Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Arsenal wanamtaka Martinez wa Inter Milan
Arsenal iko tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho msimu wa kiangazi kwa dau la £100m (euro 120m) kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, mwenye umri wa miaka 27. (Fichajes - In Spanish)
Mshambulizi wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, anasalia kuwa nambari tisa katika orodha ya wachezaji ambao Arsenal inaweza kuwasajili msimu huu wa kiangazi huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na uwezekano mkubwa wa kumpiga bei katika uhamisho wake. (Independent)
Arsenal pia ilifanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa AC Milan na Uhispania Alvaro Morata, 32, wiki iliyopita kabla ya kujiunga na Galatasaray kwa mkopo. (Athaletics- Usajili unahitajika)
Manchester City wako tayari kushindana na Real Madrid kwa ajili ya kumnunua beki wa kushoto wa AC Milan Mfaransa Theo Hernandez, 27, iwapo watamkosa beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso, 24 . (TeamTalk)
Kipengele cha kutolewa katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich na England Harry Kane, 31, kitapungua kutoka £67m hadi £54m katika mwaka ujao. (BILD - Subscription reguired)
Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca anapanga kumtumia kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos mwenye umri wa miaka 20 ambaye kwa sasa yuko Strasbourg kwa mkopo katika kikosi chake cha kwanza msimu ujao. (Fabrizio Romano)
Arsenal itatafuta kumsajili mlinda mlango wa Uhispania Joan Garcia, 23, kutoka Espanyol msimu wa kiangazi. ( Athletics - Usajili Unahitajika)
Chelsea ilishindwa katika jaribio jaribilo lake la kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Tottenham Mfaransa Mathys Tel, 19, kutoka Bayern Munich siku ya makataa. (L'Equipe -kwa Kifaransa)
Beki wa kushoto wa Manchester United na Uholanzi Tyrell Malacia, 25, angejiunga na Wolves siku ya mwisho, lakini akachagua PSV Eindhoven badala yake. (Voetbal Verslaafd - in Dutch)
Mmoja wa wachezaji wanne waliosajiliwa na Manchester City Januari atakosa mechi yao ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwasababu sheria za Uefa zinaruhusu wachezaji watatu pekee waliosajiliwa kuongezwa kwenye orodha ya kikosi kabla ya hatua ya mtoano. (ESPN)
Napoli ilisitisha mpango wake wa kumsajili winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20, kwasababu alidai mshahara mkubwa sana. (Fabrizio Romano)
Iwapo klabu itaanzisha kipengele cha kutolewa kwa Kane katika klabu ya Bayern Munich basi klabu yake ya zamani Tottenham Hotspur italazimika kuamua kama itatimiza ofa hiyo na angependelea kurejea London Kaskazini. (Telegraph - Usajili unahitajika)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi