Kwanini bandari ya Antwerp imekuwa lango la kupitishia cocaine barani ulaya?

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Jiji la Ubelgiji la Antwerp ni maarufu duniani kwa almasi. Lakini biashara nyingine ambayo inaanza kupata umaarufu sawa au yenye faida kubwa zaidi inachukua sifa ya almasi.

Bandari yake ni ya pili kwa ukubwa barani Ulaya, na ambayo mamilioni ya makontena hupita kila mwaka, imekuwa njia kuu ya kupitisha cocaine barani humo, ukiondoa pwani ya Galician kaskazini-magharibi mwa Uhispania, ambapo hadi miaka michache iliyopita, sehemu kubwa ya dawa hizo zilikuwa zinapitishwa huko.

Katika miaka mitano iliyopita, rekodi moja baada ya nyingine ilianza kubainika.

Mnamo 2022 pekee, mamlaka ya Ubelgiji ilibaini karibu tani 110 za dawa za kulevya, huku 23% zaidi ya mwaka uliopita, kulingana na data za hivi karibuni iliyotolewa na Huduma ya Fedha ya Umma ya Ubelgiji, taasisi inayosimamia forodha.

Idadi hiyo inawakilisha asilimia 40% ya cocaine zilizokamatwa Ulaya. Bandari ya pili ambayo inaingiza dawa kwa ukubwa ni bandari ya Uholanzi ya Rotterdam, ambapo mwaka 2022 tani 52.5 zilipatikana.

 Mamlaka ya Ubelgiji ilionya mwaka jana kwamba haina uwezo wa kuteketeza kiasi kibubwa kiasi hicho cha dawa zote zilizonaswa.

 Inakadiriwa, hata hivyo, kwamba kiasi hiki kinawakilisha tu sehemu ya kumi ya zote zinazofika bandarini.

Usafirishaji huja, zaidi kutoka Brazil, Ecuador na Colombia na hivi karibuni pia kutoka Panama na Costa Rica.

 Lakini ni nini kinachofanya bandari ya Antwerp kuwa mahali panapopendwa zaidi na magenge ya dawa za kulevya?

Msemaji wa Huduma ya Fedha ya Serikali, Florence Angelici anasema ni ukubwa wa bandari tu.

Ikiwa na 129 km2, bandari ya Antwerp ni kubwa kuliko jiji la Paris.

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ingawa uwezo wake ni mdogo kuliko Rotterdam katika Uholanzi, eneo lake la mbele linazidi sana eneo la jirani yake. Kwa sasa lina kilomita 160 , ikilinganishwa na 70 kwa bandari ya Uholanzi.

"Barabara zinapita ndani yake, kuna hata miji ambayo imebaki ndani kwa sababu bandari imekua sana, na hii inafanya kuwa na ugumu kufuatilia," Angelici alielezea BBC Mundo.

Ugumu wa kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya,kwa sababu wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao wanaweza kukusanya taarifa zote muhimu ili kuanzisha na kusimamia kupata dawa ya kulevya nje ya bandari.

Paul Meyer anaijua eneo hilo kama sehemu ya mkono wake.

Mholanzi huyu, ambaye alihukumiwa mwaka 2007 mpaka miaka 12 gerezani kwa kusafirisha kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kwenda Ulaya, sasa anajitolea kutoa taarifa ili kusaidia kupatikana kwa wasambazaji, yaani amekuwa sehemu ya bandari ya Antwerp (kwa maoni yake).

Katika siku za nyuma, yeye na kundi lake walijaribu kupenyeza dawa hizo kupitia bandari ya Ujerumani ya Hamburg au bandari ya Ufaransa ya Marseille, Huko Antwerp, anasema, ilikuwa rahisi kila wakati.

Katika siku za nyuma, yeye na kundi lake walijaribu kupenyeza dawa hizo kupitia bandari ya Ujerumani ya Hamburg au bandari ya Ufaransa ya Marseille. Huko Antwerp, anasema, ilikuwa rahisi kila wakati.

Hadi sasa, kuna mawakala 350 pekee wa forodha ambao wamejitolea kusimamia bidhaa zinazofika, idadi ambayo haitoshi ambayo itaongezwa, kulingana na msemaji wa Huduma ya Fedha ya Umma, na wengine 108 "ambao wanajitolea tu kudhibiti dawa za kulevya. "

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Matunda yanavyotumika kusafirisha dawa za kulevya

Pamoja na hayo, mvuto wa ufuatiliaji wake kuwa mgumu, anaongeza kuwa hii ni "njia ya kihistoria ya usafirishaji wa matunda kutoka Amerika ya Kusini hadi Ulaya. Bandari ina vituo vya jokofu la kila kitu kinachohitajika kupokea matunda," anaongeza Florence Angelici.

Njia hizi zilizoanzishwa, ambazo huhamisha mamilioni ya makontena kuvuka Bahari ya Atlantiki kila mwaka, zinachukuliwa na mitandao ya wahalifu, ambao hufaulu kuingiza cocaine kwenye makontena ambayo yatatumiwa barani Ulaya kwa hapo baadaye.

 Wafanyabiashara wa dawa za kulevya ni watu wa kufikiria, na desturi za Ubelgiji zimeona kila aina ya mbinu za kuficha dawa hizo.

"Wanatumia kila aina ya matunda, ndizi, kwa mfano, na kuweka cocaine katikati ya masanduku. Au wanatumia mananasi, wanatoboa na kuweka dawa ndani ya tunda," anasema Angelici. Aina hii ya chombo pia ni jokofu, "na katika mfumo huu wa baridi kuna shimo ambalo pia hutumiwa kuficha vifurushi."

