China na Marekani zinavyozozania madini za Amerika Kusini

madini

Chanzo cha picha, Getty Images

Zaidi ya nusu ya madini ya lithiam duniani inapatikana Argentina, Bolivia na Chile, pembetatu ya masoko ambayo yamevutia wawekezaji na serikali za kitaifa.

Nchi kama China na Markani zinatafuta kupata vifaa vya chuma muhimu kwa utengenezaji wa betri zinazotumiwa na magari ya umeme, soko linalokua ambalo limevutia wawekezaji wengi zaidi.

"Mamlaka kuu zinapigania kupata madini muhimu kwa mpito wa nishati na Amerika ya Kusini ni uwanja mkuu wa vita," Benjamin Gedan, mkurugenzi wa Mpango wa Amerika Kusini wa Kituo cha Wilson, aliiambia BBC.

"Marekani ilichelewa kwenye karamu na Washington ina wasiwasi kwamba China imetangulia mpango huo," anaongeza.

Makampuni ya China yametumia miaka mingi kutafuta mahali pa kuhifadhi madini hayo yanayoitwa dhahabu nyeupe katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa katika Amerika ya Kusini, ambako kuna akiba kubwa zaidi ya madini hayo.

Bolivia inaongoza katika orodha hiyo ikiwa na hifadhi inayokadiriwa kuwa tani milioni 21, ikifuatiwa na Argentina (milioni 19.3) na Chile (milioni 9.6), kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

gari la uchimbaji madini

Chanzo cha picha, Getty Images

Na Mexico, ingawa ina tani milioni 1.7 tu (iliyo nafasi ya tisa kwenye orodha), imekuwa kiungo muhimu katika eneo la Amerika ya Kaskazini, si tu kwa sababu ya ukaribu wake wa kijiografia na Marekani na Canada, lakini pia kwa sababu inakuwa kituo cha uzalishaji wa magari yanayotumia umeme (hasa baada ya tangazo la hivi majuzi kwamba kampuni kubwa za magari kama vile Tesla na BMW zitaanzisha viwanda huko).

Mpango wa Chile

Chile ni nchi ya pili duniani kwa uzalishaji wa madini ya lithiam baada ya Australia.

Kufikia sasa, unyonyaji wa rasilimali hiyo umekuwa mikononi mwa kampuni za kibinafsi, lakini mpango mpya uliowasilishwa na Rais Gabriel Boric unatazamia kubadilisha mtindo huu wa biashara na kujiwekea faida ya hiyo Dhahabu Nyeupe nchini.

Pesa nyingi zinazotokana na madini kama vile lithiam hazitokani na uchimbaji wa rasilimali ghafi, lakini kutokana na kuongeza thamani baadaye katika mnyororo wa usambazaji bidhaa - kwa kutumia lithiam kutengeneza betri za umeme, kwa mfano.

Rais wa Chile anatazamia kuanzisha ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ambapo serikali inashikilia hisa inayodhibiti, na kukuza maendeleo ya kiteknolojia ili kuiweka Chile ndani ya msururu wa ugavi wa sekta inayositawi.

Lakini hii haitakuwa changamoto rahisi, kwani sehemu kubwa ya dunia inajaribu kunyakua kipande kikubwa cha mkate huo.

'Shughuli mbaya'

Jenerali Laura Richardson, kamanda wa Kamandi ya Kusini mwa Marekani, alionya kwamba China "inaendelea kupanua ushawishi wake wa kiuchumi, kidiplomasia, kiteknolojia, habari na kijeshi katika Amerika ya Kusini na Caribbean," wakati alipofika mbele ya Kamati ya Huduma za Silaha ya Baraza mnamo Machi kuwasilisha ripoti yake.

Jenerali Laura Richardson

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jenerali Laura Richardson, kamanda wa Kamandi ya Kusini mwa Marekani

“Eneo hili limejaa rasilimali nyingi na nina wasiwasi na vitendo viovu vya wapinzani wetu wanaojinufaisha kwa kujifanya wanawekeza kumbe wanafanya shughuli ya uchimbaji,” alisema.

