Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 03.07.2024
Newcastle inamtaka Anthony Elanga, Arsenal wanamtazama Riccardo Calafiori, huku Matthijs de Ligt akiwa na hamu ya kutaka kuhamia Manchester United.
Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Nottingham Forest wa Uswidi Anthony Elanga, 22. (Teamtalk),
Arsenal wameipiku Juventus katika harakati za kumsaka beki wa Bologna Riccardo Calafiori, 22, ambaye aliisaidia pakubwa Italia kwenye Euro 2024. (Telegraph - usajili unahitajika)
Matthijs de Ligt ana nia ya kuhamia Manchester United , huku Bayern Munich wakithamini beki huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24 kwa euro 50m (£42.4m). (Sky Sports)
Paris St-Germain wameulizia kuhusu mshambuliaji wa Leeds United na Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (De Telegraaf - kwa Kiholanzi)
Brighton wanavutiwa na kiungo wa kati wa Feyenoord na Uholanzi Mats Wieffer mwenye umri wa miaka 24 na beki wa pembeni wa Rayo Vallecano wa Romania Andrei Ratiu, 26. (Athletic - usajili unahitajika)
Manchester United wamefanya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirzkee, ingawa AC Milan tayari wamekubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 23 (Calciomercato - kwa Kiitaliano).
Manchester City wanajiandaa kumsajili winga wa Brazil Savio mwenye umri wa miaka 20 kutoka Troyes (Athletic-Usajili unahitajika),
Chelsea wamekubali ada ya £14m na Boca Juniors kwa ajili ya beki wa Argentina mwenye umri wa miaka 19 Aaron Anselmino.(Football.London)
West Ham have had a 35m euro (£26.9m) bid rejected by Nice for France defender Jean-Clair Todibo, 24. (L'Equipe - in French), external
Ofa ya West Ham ya euro 35m (£26.9m)imekataliwa na Nice kwa ajili ya mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Borussia Dortmund itamnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, ikiwa watashindwa katika majaribio yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kutoka Brighton . (Sky Sports Ujerumani)
Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Harry Maguire msimu huu wa joto, huku vilabu vya Italia vikiwa vinamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, 31 (Talksport),
Beki wa Swansea Nathan Wood atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huko Southampton baada ya vilabu hivyo kukubaliana ada ya pauni milioni 5 kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza wa kikosi cha chini ya umri wa miaka 21, (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Aston Villa Philippe Coutinho anatarajiwa kuondoka Villa wiki hii, huku Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 32 akitamani kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Vasco da Gama. (Birmingham Live)
Manchester United haijafutilia mbali uwezekano wa kumruhusu mshambuliaji Mwingereza Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 26 kuondoka msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)
Burnley wanatazamiwa kumteua meneja wa zamani wa Fulham Scott Parker kama meneja mpya wa klabu hiyo. (Football Insider)
Wolves inamfuatilia kiungo wa Juventus Arthur Melo kabla ya uwezekano wa kumnunua Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27. (Birmingham Live)
West Ham wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa na chini ya miezi 12 kwenye mkataba wake wa sasa. (Metro)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah