Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kesi gani ya uhalifu ambayo inaweza kuwa ngumu zaidi kwa Trump kushinda?
Mashtaka matatu, mashtaka 78, kesi tatu. Je, utetezi wa Donald Trump unaweza kuwa upi mahakamani na ni kesi gani kati ya hizo tatu itakuwa ngumu kwake kushinda?
Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa uhalifu mwingi. Kupanga njama ya kupindua uchaguzi wa urais wa 2020. Kuhujumu haki ya Wamarekani ya kupiga kura.
Kuhifadhi hati za siri katika mali zake mbili. Kutumia njia za ulaghai kumlipa mwigizaji wa filamu wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2016.
Anakabiliwa na karibu makosa 80 katika majimbo matatu na pengine zaidi ikiwa, kama inavyotarajiwa, atashtakiwa kwa kuingilia uchaguzi nchini Georgia.
Tumeona kesi ya upande wa mashtaka ilivyoainishwa katika mashtaka lakini tunajua nini kuhusu jinsi Bw Trump - ambaye anakanusha makosa yoyote - atajitetea katika kesi hizo mwaka ujao?
Je atafanikiwa kujinasua?
Mashtaka yenye nguvu zaidi yanapatikana katika kesi ya hati za siri za Florida, wataalam wa sheria wameambia BBC.
"Ingawa ni kesi yenye nguvu zaidi kisheria - baraza la wazee wa mahakama linaweza kumuondolea mashtaka hayo," alisema Anthony Michael Kries, profesa wa sheria za uchaguzi na ajira katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Georgia.
Idara ya Haki imemshutumu Bw Trump kwa kuchukua kinyume cha sheria nyenzo za kuainishwa katika Ikulu ya White House baada ya kuondoka ofisini, na kuzihifadhi isivyofaa katika jumba lake la kifahari la Mar-a-Lago na kisha kuzuia majaribio ya mara kwa mara ya serikali ya kutaka kurejesha hati hizo.
Sheria ya Marekani inawataka marais wanaoondoka kukabidhi nyenzo kama hizo kwa Hifadhi ya Kitaifa. Kuna sheria inayosimamia umiliki wa nyenzo zilizoainishwa. Viongozi wengine wa zamani, kama vile Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence, wamerudisha hati kama hizo mara tu walipozipata.
Kesi hiyo inatoa ushahidi mwingi dhidi ya Bw Trump, zikiwemo picha za masanduku yaliyohifadhiwa kiholela nyumbani kwake Florida.
Waendesha mashtaka pia walipata sauti ya Bw Trump akiongea kuhusu hati iliyoainishwa mbele ya watu bila kibali kinachostahili, na kukiri kwamba hangeweza kufichua nyenzo hizo kwa vile alikuwa ameondoka madarakani.
Bw Trump amedai kimakosa hadharani kwamba angeweza kughairi nyaraka hizo.
Alikana mashtaka ya kesi yake ya kufikishwa mahakamani huko Miami mwezi Juni na ameutaja upande wa mashtaka kuwa na msukumo wa kisiasa.
Lakini anaweza kupata upendeleo kutoka kwa baraza la wazee wa mahakama la serikali .
Bw Trump anapendwa na kuchukiwa sawa katika eneo la kusini mwa Florida na wataalam wa sheria wanaoishi huko wanasema kuwa kuchagua baraza la mahakama bila upendeleo kunaweza kuwa changamoto.
"Kipengele kilichoongezwa ni watu wenye ajenda," Rob Mendell, wakili wa kesi ya Florida, aliiambia BBC mwezi Juni.
Kesi inayoyumba sana
Kesi ya kwanza ambayo Bw Trump alikabiliwa nayo mwaka huu inaweza kuwa ya moja kwa moja kwake kushinda.
Mnamo Machi, waendesha mashtaka wa New York walitoa mashtaka 34 ya uhalifu wa kughushi rekodi za biashara. Haya yanahusiana na malipo ya pesa ya $130,000 ambayo wakili wa Bw Trump alimpa nyota wa filamu katika wiki za mwisho za kampeni za uchaguzi wa 2016.
Pesa hizo zilikuwa za kumzuia kuzungumza kuhusu madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi, uhusiano uliokanushwa na rais huyo wa zamani.
Wakili wa wilaya ya Manhattan Alvin Bragg anadai kuwa Bw Trump alitekeleza malipo hayo kupitia wakili wake, Michael Cohen, na kurekodi malipo hayo kwa njia ya ulaghai kama gharama za wakili.
Kwa kawaida, kughushi rekodi za biashara kunaweza kuwa kosa. Lakini iwapo wangedanganya na kufanya uhalifu mwingine, hiyo inaweza kuwa hatia.
Bw Bragg hahitaji kuthibitisha kuwa Bw Trump alitenda kosa moja ili kupata hatia ya uhalifu. Bado hajasema kwa uhakika nadharia yake kamili ya uhalifu wa ziada ni nini.
Lakini alidai wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwezi Aprili kwamba Bw Trump alifanya malipo hayo "ili kuficha uhalifu uliohusiana na uchaguzi wa 2016", hali iliomfanya kukiuka kulipa kodi.
Kundi la mawakili wa Bw Trump limefanya mabadiliko ya kesi hiyo kutoka kusikilizwa katika mahakama ya jimbo hadi mahakama ya shirikisho na huenda ikajaribu kufuta mashtaka.
Hapo awali waliteta kuwa Bw Trump alifanya malipo hayo ili kuokoa familia yake kutokana na aibu, wala si kutenda uhalifu.