Akizungumzia juu ya "pembetatu ya lithiam" ya Amerika Kusini - inayojumuisha Argentina, Bolivia na Chile, alisema kuwa "uchokozi wa China na njama ya kunyakua lithiam ni ya hali ya juu na ni kali sana".

China inasema nini?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Chini ya Rais Xi Jinping, China inawekeza katika miradi mikubwa ya lithiam huko Amerika Kusini

Waziri wa Maliasili Wang Guanghua amesema, "China ina utegemezi mkubwa wa kigeni kwa baadhi ya rasilimali muhimu za madini, na mara hali ya kimataifa itakapobadilika, hakika itaathiri usalama wa kiuchumi au hata usalama wa taifa," Waziri wa Maliasili Wang Guanghua alisema mapema Januari katika mahojiano na shirika la habari la kitaifa, Xinhua.

Serikali imejumuisha madini 24 ya kimkakati katika Mpango wake wa Kitaifa wa Rasilimali ya Madini, uliochapishwa mwaka 2016.

Baadhi ya madini hayo ni pamoja na chuma, shaba, aluminium, dhahabu, nikeli, cobalt, lithiam, na ardhi adimu, pamoja na rasilimali za jadi za nishati kama vile mafuta, gesi asilia, gesi ya shale na makaa ya mawe.

Mpango huo unabainisha kuwa madini ni muhimu katika "kulinda usalama wa uchumi wa taifa, usalama wa ulinzi wa taifa, na maendeleo ya viwanda vinavyoibukia kimkakati".

Ongezeko kubwa la uwekezaji wa China

Wakati makampuni ya China yanaendelea katika Amerika Kusini na uwekezaji mkubwa wa madini, nchi tatu zilizo na idadi kubwa ya madini ya hayo zinakusudia kuchukua fursa ya teknolojia na mtaji wa makampuni ya Kichina ili kukuza maendeleo ya viwanda vya ndani.

Katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu pekee, makampuni ya China yametia saini mikataba kabambe ya kuwekeza katika nchi za Bolivia, Argentina na Chile.

Rais Xi Jinping

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chini ya Rais Xi Jinping, China inawekeza katika miradi mikubwa ya lithiam huko Amerika Kusini

Katika miezi mitatu iliyopita, China imetangaza uwekezaji mkubwa katika Amerika ya Kusini.

Nchini Bolivia, makampuni ya Kichina ya CATL, BRUNP na CMOC yamejitolea karibu dola bilioni mja ($1bn) katika miradi ya lithiam katika idara za Potosí na Oruro, kulingana na Taasisi ya washauri wa Atalantiki wa masuala ya kibiashara na kiuchumi.

Nchini Argentina, kampuni ya Chery Automobile itawekeza kiasi cha dola milioni 400 katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza magari ya umeme, ikiwezekana huko Rosario.

Na nchini Chile, Tsingshan Holding Group, Ruipu Energy, Battero Tech, na FoxESS wamejitolea kuwekeza katika bustani ya viwanda vya lithiam katika jiji la Antofagasta, kwa kiasi ambacho bado hakijajulikana.

Uhusiano wa kibiashara kati ya Argentina na Uchina umezidi kuwa wa karibu katika uchimbaji madini ya lithiam, na tangazo la angalau miradi tisa ya uwekezaji mnamo 2022 pekee katika maeneo ya Salta, Catamarca, na Jujuy.

Ushindani wa kiteknolojia na kijiografia kati ya mataifa makubwa

Kulingana na mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Amerika ya Kusini cha Adrienne Arsht cha Taasisi ya Sera ya Atlantiki, Pepe Zhang, "Marekani inatafuta kikamilifu kuimarisha nafasi yake katika usambazaji wa kimataifa na ugavi wa madini muhimu na teknolojia ya kijani."

Hii ina maana kwamba "lithiam inathibitisha kuwa eneo muhimu zaidi katika ushindani wa kiteknolojia na kijiografia kati ya Marekani na China," aliiambia BBC.

Na China inapiga hatua kwa kasi katika.