Video: Wanajeshi wa Israel waonekana wakisherehekea uharibifu wa jengo huko Gaza

Chanzo cha picha, MTANDAO WA KIJAMII
Hivi majuzi kuliibuka video inayowaonyesha wanajeshi wa Israel wanaozungumza Kiebrania wakishangilia na kucheka wakati wakilipua jengo moja ndani ya Gaza.
Mmoja wao anasema kwenye video, "Inafanyika hivi ili kusiwe na nafasi iliyobaki kwao kurudi."
Video hiyo, bila shaka, iliamsha hasira za watu wengi katika ulimwengu wa Kiarabu, haswa kwa kuzingatia uhamishaji wa wakaazi wa Ukanda wa Gaza kutoka kwa makazi yao, uhamisho wao kuelekea mpaka wa Misri, na shutuma zilizoenea kwamba Israel iliharibu miundombinu kwa makusudi huko Gaza.
Tuliwasiliana na jeshi la Israeli na lilisema linachunguza kile ilichoelezea kama matendo ya kesi za kibinafsi.

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kuna ukweli gani kuhusu video hiyo?
BBC Fact Check ilithibitisha uhalisia wa video hiyo na kwamba inahusiana na matukio ya sasa ya Gaza na si ya zamani.
Ilithibitisha pia kwamba kile kinachosemwa kwenye video kilitafsiriwa kwa Kiebrania.
Video hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye akaunti ya Facebook inayohusishwa na mwanajeshi wa Israeli anayeitwa Oren Shmuel, katika ujumbe uliojumuisha video zingine mnamo Januari 23.
Mwanajeshi huyu alikuwa sehemu ya kikosi cha Brigedi ya Golani kilichoshiriki katika vita vinavyoendelea ndani ya Gaza hadi kilipotolewa ndani ya Ukanda huo mnamo Desemba 21, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya jeshi la Israel, ambayo ilisema, "Jeshi la Israel linatoa vikosi vyake maalum 'kipindi cha kupumzika' katikati ya vita.''
Katika video nyingine iliyochapishwa katika chapisho sawa na video ya kwanza, wakati ambapo kikosi kilipokea habari za mwisho wa misheni yake ndani ya Gaza inaweza kuonekana.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Facebook ujumbe
Kutokana na uharibifu wa maeneo mengi muhimu katika eneo hilo ambapo video ilirekodiwa, hatukuweza kufahamu eneo halisi ndani ya Gaza, lakini tunajua kuwa Brigedi ya Golani ilishambulia wakati wa uwepo wake katika kitongoji cha Shujaiya huko mashariki ya ukanda wa Gaza, ambako kulitokea mauaji ya maafisa na wanajeshi kadhaa katika brigedi, kulingana na taarifa za jeshi la Israeli.
Brigedi ya Golani ni mojawapo ya brigedi za kwanza kujiunga na jeshi la Israel, Februari 1948, hivyo pia ina jina la "Brigade 1." Ni ya wanajeshi wanaotembea kwa miguu, na ni mojawapo ya vikosi vya wasomi katika jeshi.
Misheni kuu ya kikosi hiki ilikuwa kuwekwa kwenye mpaka wa Syria na Israel, kwenye mabonde na vilima vya Galilaya ya Chini.
Golani imeshiriki katika vita vya sasa vya Gaza tangu siku ya saba ya Oktoba 2023.
Israel inafanya uchunguzi
Tuliwasiliana na jeshi la Israeli ili kutoa maoni, na jibu lilikuwa kwamba jeshi la Israeli bado linachunguza vitendo vya kesi za kibinafsi, ambazo zinatofautiana na kile kinachotarajiwa kwa wanajeshi wa jeshi la Israeli. Hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wanajeshi wanaohusika na vitendo hivi.
Ameongeza kuwa, mafundisho ya jeshi la Israel hayalengi kudhuru miundo mbinu ya raia isipokuwa kwa mahitaji ya kijeshi na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Kuna utaratibu wa uchunguzi unaohusishwa na Mkuu wa Wafanyakazi ambao huangalia malalamiko ya ukiukaji na matendo ya wanajeshi wa jeshi la Israeli.
Hata hivyo, maoni hayakujumuisha jibu la moja kwa moja kwa maudhui ya video inayosambaa mitandaoni.