Uamuzi wa Julai wa jaji wa shirikisho kukataa jaribio la Bw Trump kupeleka kesi katika mahakama ya shirikisho ulikuwa "ushindi wa 100% kwetu," Bw Bragg aliambia kituo cha redio cha WCBS wiki hii.
Jaji wa serikali pia aliashiria kuunga mkono jaribio la wakili wa wilaya kuinua uhalifu huo kuwa makosa.
Kesi ngumu kuikabili
Wiki iliyopita, Idara ya Haki ilimshtaki Bw Trump kwa makosa manne yanayohusiana na udanganyifu katika uchaguzi. Ni kisa ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kinachomhusisha rais anayedaiwa kujaribu kutumia vishawishi vya serikali kung'ang'ania madaraka.
Anashutumiwa kwa kuwashinikiza maafisa wa uchaguzi na makamu wa rais kubadili matokeo ya uchaguzi wa 2020, ambao alishindwa na Joe Biden.
Pia anashutumiwa kwa kueneza habari potofu kwamba uchaguzi uliibiwa, ambayo hatimaye ilisababisha ghasia za Bunge la Marekani.
Baadhi ya wataalam wa sheria wanafikiri kwamba ushahidi mwingi, mamlaka isiyo na huruma ya Washington DC, na jinsi Wakili Maalum Jack Smith alivyounda kesi hiyo yote yanamaanisha kuwa ni vita vikubwa kwa Bw Trump.
"Ukiukaji wa uchaguzi katika DC - nadhani hiyo ni itakuwa vigumu kisheria," alisema Bw Kreis. "Nadhani hiyo inaweza kuwa ngumu zaidi [kwa Trump] kushinda."
Jambo moja muhimu ambalo Bw Trump anaweza kupigana nalo ni suala la nia, ikiwa kweli alipanga kutekeleza uhalifu huu au la. Waendesha mashtaka watalazimika kuonyesha kuwa Bw Trump alitoa madai ya uwongo akijua alitaka kufanya uhalifu.
"Mtu anapaswa kujua kwamba ni uongo, na kisha kwa makusudi, kutoa taarifa hiyo kwa makusudi, kwa madhumuni ya kushawishi shughuli za serikali," Morgan Cloud, profesa katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Emory alisema.
Hilo ndilo la msingi, anaongeza Bw Kreis. "Je, Donald Trump aliamini kwa uaminifu na kwa ufahamu wake kwamba uchaguzi ulikuwa wa udanganyifu na kwamba alikuwa ameshinda?"
Bw Smith alipata uchungu mkubwa katika hati ya mashtaka kuonyesha mara kadhaa ambapo wasaidizi wakuu na washirika walimwonya Bw Trump kwamba madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi yalikuwa ya uwongo, lakini akaendelea.
Wakili wake John Lauro alisema rais huyo wa zamani aliamini “moyoni mwake” kwamba alishinda uchaguzi na upande wa mashtaka hautaweza kuthibitisha vinginevyo.
Mteja wake alikuwa akishambuliwa kwa kutekeleza haki yake ya Marekebisho ya Kwanza ya uhuru wa kujieleza, aliongeza, na maombi yake kwa maafisa wa uchaguzi yalikuwa "ya matarajio".
Kuna nafasi kubwa, hata hivyo, kwamba Bw Trump hawezi kutegemea hoja huru ya kujieleza. Baadhi ya aliyosema yanaweza kulindwa na Marekebisho ya Kwanza, alisema Aziz Huq wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Chicago.
Lakini, aliongeza, "hotuba ambayo inatumiwa kuwezesha uhalifu haipatikani kamwe".
Bw Smith alitoa hoja hii katika mashtaka, kwamba ingawa Bw Trump anaweza kusema kwa uhuru anachopenda kuhusu matokeo ya uchaguzi, hawezi kutumia imani hiyo kujaribu kubatilisha matokeo.
Lakini sio kila mtu anaamini kuwa kesi hiyo itasababisha hatia.
Sarah Isgur, mtoa maoni wa kisheria katika tovuti ya kihafidhina The Despatch, aliiambia Economist sheria ambazo hesabu hizi zililetwa zinahitaji uthibitisho wa nia. Hii ina maana ukweli kwamba watu walikuwa wakimwambia madai yake si ya kweli haitoshi, alisema.
Bw Trump pia anaweza kuelekeza kwa mawakili kama John Eastman na wengine waliokuwa wakimwambia madai yake yalikuwa sahihi, aliongeza.
Kadi isiotabirika – Baraza la wazee wa mahakama
Bila kujali jinsi pande zote mbili zinavyobishana katika kesi hiyo, lazima zishawishi baraza la wazee wa mahakama.
Na ni tofauti hii ambayo wataalam wa sheria wanasema ni ngumu sana kutabiri.
Mamlaka nne tofauti zinazochezwa - Washington DC, Florida, Manhattan na uwezekano wa Georgia - zitashawishi mienendo minne tofauti ya baraza la wazee wa mahakama.
Kizingiti cha kuhukumiwa hakina shaka yoyote na ni lazima maamuzi yawe ya pamoja, mambo mawili yanayompendelea Bw Trump.
"Hakika hiyo itarahisisha kesi ya Trump," asema Bw Kreis. "Haitaji kuwashawishi watu 12 ... wanahitaji mtu mmoja tu."
Tofauti nyingine kubwa ni Bw Trump mwenyewe.
Kinadharia angeweza kuchelewesha hukumu yoyote kwa kukata rufaa, kushinda urais, na kushinikiza Idara ya Haki kuacha uchunguzi wake.
Au hata, kama alivyoripotiwa kutafakari siku za nyuma, ajisamehe mwenyewe.