 600,000 kila wanapotuma pesa," Hwang anasema.

"Siku hizi, kama utakamatwa na afisa wa usalama na kuhukumiwa, utakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela. Kama utapatikana na hatia ya ujasusi, utapelekwa katika kwan-li-so."

Bwana Hwang anatuonyesha mashahidi miongoni mwa raia wa Korea Kaskazini ambao wamepokea pesa kupitia kwa madalali wake.

g

Chanzo cha picha, Jungmin Choi / BBC

Maelezo ya picha, Korea Kaskazini huhesabu fedha hizo baada ya kupokea malipo kutoka kwa madalali

"Nilikuwa na njaa kila siku na kula nyasi," analia mwanamke mzee mmoja wao, ambaye mikono yake imevimba kutokana na kutafuta chakula katika misitu.

Katika video hiyo hiyo, mwanamke mwingine anasema: "Ni vigumu sana hapa kiasi kwamba nataka niwashukuru mara 100."

Bi Joo anasema moyo wake huvunjika kila wakati anapoona video hizi.

"Baadhi ya waasi wamewaacha wazazi na watoto wao nyuma. Wanataka tu kuhakikisha kwamba familia zao nchini Korea Kaskazini zitaishi ili waweze kuungana tena siku moja."

Anasema pesa milioni moja inatosha kulisha familia ya watu watatu kwa mwaka mmoja kaskazini.

Mfumo unaonusuru maisha

Haijulikani ni kwanini Korea Kusini imeanza kuwakandamiza madalali, lakini wakili Park Won-yeon, ambaye amekuwa akitoa msaada wa kisheria kwa waasi, anaamini kuwa ukaidi unaweza kuwa sababu, kwani nguvu ya kuchunguza kesi za usalama wa taifa, kama vile ujasusi, ilihamishiwa kwa polisi kutoka kwa Huduma ya Taifa ya Upelelezi mwaka huu.

"Kama polisi watashindwa kuthibitisha mashtaka ya ujasusi, watawafungulia mashtaka chini ya Sheria ya Miamala ya Fedha za Kigeni," anasema.

Kutokana na shinikizo kubwa kutoka kwa serikali zote mbili, mfumo huu wa kunusuru familia za waasi wa Korea Kaskazini unaweza kuathiriwa.

Bwana Hwang yuko tayari kupeleka kesi ya mkewe katika mahakama kuu iwapo atapatikana na hatia. Anaamini kuwa malipo kutoka kwa waasi sio tu kuhusu pesa.

"Ni njia pekee ya kuiangusha Korea Kaskazini bila ya mapigano," alisema. "Pamoja na fedha, pia mfumo huu huambatana na habari kwamba Korea Kusini ina mafanikio na tajiri... Hivyo ndivyo Kim Jong-un anavyoogopa."

Kim anaamini kuwa waasi kama yeye hawataacha kutuma pesa kwa wapendwa wao nyumbani, ingawa mamlaka kutoka pande zote mbili zinataka kuwazuia. Anasema atasafiri kwenda China mwenyewe kutoa fedha hizo ikiwa ni lazima.

"Nilijiingiza katika hatari ya kutowaona watoto wangu tena, lakini angalau watoto wangu watakuwa na maisha mazuri," anasema.

"Tutatuma pesa kwa njia yoyote tunayoweza, na bila kujali ni nini."

Sasa anafanya kazi kama dereva wa lori nchini Korea Kusini na analala kwenye gari lake siku tano kwa wiki.

Anajinyima na kuweka pesa kadri iwezekanavyo ili aweze kutuma pesa milioni nne kwa mke wake na watoto wawili wa kiume korea Kaskazini kila mwaka. Amekuwa akisikiliza ujumbe wa sauti kutoka kwa familia yake mara kwa mara.

Mmoja wa watoto wake anasema, "Wewe ni nani, baba? Una maumivu kiasi gani? Ugumu wetu wa maisha si kitu ukilinganishwa na wako."

Kim Jin-seok amepewa jina bandia kama njia ya kulinda usalama wake.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi