Wanyama wanane walioangamia mikononi mwa binadamu

Dinosari walitoweka karibu miaka milioni 6.6 iliyopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dinosari walitoweka karibu miaka milioni 6.6 iliyopita

Tunaweza kufikiria kutoweka kwa spishi kuwa tukio la ghafla au la mara kwa mara, lakini ukweli ni kwamba kutoweka ni jambo la kawaida sana.

Kulingana na Hazina ya Wanyamapori wa Asili Duniani (WF), shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi kulinda wanyamapori, takriban spishi 10,000 hutoweka milele kila mwaka.

Lakini WWF linasema kwamba idadi halisi kujulikana kwa sababu bado hatujui ni spishi ngapi zinapatikana kote duniani.

Kwa kuwa ulimwengu huadhimisha Siku ya Viumbe Vilivyo Hatarini kuangamia kila Novemba 30, tunaangazia baadhi ya wanyama waliokuwa wingi katika sayari hii na sasa hawapo tena.

Wafuatao ni wanyama wanane ambao wameangamia kutokana na shughuli za binadamu katika makazi yao asilia na hatutawahi kuwaona tena.

1: Miss Waldron's Red Colobus (Ghana NA Ivory Coast)

Zanzibar red kolobus ndiye jamaa wa karibu zaidi wa Miss Waldron red colobus aliye hatarini kutoweka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zanzibar red kolobus ndiye jamaa wa karibu zaidi wa Miss Waldron red colobus aliye hatarini kutoweka

Tumbili huyu mwenye ukubwa wa kadri na mwenye nywele nyekundu amesadikiwa kutoweka tangu mwanzoni mwaka miaka ya 2000.

Miss Waldron's Red Colobus, anayeishi kwenye mpaka wa Ghana na Ivory Coast, alikuwa mmoja wa wanyama wa ajabu kwa sababu hakuwa na vidole gumba.

Mnyama huyu anaishi na wenzake kwenye makundi makubwa juu ya miti na ni mpole.

Alilazimika kubadili mtindo wake wa maisha kutokana na ukataji miti unaofanywa na wanadamu.

Misitu ilipoanza kupungua idadi ya tumbili hao pia ilipungua, na kuwafanya kuwa hatarini kuliwa na wanyama wenzao.

2: Pomboo ya Mto Yangtze (China)

Pomboo wa Mto Yangtze wa China, anayeitwa Baiji, alifikiriwa kuwa mmoja wa mamalia wa zamani zaidi ulimwenguni.
Maelezo ya picha, Pomboo wa Mto Yangtze wa China, anayeitwa Baiji, alifikiriwa kuwa mmoja wa mnyama wa zamani zaidi ulimwenguni.

Pomboo wa Mto Yangtze aliyetangazwa kutoweka mwaka wa 2006,alikuwa rangi ya kijivu asiye na nguvu ambaye alionekana kuwa na udhaifu kuliko wanyama wenzake wanaoogelea baharini.

Chini ya mwili wake laini kulikuwa na mfumo wa hisia wakusaidia kuna vitu ambao ulikuwa bora zaidi kuliko ule wa pomboo wengine.

Mfumo wake uliweza kufanya kazi vizuri sana hivi kwamba ungeweza kupata eneo la samaki hata mmoja.

Lakini pomboo hao wakakabiliwa na tishio la kuangamia wakati mto boti za uvuvi zilipofurika katika mo huo, meli za kontena, meli na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na mwanadamu.

Kutokana na msongamano huo mkubwa wa vyombo majini, hawakuwa na na uwezo wa kuendelea kuishi.

3: Caribbean Monk Seal (Serranilla kati ya Jamaika na Nikaragua. )

Mnyama

Chanzo cha picha, Getty Images

Ndama huyu wa asili wa mto wa eneo la Caribea alipatikana kwenye pwani ya mashariki ya Amerika ya Kati, pwani ya kaskazini ya Amerika Kusini, na Ghuba ya Mexico.

