Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph

Chanzo cha picha, Reuters
Makubaliano ya muda yaliyoafikiwa kati ya Hamas na Israel yanaingia siku yake ya tatu, na mchakato wa kubadilishana mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina unaendelea huku kukiwa na matarajio ya tahadhari kati ya pande hizo mbili kuhusu kitakachotokea baada ya kumalizika kwa siku nne za kusitisha mapigano.
Magazeti ya leo yanafuatilia mabadilishano hayo na mijadala ya pande zote mbili na duniani kote.
Gazeti la Uingereza The Telegraph lilifuatilia kuwasili kwa mateka na wafungwa kwa familia zao, na Jake Wallis Simons aliandika makala ya maoni kuhusu “Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyobadilisha ulimwengu milele.''
Mwandishi huyo anasema kwamba kabla ya Oktoba 7, taasisi ya usalama ya Israel na raia wa kawaida walikuwa katika hali ya kuridhika sana na kwenye usingizi mzito kabisa kuhusiana na tishio linalotoka Gaza baada ya takribani muongo mmoja bila vita vya ardhini katika ukanda huo.
Kila mtu aliamini kwamba tishio la makundi ya Wapalestina huko Gaza linaweza kudhibitiwa, licha ya mgawanyiko mkubwa ndani ya Israeli, ambao ulichochewa na kurudi kwa Benjamin Netanyahu madarakani, na kushinikiza maelfu kuandamana kila Jumamosi, na makampuni ya teknolojia na wawekezaji kuondoka nchini.
Uzio wa mpaka wa mabilioni ya dola, mfumo wa makombora wa Iron Dome, jeshi la anga, na uwezo wa kutisha wa kijasusi uliipatia Israeli kizuizi kikali na, isipokuwa mashambulizi machache, ilifanikiwa kuwaweka raia wa Israeli salama.
Ikiendana na nguvu hii kubwa iliyoongezeka, kulikuwa na majaribio ya Israeli ya kuleta utulivu ukanda huo, kulingana na mwandishi, na makumi ya maelfu ya wafanyakazi wa Gaza waliruhusiwa kuvuka Israeli kila wiki kufanya kazi.
Maji, malori ya chakula na rasilimali zingine pia ziliruhusiwa kuingia kufidia matumizi ya Hamas ya pesa zake kujenga mahandaki.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Badala yake, hali ya kuridhika iliyokuwepo nchini Israeli, mwandishi anaongeza, iliwafanya Wasaudi kufikiria juu ya makubaliano ya kuhalalisha, na matumaini yaliyopo katika sehemu nyingi ni kwamba kufikia suluhu la kisiasa katika eneo hilo kunaweza siku moja kudhoofisha tishio lolote la baadaye.
Kwa kweli, mwandishi anasema kwamba chanzo kilimwambia kwa wasiwasi, "Kama Iran ingeelekeza mashambulizi, Mossad wangejua kuyahusu." Wiki mbili kabla ya milango ya kuzimu kufunguka, ikimaanisha Oktoba 7, rubani wa wasomi wa Israeli alisema katika mahojiano na Jewish Chronicle kwamba atafanya uvamizi dhidi ya vitisho vilivyopo vinavyoletwa na Hezbollah au Iran, lakini ujumbe juu ya Gaza ungemfanya kusitasita, na kuongeza, "Hapana." "Nadhani kutakuwa na vita kesho".
Saa 6:30 asubuhi mnamo Oktoba 7, yaliyokuwa yakisemwa yakatimia. Haukupita muda mrefu marubani hao walirejea katika anga ya Gaza na nchi hiyo ikagundua tena mshikamano wake chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.
Maandamano ya mitaani yalisahaulika na siku hiyo ilikuwa ni hatua muhimu katika historia ya Israeli, eneo hilo na kwa kiasi fulani dunia nzima.
Israeli daima imekuwa na mtazamo wa kipekee kuhusu uhuru wa wafungwa wake, kama ilivyooneshwa mwaka 2011, ilipobadilishana wafungwa 1,027 wa Kipalestina badala ya mwanajeshi aliyetekwa nyara Gilad Shalit.
Kwa ulimwengu wa nje, hii inaweza kuonekana kuwa ya kutatanisha, lakini jeshi la Israeli ni tofauti. Kila mtu anajua kwamba juhudi za hali na mali zitafanyika ili kuhakikisha kurudi kwa mwanajeshi mmoja, awe hai au amefariki.
Lakini Hamas imekuwa hodari katika kugeuza ubinadamu wa Israeli wasiwasi wake kwa wanajeshi na raia wake dhidi yake yenyewe, kulingana na mwandishi, na Hamas inatumai kuwa mateka hao pia watatumika kuzuia, kuchelewesha na hatimaye kusimamisha kulipiza kisasi kwa Israeli, kuruhusu kundi hilo kurudia "mauaji," kama mmoja wa viongozi wake alivyosema, Ghazi Hamad, "Mafuriko ya Al-Aqsa ni mara ya kwanza tu, na kutakuwa na mara ya pili, ya tatu, na ya nne kwa sababu tuna dhamira na uwezo wa kupigana.”
Mwandishi anaeleza kuwa kutumia vibaya ubinadamu wa Israeli dhidi yake hakutafaulu safari hii. Hamas ilifanya makosa katika hesabu zake kwamba kama wafungwa 1,027 wangebadilishwa kwa mateka mmoja huko nyuma, mateka 240 wangeleta wafungwa 246,480 wa Kipalestina.
