Kwanini wazima moto Marekani wameshindwa kuudhibiti moto wa nyikani?

Mzina moto akiwa kazini e

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Chris Baraniuk
    • Nafasi, Mwandishi wa Sayansi na Teknolojia
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Ilitokea kwa wakati mbaya. Asubuhi ya Jumanne January 7, upepo wenye dhoruba kali unasababisha hasara kubwa ulikuwa unaelekea katika mitaa iliyopo kaskazini mwa Los Angeles. Kituo cha eneo hilo cha huduma ya hali ya anga ya Marekani USNWS kilichapisha tahadhari iliyokuwa na maneneo mazito mwendo wa saa 4:30 asubuhi huko Carlifornia. Na punde tu taarifa hiyo ilipotolewa, moto ukazuka katika mtaa wa Palisades jijini Los Angeles.

'Moto huo ulianza pole pole na hatimaye kusambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali,' alisema Ellie Graeden, Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya RedZone Analytics, ambayo inatengeza vinyago vya kuangazia masuala ya moto wa nyikani kwa ajili ya kampuni za bima.'Hali hii ni mbaya sana.'

Moto huo ulilipuka, na kufuatiwa na moto nyinginezo za nyika katika maeneo ya karibu. Maelfu wa majumba ya makazi na mengineo yameteketezwa hadi yakasalia kuwa majivu. Eneo la Sunset Boulevard limesalia na magofu. Kufikia sasa, moto unaozidi kuteketeza mji wa Los Angeles umesababisha vifo vya takriban watu 16. Mamlaka zimewaamuru takriban watu 180,000 kuondoka.

Moto huu sasa umeorodheshwa kuwa mkasa uliosababisha uharibifu mkubwa katika historia ya Los Angeles, huku hasara ikikadiriwa kuwa ya thamani kati ya dola bilioni 52 na 57 sawia na Pauni bilioni 42 na 46.

Gari lililoteketea likiwa mbe ua nyumb

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Haijabainika moto wa LA ulianza vipi- lakini mioto mingi ya nyika husababishwa na wanadamu

Hadi sasa hatujui ni kwa nini moto ulianza, hata hivyo. Huenda chanzo ni kutokana na kimulimuli cha radi, mliongoti wa nyaya zau meme ulioanguka, au hata kipande cha sigara kilichotupwa kabla hakijazimika kabisa. Kuna uwezekano wa sababu nyingi za kuzuka kwa moto ikiwemo kuwasha moto kimakusudi. Idadi kubwa ya mioto ya nyika husababishwa na binadamu.

Lakini huku mamlaka za Los Angeles zikianza kukusanya taarifa na vitu muhimu kubaini chanzo halisi cha kuzuka kwa moto, kasi ya moto huo, na jinsi ilivyotekekeza eneo kubwa kwa haraka na nguvu inaambatana na jambo ambalo linafanyika kwa ukubwa.

'Hali mbaya ya mlipuko'

Katia kisa hiki, mkusanyiko wa sababu za kimazingira, yaliyojitokeza kwa wakati mmoja yalifanyika kwa wakati mbaya. Mchanganyiko wa muda mrefu wa ukame uliochukuwa muda mrefu na mvua kubwa iliyonyesha siku chache kabla ya mkasa kutokea, huku mgandamizo mkali – uliotokana na kimbunga- ukisukuma upepo mkali ambao ulichangia moto kuwa mkubwa na kutekekeza mali kwa kasi.

Hapo mwanzoni, upepo wa Santa Ana kama unavyotambuliwa – huwa mkali na hupiga kutoka baharini kuingia ndani kwenye bara – na wakati huu ulikuwa unasafiri kwa kasi ya kilomita 129 kwa saa moja, hali iliyosukuma moto na kuufanya kuwa mkali zaidi.

Katika hali iliyosababisha uharibifu mkubwa, upepo huo mkali uliwazuia baadhi ya wazima moto wanaotumia ndege za helikopta kumwaga maji kutoka juu katika maeneo yaliyokuwa yanatekekea.