Mabaki ya dawa za kulevya yamepatikana ndani ya vigogo vya mbao , anakumbuka msemaji huyo, "katika nguo ambazo zilikuwa zimepachikwa cocaine. Mawakala wa forodha walipofungua masanduku waliona nguo tu, lakini walipofanya udhibiti kamili waligundua dawa hizo zilikuwa kwenye tishu."

Hata hivyo, kutokana na ugumu wa kulinda bandari, mojawapo ya mbinu zinazotumiwa sana za kupitisha cocaine ni moja kwa moja zaidi.

Mfano kuna inayojulikana kama " rip on/rip off " , hii inajumuisha kuweka pakiti za cocaine juu ya bidhaa za kawaida kwenye vyombo, bila kuzificha, mara nyingi kwenye mifuko ya michezo ambayo inaweza kusafirishwa kwa urahisi. Mara nyingi, wasafirishaji hawajui kuwa mizigo yao imenaswa na walanguzi wa dawa za kulevya.

“Wanapofika bandarini kuna watu ndani ya vituo wanakuja haraka kuwatoa kwenye makontena wanaweza kuwa na kilo 100 au 200 lakini wananyumbulika sana,” anaeleza Angelici.

Wakati mwingine watu hawa badala ya kuzitoa dawa bandarini huzihamishia kwenye makontena mengine ambayo wanajua hayatafanyiwa ukaguzi ama kwa kuwa tayari yameshadhibitiwa au hayahitaji ukaguzi mfano yale yanayosafirisha mizigo kutoka nchi hadi nyingine ya Umoja wa Ulaya.

Kutoka Antwerp, ambayo iko katikati ya barabara ya ulaya, ni rahisi sana kufikia nchi ambazo itatumiwa, kama vile Ufaransa au Ujerumani.

Lakini kulingana na Europol, Shirika la Umoja wa Ulaya la Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria, sehemu kubwa ya dawa hii husafirishwa hadi Uholanzi, kutoka ambapo vikundi vya wahalifu vilivyoko huko huvisambaza kote Ulaya.

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuongezeka kwa matumizi

Dawa hizo zinapita licha ya idadi ya rekodi ya kukamatwa, na taasisi za Ulaya zinajua hili kwa sababu bei ya cocaine mitaani haijaongezeka na hata imepungua katika baadhi ya matukio.

"Tumeona kwamba katika Amerika ya Kusini, mbinu za kupata dawa zimebadilika. Sasa wana vyanzo ambavyo vilibadilishwa vinasaba na, badala ya moja, wanapata mavuno mara mbili au tatu kwa mwaka, "anasema Angelici.

Kwa kuzalisha zaidi, dawa zaidi zinaweza kusafirishwa. "Na kadiri tunavyokamata, ndivyo wanavyopoteza zaidi, kwa hiyo lazima watoe faida zaidi ili kufuta hasara hizi," msemaji huyo anasema. "Hii ni sababu nyingine kwa nini cocaine zaidi kuja."

Cocaine ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana barani Ulaya. Matumizi yake yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, kwa kiasi fulani kwa sababu bei yake imeshuka, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kuhusu soko la cocaine kutoka Kituo cha Ufuatiliaji cha Ulaya cha dawa za Kulevya, iliyotayarishwa na Europol.

Katika mitandao ambapo wananunua, watumiaji mara nyingi hupata ofa 2 kwa 1 , kama vile zile zinazoweza kuonekana kwenye maduka makubwa. Katika hali nyingi, sio lazima tena kwenda chini ya uchochoro. Ujumbe kupitia mitandao ya aina ya WhatsApp unatosha, na cocaine hutumwa nyumbani kwako.

Ripoti hiyo ilikadiria kuwa biashara ya cocaine barani Ulaya ilikuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 11.3 mnamo 2020, theluthi moja ya biashara zote za dawa za kulevya, na nyuma ya biashara ya bangi pekee.

Na pale ambapo pesa huongezeka kwa kiwango kikubwa, ndivyo uhalifu uliopangwa.

Antwerp, ambapo hadi hivi karibuni lilikuwa jiji tulivu kiasi, lakini katika miaka ya hivi karibuni mlipuko wa vurugu zinazohusiana moja kwa moja na magenge tofauti ya dawa za kulevya, kwa risasi na hata milipuko ambayo imewatia hofu wakazi wake.

Kifo cha kwanza kilikuwa msichana wa miaka kumi na moja, ambaye alikufa kwa kupigwa risasi wiki hii.

Katika miaka mitano iliyopita kumekuwa na hadi matukio 200 ya vurugu, jambo ambalo lilikuwa la kawaida katika nchi jirani ya Uholanzi, lakini sio Antwerp.

Miongoni mwa magenge ya kigaidi ambayo yanatawala biashara hiyo ni lile linalojulikana kama "Mocro Maffia" , linalotokea Uholanzi na kuhusika na mauaji mengi, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa habari wa uchunguzi wa Uholanzi Peter R. de Vries na wakili Derk Wiersun, akiwakilisha mtu ambaye angeenda kutoa ushahidi dhidi ya kundi hili. Zote mbili zilifanyika Amsterdam.

Hata Waziri wa Sheria wa Ubelgiji, Vincent Van Quickenborne, amelazimika kuimarisha usalama wake baada ya washukiwa wanne wa Uholanzi wanaodaiwa kupanga kumteka nyara kukamatwa.