Pia ilikuwa makosa kudhani kwamba uhasama ungekoma kwa muda mrefu. Wakati huo huo, kumruhusu kupigana siku nyingine.
Kile ambacho Hamas imekuwa ikikosa siku zote ni ukweli kwamba Israel si nchi ya kikoloni kama Ufaransa, ambayo kuikalia kwa mabavu Algeria kuliishia vifo na maelfu kupata majeraha.
Waisraeli hawana nchi nyingine ya kujiondoa, kwani dola hiyo ya Kiyahudi imedhamiria kumshinda adui bila kujali gharama.
Kwa upande wa Israeli, kila kitu kilibadilika mnamo Oktoba 7. "Kwa kuwachinja watu wasio na hatia kwa ukatili kama huo na kuwachukua mateka wengi, wakiwemo watoto wachanga na walionusurika katika mauaji ya Holocaust," kulingana na mwandishi, Hamas walikuwa wamebadilisha hesabu za usalama bila kujua.
Sera ya kuzuia, ambayo kwa miongo kadhaa ilitumika kama sehemu kuu ya ulinzi wa Israeli, ilivunjwa.
Kwa Waisraeli wengi, kusitishwa kwa mapigano kwa siku nne ni gharama kubwa kulipa, wakijua kwamba kungewaweka wanajeshi wao katika hatari.
Aidha, upatikanaji wa mafuta na misaada mingine katika Ukanda huo bila shaka ungevamiwa na kutumiwa na Hamas.
Na kutoa nguvu mpya kwa wapiganaji wake na kuimarisha mtandao wake wa kwenye mahandaki, hata hivyo, hamu ya Israel ya kuwaokoa raia wake ilishinda.
"Ni kama athari za tetemeko la ardhi."

Chanzo cha picha, Reuters
Na kwa gazeti la Israeli la Haaretz na makala ya uchanganuzi ya mwandishi Shirin Falah Saab yenye kichwa "Usitishaji vita wa muda huwapa faraja kidogo wakazi wa Gaza ambao wanakabiliwa na ukweli mpya."
Mwandishi anaanza makala yake kwa maneno yaliyosemwa na Israa, mwalimu wa Kiingereza kutoka Gaza, katika mahojiano na gazeti la Haaretz: "Maisha hayarudi kuwa ya kawaida wakati wa usitishaji wa mapigano. Ni sasa tu ndipo tunapogundua ukubwa wa uharibifu."
Israa, ambaye aliolewa majira ya joto yaliyopita na kuhamia Beit Lahia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, anaongeza, "Natumai hakuna usitishaji vita," na maneno yake yanaonyesha kufadhaika na hasara kubwa aliyoipata katika siku ya kwanza ya usitishaji vita wa muda.
Kama raia wengi wa Gaza, aliibuka kutoka mafichoni na kupata picha halisi ya uharibifu.
Kufikia asubuhi na mapema ya Ijumaa, yeye na mume wake waliondoka Deir al-Balah, walipokuwa wakiishi tangu kuanza kwa vita, na kuelekea kaskazini.
Israa alisema, “Tulitembea kwa miguu ili kujua nini kimetokea kwenye nyumba yetu, sijui kwa nini tulichukua hatari kiasi hiki, kulikuwa na miili imetawanyika kando ya barabara, na tulipokwenda kaskazini tuliona uharibifu mkubwa.
Alipoulizwa kwa nini waliamua kurejea Ukanda wa Kaskazini wa Gaza, alijibu, "Nilitaka kuona ni nini kilibaki kwenye nyumba ambayo nilikuwa na ndoto ya kuanza maisha yangu mapya. Kila kitu kilikuwa magofu. Tulichukua baadhi ya vitu vya kibinafsi, baadhi ya mali na nguo chache. Vitongoji vyote vilikuwa nimeangamizwa.”
Alijaribu kuwasiliana na wazazi wake, baada ya kupoteza mawasiliano nao kwa muda wa wiki tatu.“Walisisitiza kukaa sehemu ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza, lakini tuliondoka. Sasa kwa siku chache zijazo tutatembelea shule zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa, kujaribu kuwatafuta.”
Ahmed mume wa Israa anasema mitaa ya Beit Lahia imeharibika, barabara kuu ya mji wa Al-Shaima ilipata uharibifu mkubwa kutokana na vifaru vya Israel vilivyokusanyika hapo. Anaongeza, “Uharibifu wa miundombinu haueleweki .
Wenzi hao wapya, waliokuwa wakiishi katika moja ya minara ya juu ya makazi huko Beit Lahia, walionekana kusikitishwa na kile walichokiona waliporejea kaskazini mwa Gaza.”
Israa inauliza, "Tatizo la Israel ni Hamas, Kwa nini kuwadhuru raia? Maisha yetu yameharibiwa, na familia zetu zimeharibiwa."
Ahmed anaongeza, "haiwezekani kuishi hapa. Ni kama mji wa mashetani. Tutarudi kuishi katika shule ya UNRWA." Watu hawatarejea eneo la kaskazini mwa Gaza hivi karibuni, kulingana na Ahmed.
Imetafsiriwa na Asha Juma na kuhaririwa na Seif Abdallah.












