Je! tunajua nini kuhusu silaha ya Vita vya Pili vya Dunia ambayo Hamas iliitumia kupita ulinzi wa Israeli?
- Author, Mohammad Hamdar & Hanan Razek
- Nafasi, BBC News Arabic
- Muda wa kusoma: Dakika 5

Chanzo cha picha, Hamas
Wakati Hamas walipoanzisha shambulio la siku ya Jumamosi dhidi ya Israel, wapiganaji wavamizi walijumuisha wale waliokuwa wakivuka mpaka.
Vikosi vya “Izz al-Din al-Qassam” - mrengo wa kijeshi wa wa vugu vugu hilo - ulifanya mashambulizi dhidi ya watu waliokuwa wakijivinjari na miji ya Israeli inayozunguka Ukanda wa Gaza. Iliita shambulio hilo la kushtukiza "Mafuriko ya Al-Aqsa."
Msemaji wa jeshi la Israel Richard Hecht alithibitisha kuwa wapiganaji wa Kipalestina walijipenyeza kwa "parachuti", bahari na nchi kavu.
Picha na kanda za video zilizoshirikishwa kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha Vikosi vya Al-Qassam vikishuka kwa parachuti. Ni mara ya kwanza wanasadikiwa kutumia mbinu hiyo katika uvamizi wa Israel.

Chanzo cha picha, Hamas
Kuvuka uzio wa mpaka kupitia angani
Wanamgambo wa Kipalestina waliweza kuvuka uzio unaotenganisha Gaza na Israel kwa ndege, wakitumia parachuti zilizobeba kiti cha mtu mmoja au wawili.
Zikitumia jenereta na vipeperushi vya vyuma viliongozwa vikielekea katika eneo linalozunguka Ukanda wa Gaza.

Chanzo cha picha, Reuters
Mbinu ya Vita vya Pili vya Dunia
Parachuti za kijeshi hutumiwa mara kwa mara kupeleka vifaa vya matumizi kwa vitengo vya jeshi, kwa lengo la kupenya safu za adui nyuma ya uwanja wa vita.
Timu za miamvuli zilitumwa kwa mara ya kwanza kupigana na nchi zinazopigana za Ujerumani na Washirika wakati wa Vita vya pili vya dunia.

Chanzo cha picha, Getty images
Mashambulizi ya 1987 ya ndege za miavuli (glider)
Shambulio la Hamas Jumamosi lilizua kumbukumu ya oparesheni ya kurusha ndege iliyofanywa na Wapalestina wawili, Msyria, na Mtunisia kutoka kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine - Kamandi Kuu.
Waliondoka Lebanon na kushambulia eneo la kijeshi la Israeli mnamo Novemba 1987.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashambulizi ya Ardhini
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa kutumia miamvuli iliyo na injini na vidhibiti vya kuelekeza, wapiganaji hao waliweza kurusha makombora kutoka chini.
Hii ilimaanisha kuwa wangeweza kusafiri bila haja yoyote ya kupanda kilima au kushushwa kutoka kwa ndege.
Injini husaidia kuipa mwavuli nguvu ya kusukuma hadi 56km kwa saa.
Paraglider wanaweza kuruka kwa saa tatu, kwa wastani wa mwinuko wa mita 5,000 juu ya ardhi.
Wanaweza kubeba hadi kilo 230 - au sawa na watu 4 - kulingana na tovuti za paragliding.
Ndege hii inayofanana na mwavuli inaweza kuwa na kiti cha mtu mmoja au mkokoteni wa magurudumu matatu ambayo inaweza kuchukua watu wawili.
Klipu za video zilizotumwa na "Vyombo vya Habari vya Kijeshi" vya vikosi vya Izz al-Din al-Qassam, zikionyesha waendeshaji wa ndege wakirushwa kutoka ardhini, kila moja ikiendeshwa na mpiganaji mmoja au wawili.
Picha nyingine zinaonyesha wapiganaji wakifyatua risasi kutoka angani, kabla ya kutua na kuvamia maeneo ya Israel. Baadhi ya myavuli zilikuwa zimebeba wapiganaji kwenye pikipiki.
Hamas ilikiita kikundi cha askari wa miamvuli waliopenya uzio wa kujitenga "Saqr Squadron".

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa nini jeshi la Israel halijagundua parashuti hizo?
Sehemu za video zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Hamas zinaonyesha askari wa miavuli wenye silaha wakiruka kutoka Gaza wakati mashambulizi makubwa ya roketi yakiendelea kutoka Ukanda huo.
Baadhi yao walionekana kuruka katika mwinuko wa chini, huku wengine wakiwa juu zaidi angani.
Waliweza kuonekana wazi kwa macho katika anga inayozunguka Gaza.
Vyombo vya habari vya Israel vimehoji ni kwa nini vitengo vya jeshi vilishindwa kuwagundua.
Vikosi vya Israel bado havijafichua kwanini ulinzi wao wa angani haukuchochewa na wapiganaji waliokuwa wakivuka mpaka kupitia angani - huku miamvuli ikionekana kuwa kubwa kiasi kwamba watu walizirekodi kwenye simu zao.

Chanzo cha picha, EPA
Iron Dome
Je, Waisraeli wamekuwa wakitegemea sana teknolojia badala ya kutumia doria za mstari wa mbele?
Baadhi ya ripoti zimependekeza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel, kama vile Iron Dome na rada, haikuundwa kushughulikia vitu vidogo hivyo vinavyoruka.

Chanzo cha picha, Reuters
Mashambulizi ya pande nyingi
Hamas ilianza mashambulizi yake ya kushtukiza kwa kurusha roketi 5,000, kulingana na taarifa ya Kamanda wa vikosi vya Al-Qassam Muhammad Al-Deif siku ya kwanza.

Chanzo cha picha, EPA
Urushaji wa roketi uliambatana na uvamizi wa wapiganaji wa Hamas ardhini na baharini, kwa kutumia boti zenye bunduki na angani kwa kutumia miamvuli.
Vyombo vya habari na ripoti za kijeshi zinaonyesha shambulio la parachuti na uwezo wake wa kupita ulinzi wa anga ilikuwa sababu kuu ya wanamgambo hao kujipenyeza ndani ya Israel.
Katika siku yake ya kwanza, shambulio hilo lilisababisha hasara kubwa na isiyokuwa ya kawaida miongoni mwa raia na wanajeshi nchini Israel.
Wapiganaji hao waliwateka nyara zaidi ya raia 100 wa Israel na wanajeshi, ambao Hamas sasa inatishia kuwaua.













