Wafahamu 'viongozi watatu' wa Al shabab wanaosakwa na Marekani
Na Ambia Hirsi

Chanzo cha picha, AL KATAIB
Siku moja baada ya Marekani kutangaza zawadi ya dola milioni 10 za Kimarekani kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wanaume watatu wanaosadikiwa kuwa uti wa mgongo wa kundi la kigaidi la Alshabab linalohangaisha mamlaka nchini Somalia gumzo limeibuka kuhusu utambulisho wao.
Siku ya Jumanne kupitia taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa Twitter wa Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani na kushirikishwa katika akaunti ya Twitter Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi ilisema: " Zawadi ya hadi dola milioni 10 itatolewa kupata taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa magaida kama vile MAHAD KARATE, AHMED DIRIYE & JEHAD MOSTAFA,ambao wamehusika katika mashambulio yaliyosababisha vifo vya maelfu ta watu, Somalia, Kenya na mataifa mengine. Je unajua wanakojificha? Tufahamishe!
Je wanaume hawa ni kina nani
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
1. Mahad Karate

Chanzo cha picha, Social Media
Abdirahman Mohamed Warsame,anayefahamika kama "Mahad Karate" ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika kundi la Al-Shabaab.
Kulingana na serikali ya Marekani, inaaminika uwa alizaliwa kati yam waka 1957 na 1962 huko Harardhere, uliopo eneo la Mudug katikati mwa Somali.
Alikuwa naibu kiongozi wa Al-Shabaab,aliyehudumu katika kitengo kikuu cha intelijensia cha kundi hili linalojulikana kama usalama n ahata wakati mwingine kuwa sehemu ya usimamizi wa masuala ya kifedha ya kundi hilo.
Marekani inasema Mahad Karate anaongea Kisomali, Kiarabu na
Swahili.
2. Ahmed Diriye
Ahmed Diriye Omar, ambaye pia anafahamika kama "Abu Ubaydah" ni mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Al-Shabaab.
Hakuna maelezo mengi yanayojulikana kuhusu Maisha yake lakini aliwahi kuwa mkuu wa mrengo wa Al-Kataib.
Sauti iliyotolewa na chombo cha habari cha Al-Shabaab mnamo Septemba 2019 inasadikiwa kuwa ya Ahmed Diriye na alisikika akizungumzia masuala ya Somalia ijapokuwa kumekuwa na uvumi kuhusu kifo chake.
Ni nadra sana kumuona hadharani Ahmed Diriye lakini aliwahi kutuma ujumbe wa vitisho kwa wajumbe waliokuwa wakiwateua Wabunge wa bunge la Somalia mwezi Julai mwaka jana na kuwakosoa katika hotuba yake ya mkusanyiko wa half a ya Eid shere za Eid.

Chanzo cha picha, Getty Images
3. Jehad Serwan Mostafa
Kwa mujibu wa tuvufi rasmi ya serikali ya Marekani Jehad Serwan Mostafa anaaminika kuwa raia wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani anayepigana na kundi la kigaida la al-Shabaab, lenye makao yake nchini Somalia.
Inaaminika kuwa Mostafa alijiunga na al-Shabaab takriban 2006 na amehudumu katika nyadhifa tofauti, ikiwa ni pamoja na kuwa mwalimu wa kijeshi katika kambi za mafunzo za al-Shabaab, kiongozi wa wapiganaji wa kigeni, kiongozi na muenzaji propaganda katika tawi la vyombo vya habari la al-Shabaab, mpatanishi kati ya al-Shabaab na mashirika mengine ya kigaidi, na kama kiongozi katika matumizi ya milipuko ya kikundi katika mashambulizi ya kigaidi.
Mostafa kwa sasa anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Wilaya ya San Diego, kusini mwa California kwa kula njama ya kutoa msaada wa kifedha kwa magaidina pia njama ya kutoa msaada wa nyenzo kwa shirika la kigaidi la kigeni

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wengine ambao majina yao yamefichuliwa na pia kuwekewa vikwazo ni pamoja na:
Abdullah Jeri- ambaye anasemekana kuwasilisha silaha kisiri kwa wanamgambo wa Al-Shabaab. Marekamiinamuelezea Jeri kama mkuu wa kitengo cha ununuzi wa silaha cha Al-Shabaab, anayehusika na uuzaji wa silaha katika masoko ya ndani na nje ya nchi, ambayo mengi yanaagizwa kutoka Yemen.
Khalif Adale - Anadaiwa kuwa mchangishaji wa fedha wa Al-Shabaab kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali.
Hassan Afgooye- anayesemekana kuwa kiongozi mkuu wa Al-Shabaab, ambaye anasimamia sekta ya fedha. Marekani ilitoa zawadi ya dola milioni 5 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake.
Abdikarim Hussein Gagaale - ambaye inasemekana aliwahi kuwa naibu mkuu wa idara ya fedha ya Al-Shabaab, na kufanya kazi chini ya Mahad Karate.
Abdi Samad - anaelezewa kama mwanachama wa Al-Shabaab mwenye uhusiano wa karibu na Baraza Kuu la kikundi.
Abdirahiman Nurey - anaelezewa kama kiungo kati ya Al-Shabaab na kampuni zinazomilikiwa na watu binafsi Wanachama watatu wa mtandao unaohusika na uhamisho wa silaha, waliyotajwa kama: Mohamed Hussein Salad (Salad), Ahmed Hasan Ali Sulaiman Mataan (Mataan), na Mohamed Ali Badaas (Badaas).
Katika siku za hivi karibuni, Marekani inaonekana kuzidisha hatua zake dhidi ya Al-Shabaab, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Marekani yakiendelea nchini Somalia.