'Bila ya usaidizi wa angani, hatukuwa na uwezo wa kukabiliana na moto ipasavyo na hatukuwa na uweza kuzuia hasara kubwa katika baadhi ya maeneo,' alisema bi Graeden.

Hali hiyo zilijitokeza wakati ambapo tunashuhudia mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaongeza uwezekano wa moto wa nyika kuzuka kote duniani, lakini pia kufanya moto ya aina hiyo kuwa mkali na kusambaa kwa kasi. Moto huu ulikuwa mdogo, ila ghafla uliugeuka mkubwa na kuwa mkali zaidi kiasi cha kutoweza kudhibitiwa haraka.

The San Bernardino Mountains covered in snow above downtown Los Angeles under a menacing sky

Chanzo cha picha, Shutterstock

Maelezo ya picha, Upepo wa Santa Ana ambão unasemekana kuchochea moto wa nyika kuathiri Los Angeles.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Huko California, hatari ya moto za aina hii kukuwa kwa kasi na haraka sana imeongezeka kwa asilimia 25 kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi inayosababishwa na binadamu, kw amujibu wa baadhi ya tafiti.

Ongezeko la joto na ukame unaochukuwa muda mrefu unamaliza mimea na kuondoa kabisa maji kwa baadhi ya mimea iliyokuwa inanyauka kumaanisha moto unapozuka, hakuna njia ya kuidhibiti.

Matt Jones ambaye ni mwanasayansi wa mpangili wa dunia katika chuo kikuu cha East anglia, ambaye masomo yake yanangazia athari ya mabadiliko ya tabianchi kwa moto za nyika , ametaja kwamba mnamo 2022 na 2023 , Los Angeles ilipoea viwango vikubwa vya mvua, ambavyo vilivunja rekodi za awali.

Mvua hiyo kubwa, ilisaidia mimea katika eneo hilo kukuwa, lakini katika mwaka wa 2024, hali ya anga ikabadilika. Mwaka jana, kulikuwa na ukavu na hali iliyokinzanana miaka miwili iliyopita. Ilimaanisha kwamba kuna idadi kubw aya mimea iliyokauka kote katika eneo la kusini mwa California.

'Tunasalia na hali mbaya ya mlipuko,' amesema bwana Jones.

Moto na upepo: athari ya Santa Ana

Upepo wa Santa Ana ambao unatambuliwa kwa majina tofauti; kulingana na mahali unapoishi. Unafahamika kama upepo wa Fohn au Fohnwind katika eneo la milima ya Alpine huko Ujerumani, Autsria na Uswizi, unashirikishwa na imani za mila na detsuri za jamii huko kuwa na aina mbalimbali za ishara katika mwili wa binadamu kama vile kuumwa na kichwa, kuwa na msongo wa mawazo, kutoweza kulala vyema, kuchanganyikiwa na kutokea kwa idadi kubwa ya ajali.

Taarifa moja iliyochapishwa katika jarida la kisayansi mnamo 1911, ilieleza wazi athari kuu ya upopo wa Fohnwind huko Innsbruck,Austria: ''Upepo huu hupiga mara nyingi kwa nguvu kali na kusababisha hasara kubwa, madirisha ya nyumba yasipofungwa kila kitu kilichoko ndani ya nyumba hiyo kitafunikwa na vumbi.''

Mabadiliko ya tabianchi yanasababisha halijoto kuzidi katika maeneo kadhaa ambayo hushuhudia upepo wa aina ya Santa Ana.

Mxima moto akiwa kazini

Huku upepo wa Santa Ana unaovuma kwa kasi kuelekea maeneo ya chini – unaendelea kuzidisha moto wa nyika unaotekekeza Los Angeles kushika kasi – hali tofauti kabisa zinaweza kusababisha moto wa aina hii kulipuka na kusambaa kwa kasi. Kama hakuna upepo mkali, moto wa nyika wakati mwingine hubuni hali yake ya anga,' asema bwana Jones.

'Hutengeza upepo wa aina yake, wenye nguvu, katika eneo ambalo moto unawaka, hali ambayo huathiri kasi ya kusambaa kwa moto lakini pia kuchochea moto huo kuwaka katika maeneo mbali mbali bila mpangilio wowote,' anaelelzea.