Marekani sasa inasafisha mafuta ghafi ya Venezuela

    • Author, Samira Hussain & Nathalie Jimenez
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Meli ya Minerva Gloria imetia namba kwenye gati la Mississippi Sound, si mbali na akiba kubwa ya mafuta ya Marekani katika Ghuba ya Mexico.

Meli hiyo, yenye urefu wa futi 820 (mita 250, imebeba mizigo ya thamani kutoka Venezuela ambayo, miezi sita tu iliyopita, isingeweza kufikishwa Marekani – nayo ni mapipa 400,000 ya mafuta ghafi.

Venezuela ina akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani. Chini ya rais wa zamani wa Venezuela Nicholas Maduro, mauzo ya mafuta nje yalipungua sana, kutokana na ukosefu wa uwekezaji. Kisha vikwazo vya Marekani vikaja dhidi ya kuingiza mafuta katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Lakini Rais wa Marekani Donald Trump aliapa kutumia mafuta hayo baada ya jeshi la Marekani kumkamata Maduro katika shambulio la ghafla la usiku mwezi Januari.

Sasa mafuta yanaingia tena nchini Venezuela. Mwezi Machi mauzo ya nje ya mafuta ghafi ya kila mwezi nchini humo yalizidi mapipa milioni moja kwa siku. Hii ni mara ya kwanza tangu Septemba.

Huku dunia ikiyumba kutokana na athari za bei za nishati duniani zilizosababishwa na Iran kuzuia Mlango-Bahari wa Hormuz, makampuni makubwa ya mafuta na gesi kama Chevron sasa yanaagiza mafuta ghafi ya Venezuela kwa meli.

Mafuta ya Venezuela

"Ni jambo kubwa," anasema Tim Potter. Mkurugenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Chevron huko Pascagoula, Mississippi. Pia ni kampuni pekee kubwa ya mafuta ya Marekani inayofanya kazi nchini Venezuela kwa sasa.

Kwa pamoja hii ina maana kwamba Chevron inaweza kuchukua mafuta ya Venezuela, kuyachakata, na kuyapeleka moja kwa moja kwa watumiaji wa Marekani.

Mafuta ghafi ya Venezuela ni rahisi kununua kwa sababu ni magumu zaidi kuyachaka. Ni mazito sana, manene, meusi na yana salfa nyingi. Hutumika kutengeneza dizeli, petroli (petroli), mafuta ya ndege na bidhaa zingine.

Chevron sasa inaagiza mafuta ghafi ya Venezuela yanayofikia mapipa 250,000 kwa siku, anasema Andy Walz, rais wa Chevron.

Ingawa Chevron ndiyo kampuni pekee ya Marekani yenye uwezo wa kuchimba mafuta, wengine wananunua mafuta ya Venezuela kutoka kwa wazalishaji wa ndani.

Chevron pia sio kampuni pekee linapokuja suala la kusafisha mafuta nchini Marekani. Kuna viwanda 132 vya kusafisha mafuta nchini Marekani vinavyosafisha mafuta ghafi.

Marekani inaagiza mafuta machache sana kutoka Mashariki ya Kati, takriban 8% mwaka 2025. Ongezeko la uagizaji kutoka Venezuela linamaanisha kuna mafuta zaidi yatapatikana, ikimaanisha bei nafuu ya petroli itakuwa nafuu zaidi kwa madereva wa Marekani.

"Marekani huagiza mafuta kidogo sana kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, na haitaagiza mafuta yoyote katika siku zijazo kupitia mlango huo," alisema Rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake wiki iliyopita.

Lakini bei iko juu

Lakini maili chache tu kutoka kiwanda cha kusafishia mafuta cha Chevron, bei ya mafuta inaendelea kuongezeka.

Bei ya wastani ya galoni moja ya petroli katika sehemu hii ya Mississippi bado ni nafuu kuliko wastani wa bei kitaifa, kulingana na Chama cha Magari Marekani.

Kabla ya vita nchini Iran, mafuta yalikuwa nafuu, karibu dola moja kwa lita.

Katika hotuba hiyo hiyo, Rais Trump alisifu uwezo wa Marekani wa kuzalisha mafuta. "Sisi ndio wazalishaji nambari moja wa mafuta na gesi duniani, bila kusahau mamilioni ya mapipa tunayopata kutoka Venezuela."

Lakini upatikanaji wa akiba hiyo kubwa ya mafuta bado haujamaanisha iko bei iko chini kwa Wamarekani. Hiyo ni kwa sababu Marekani iko katika hatari ya kuathirika na bei ya soko la mafuta duniani kama nchi zingine.

"Ingawa bado tunaweza kupata mafuta ghafi yanayopatikana hapa kwenye kiwanda hiki cha kusafishia mafuta kwa sababu ya usambazaji wetu wa ndani, bei ya jumla ya mafuta hayo ghafi imepanda kwa sababu inategemea masoko ya dunia," anasema Potter.

"Mambo yatakaporejea katika hali ya kawaida, mafuta kutoka Venezuela yatasababisha bei ya chini kwa Wamarekani. Hali itakuwa hivyo katika siku zijazo," anasema Walz.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Ambia Hirsi