Damu iliyotengenezwa maabara na kuwekwa kwa binadamu,ni damu ya aina gani na imetengenezwa vipi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pakiti za damu

Nyama iliyooteshwa kwenye maabara...viungo vilivyotengenezwa na maabara... na sasa damu inaingia kwenye orodha hiyo.

Kwa mara ya kwanza duniani, damu iliyoundwa katika maabara imeweza kuwekwa kwa binadamu, watafiti wa Uingereza walisema.

Kama sehemu ya majaribio , kiasi kidogo cha vijiko viwili vya damu vilitiwa katika mwili wa binadamu.

Watafiti wanaona jinsi damu iliyotengenezwa kwenye maabara inavyofanya kazi baada ya kuingia mwilini.

Kundi la maafisa wa afya kutoka NHS Blood and Transplant ya Uingereza na wenza kutoka Bristol, Cambridge na London walifanya kazi kwa pamoja kwenye mradi huu.

Kwa sasa hakuna chaguo jingine ila kutegemea wafadhili wa damu.

.

Chanzo cha picha, NHSBT

Maelezo ya picha, Seli nyekundu ya damu

Aina adimu za damu ni ngumu kupata

Kupata damu kutoka kwa vikundi adimu sana kama vile 'Bombay blood' na 'AB-ve' ni kazi ngumu sana. Lengo kuu la watafiti ni kukuza vikundi kama hivyo kwenye maabara.

Watu wanaougua magonjwa kama vile anemia ya seli mundu mara nyingi huhitaji kutiwa damu mishipani.

Damu ya kundi moja la damu na mwili wa mgonjwa inapaswa kuongezwa. Ikiwa damu ni ya kundi tofauti, mwili hautakubali.

Baadhi ya aina za damu 'ni nadra sana', alisema Prof Yasley Toye wa Chuo Kikuu cha Bristol. Alisema kuwa ni 'watu 10 tu duniani' wanaweza kuchangia baadhi ya vikundi.

'Bombay blood' ni mojawapo ya makundi ya damu adimu zaidi duniani. Ilitambuliwa kwa mara ya kwanza huko Bombay. Kwa sasa kuna vitengo vitatu pekee vya aina hii ya damu vinavyopatikana kote Uingereza.

Watafiti wanatumai kutengeneza damu katika maabara kama suluhisho la shida kama hizo.

Jinsi inavyoandaliwa katika maabaara

.

Chanzo cha picha, NHSBT

Maelezo ya picha, Jinsi damu ya maabara invyoandaliwa

Seli nyekundu za damu zina jukumu muhimu katika kubeba oksijeni kutoka kwa mapafu hadi sehemu zingine za mwili.

  • Kwanza, karibu 470 ml ya damu hukusanywa kutoka kwa wafadhili.
  • Seli za shina ambazo zina uwezo wa kuwa seli nyekundu za damu hukusanywa kutoka kwa damu kwa msaada wa shanga za sumaku.
  • Seli shina hizi hukuzwa kwa wingi katika maabara.
  • Seli za shina zilizotengenezwa kwenye maabara hubadilishwa kuwa seli nyekundu za damu.
  • Utaratibu huu wote unachukua kama wiki tatu. Hivi sasa, seli nyekundu za damu crore 5,000 zinazalishwa kutoka kwa seli za shina laki 5. Baada ya hapo, huchujwa katika hatua kadhaa na hatimaye chembe nyekundu za damu milioni 1,500 hukusanywa.

 Chembe hizi nyekundu za damu crore 1,500 hukua na kuwa damu.

 "Tunatumai kutoa damu nyingi iwezekanavyo katika siku zijazo. Ndoto yangu ni kuwa na mashine kubwa inayoendelea kutoa damu,' alisema Prof. Yasli Toi.

'Bora kuliko damu ya kawaida'

.

Chanzo cha picha, NHSBT

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Watu wawili waliojitolea sasa wamewekewa damu iliyotengenezwa na maabara.

Jumla ya watu 10 wenye afya njema watachangia damu kama sehemu ya utafiti huu. Kati ya mililita 5-10 za damu hutiwa katika miili yao kila baada ya miezi minne. Moja hupewa damu ya kawaida na mwingine ni damu iliyotengenezwa katika maabara.

Seli za damu zinazokuzwa katika maabara zimetambulishwa kwa nyenzo za mionzi. Kwa njia hiyo watafiti wanaweza kuona ni muda gani damu hiyo inakaa mwilini.

Damu iliyotengenezwa na maabara inadhaniwa kuwa na ufanisi zaidi kuliko damu ya kawaida.

Kwa kawaida chembe nyekundu za damu mwilini hufa ndani ya siku 120 hivi.

Baada ya hayo, wanapaswa kubadilishwa na kupata mpya. Wakati damu inakusanywa kutoka kwa mwanadamu, ina chembe nyekundu za damu changa na za zamani. Kwa hiyo baadhi ya seli nyekundu za damu hufa.

Lakini damu iliyotengenezwa na maabara ina chembechembe zote nyekundu za damu. Kwa hivyo zinaishi kwa siku 120. Hivyobasi, watafiti wanasema, hakuna haja ya kuwekewa damu nyengine

Lakini kuendeleza damu katika maabara kunahitaji kushinda changamoto za kifedha na kiufundi. Gharama ya wastani ya kuchangia damu kwenye NHS nchini Uingereza ni £130. Lakini kuikuza katika maabara kunagharimu zaidi ya hiyo.

Seli za shina zilizovunwa kutoka kwa damu hufa haraka. Kwa hiyo, idadi ya kutosha ya seli nyekundu za damu haiwezi kutengenezwa. Hivyo, kiasi kidogo cha damu kinatengenezwa. Hii ni changamoto nyingine. Utafiti mwingi bado unahitajika ili kutengeneza damu ya kutosha kwa mahitaji ya binadamu.