Lakini walisakwa bila huruma kwa ajili ya mafuta yaliyopatikana katika mafuta yao, ilhali uvuvi wa samaki wao wa chakula kupita kiasi ulisababisha uhaba wa chakula kwa ndama wa mto waliosalia.

Walionekana mara ya mwisho mnamo 1952 karibu na pwani ya Serranilla kati ya Jamaika na Nikaragua.

4: Alabama Pigtoe (Marekani)

Oyster hizi za mto zinapatikana katika Jamhuri ya Czech

Chanzo cha picha, Getty Images

Konokono huyu wa kipekee alipatikana Katika mto wa Alabama nchini Marekani hadi mwaka wa 2006.

Ilipewa jina hili kwa sababu ilikuw ana muonekano kama wa mguu wa nguruwe, lakini ilikuwa ikichuja maji ya mto yaliyochafuliwa. Lakini uchafuzi wa mto ulikuwa mwingi hivi kwamba Pigto hakuweza kustahimili tena.

 Kuangamizwa kwa kiumbe huyo mdogo kulifichua mambo mengi ya kutisha kuhusu maji hayo, ambayo yalikuwa yakichafuliwa na sumu kutoka viwandani na kusababisha magonjwa hatari katika jamii ya Waamerika wenye asili ya Afrika wanaoishi kando ya mto huo.

5: Dodo (Mauritius)

DODO

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuwa ndege maarufu lakini anayetoweka kunaweza kuwa heshima isiyo ya kawaida, lakini mbali na dinosauri, dodo ni spishi iliyotoweka kwa muda mrefu ambayo kila mtu anawafahamu. Ndege huyu, anayefanana na mhusika wa katuni Daffy Duck, aliachiliwa mara moja kwenye kisiwa cha Mauritius. Hakukuwa na wanyama waliowawinda asili ya ndege hii isiyoweza kuruka. Watu walipofika Mauritius, walikuja na wanyama wengine waliokuwa na hamu ya nyama. Dodos hakuweza kuishi mbele yao kwa muda mrefu. Dodo wa mwisho alikufa mwanzoni mwa karne ya 18.

6: Ng'ombe wa Bahari (Steller)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Ng'ombe hawa wa baharini waliokuwa wanafanana na manatee na dugongs, lakini walikuwa wakubwa zaidi kuliko viumbe hivyo. Ng'ombe wa baharini wa Steller wanaweza kukua hadi mita tisa kwa ukubwa. Ni shabaha ya wawindaji kwa sababu ya sura yake ya kupendeza, manyoya na mafuta yake yenye thamani. Inaaminika kuwa walikufa muda mfupi baada ya kutoweka kwa dodo kutokana na uwindaji na mabadiliko ya mazingira ya chakula chao.

7: Quagga (Afrika Kusini)

K

Alikuwa na uzuri wa ajabu wa quagga na ndio uliosababisha kutoweka kwake. Nusu ya mwili wa kiumbe huyu wa kivutia Afrika kwa mbele ilikuwa na mistari kama pundamilia, lakinimostari yake ilikwenda inafifia kadri inavyoelekea sehemu ya nyuma ya mwili na kutoweka kabisa kushuka kwa chini miguuni kama farasi. Kwa sababu ya umbo lake la kustaajabisha, aliwindwa sana kinyume cha sheria kiasi cha kutoweka. Mnyama wa mwisho wa jamii hii alikufa katika miaka ya 1880.

8: Irish Elk (Ireland)

P

Chanzo cha picha, Getty Images

Spishi hii ua wanyama wakubwa zilizotoweka walikuwa wanafanafana kwa kiasi kikubwa na wanyama wanaofahamika leo, lakini wanatofautiana kiasi. Tofauti pekee ni kwamba wanaweza kuwa na urefu wa mita mbili huku pembe zao zikikuwa hadi mita 3.65. Walitoweka karibu miaka 7700 iliyopita na labda illisababishwa na uwindaji na mabadiliko ya hali ya hewa.