Chanjo ya HPV ni nini na ni nani anayeweza kuipata?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti unaonyesha kuwa chanjo ya HPV inaweza kupunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu asilimia 90.

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa wanawake duniani kote, na huwauwa zaidi ya watu 300,000 kila mwaka.

Chanjo ya HPV inaweza kuzuia vipi saratani?

Chanjo ya HPV ina uwezo wa kuzuia aina tisa za HPV.

Ni pamoja na mbili zinazosababisha karibu visa vyote vya saratani ya shingo ya kizazi, zile zinazosababisha saratani nyingi za njia ya haja kubwa, na saratani znyingine za sehemu za siri, kichwa na shingo.

Utafiti umeonyesha kuwa chanjo hiyo ina kinga dhidi ya maambukizi ya HPV kwa angalau miaka 10, ingawa wataalamu wanatarajia kinga hiyo kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Utafiti unaonyesha kuwa inaweza kupunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu 90%.

Nani anaweza kupewa chanjo ya HPV?

Chanjo ya HPV inafanya kazi vizuri zaidi ikiwa wasichana na wavulana wataipata kabla ya kupata HPV.

Hii ni kwa sababu chanjo inaweza tu kuzuia maambukizi, haiwezi kuondoa mwili wa virusi mara mtu anapopatwa na maambukizi.

Virusi hivyo vimeenea sana kiasi kwamba chanjo inapaswa kulenga watoto kabla ya kufanya ngono.

Chanjo hiyo inaweza kutolewa kama dozi moja au mbili, linasema shirika la afya duniani (WHO). Watu walio na mifumo ya kinga iliyopunguzwa wanapaswa kupokea dozi mbili au tatu, linaongeza.

HPV ni nini?

HPV (ni ufupisho wa virusi vya papilloma ya binadamu) ni jina la kundi la kawaida la virusi.

Kuna aina zaidi ya 100 tofauti za HPV na maambukizi hayasababishi dalili zozote - ingawa baadhi ya aina zinaweza kusababisha maumivu. Virusi hivi vinaweza kuonekana kwenye mkono wako, mguu, sehemu za siri au ndani ya mdomo wako.

Watu wengi, hata hivyo, hawatajua wameambukizwa na miili yao itaondoa virusi bila matibabu.

Aina za hatari za HPV, kwa upande mwingine, vinaweza kusababisha ukuaji wa tishu zisizo za kawaida ambazo zinaweza kusababisha saratani.

Ni nani anayepata HPV na anaambukizwa kwa njia ya ngono?

Ni rahisi sana kuvipata kwa kuwa vinaambukizwa sana na kwa haraka , kuwa na kuambukiza sana, na huenezwa kwa mgusano wa karibu wa ngozi.

Asilimia 80 ya watu huambukizwa virusi vya HPV wakiwa na umri wa miaka 25.

Katika visa vingi watu huambukizwa kwa miezi 18 hadi miaka miwili.

Sio ugonjwa wa zinaa, kwani hauenezwi na maji ya ngono, kwa njia sawa na magonjwa kama vile kisonono.

Hata hivyo, mara nyingi huambukizwa wakati wa mawasiliano ya ngono, ikiwa ni pamoja na mgusano.

Je, chanjo ya HPV imeenea kwa kiasi gani duniani kote?

g

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Ethiopia ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotoa chanjo ya HPV
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kiwango cha juu cha maambukizi ya HPV ya kizazi miongoni mwa wanawake ni kinapatikana katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara (24%), ikifuatiwa na Amerika ya Kusini na Caribbean (16%), Ulaya Mashariki (14%), na Kusini Mashariki mwa Asia (14%), inasema WHO.

Mipango ya uchunguzi ilisoyotosha , ufikiaji mdogo wa huduma za matibabu na kusita kwa chanjo zote zinachangia hili.

Rwanda ilikuwa moja ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha kampeni ya chanjo. Ilianzisha mpango huo mwaka 2011 wa kuwawezesha wasichana kupata chanjo mapema na kuanzisha uchunguzi wa shingo ya kizazi kwa wanawake.

Katika mwaka wa kwanza iliwafikia wasichana tisa kati ya 10 wanaostahili kupata chanjo hiyo, matokeo ambayo wataalamu wanayataja kama mfano kwa nchi nyingine.

Ingawa chanjo hiyo inaonekana kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya kizazi, sio kinga dhidi ya aina zote za HPV.

Hivyo ni muhimu kwa wanawake pia kufanya kipimo cha uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi ( Papsmears ) wa mara kwa mara wanapofikia umri wa miaka 25.

Unaweza pia kusoma:

Karibu asilimia 90 ya vifo vya saratani ya shingo ya kizazi viko katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, kwa mujibu wa WHO.

Katika nchi hizi, saratani ya shingo ya kizazi mara nyingi haitambuliwi hadi itakapofikia katika kiwango cha hali ya juu zaidi na dalili kuonekana.

Awali WHO lilisema inalenga kutokomeza ugonjwa huo "ndani ya karne ijayo" kwa kufikia asilimia 90 ya chanjo ya HPV ifikapo mwaka 2030.

Nchi 140 sasa zimeanzisha chanjo ya HPV, inasema.

Kiwango cha juu cha maambukizi ya HPV ya kizazi miongoni mwa wanawake ni kinapatikana katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara (24%), ikifuatiwa na Amerika ya Kusini na Caribbean (16%), Ulaya Mashariki (14%), na Kusini Mashariki mwa Asia (14%), inasema WHO.

Mipango ya uchunguzi ilisoyotosha , ufikiaji mdogo wa huduma za matibabu na kusita kwa chanjo zote zinachangia hili.

Rwanda ilikuwa moja ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha kampeni ya chanjo. Ilianzisha mpango huo mwaka 2011 wa kuwawezesha wasichana kupata chanjo mapema na kuanzisha uchunguzi wa shingo ya kizazi kwa wanawake.

Katika mwaka wa kwanza iliwafikia wasichana tisa kati ya 10 wanaostahili kupata chanjo hiyo, matokeo ambayo wataalamu wanayataja kama mfano kwa nchi nyingine.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi