Jinsi mapigo ya moyo yanavyoweza kukupa tahadhari kuhusu hali yako

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiwango ambacho tunaweza kutambua mpigo wa moyo wetu kinaweza kuwa na athari muhimu kwa ustawi wetu

Ilikuwa katika siku ya 29 ya safari ngumu ya mtumbwi ya kilomita 966 katika eneo la chini ya ardhi la Canada ambapo Alex Messenger mwenye umri wa miaka 17 alishambuliwa kikatili na dubu.

Siku hiyo mwaka 2005, aliondoka kambini peke yake ili kupanda kilele cha mlima cha karibu.

Wakati wa kupanda, kichwa chake kiliinama, mawazo yake yalizunguka kati ya mambo ya maisha ya kila siku - kitabu alichokuwa akisoma shuleni, Klabu ya Waongo; uzito wa kamera aliyobeba; maua madogo mazuri chini ya miguu yake.

Lakini Messenger alipokuwa anaota ndoto za mchana, dubu alikaribia bila kuonekana upande wa pili wa milima.

Wakati hatimaye walikutana, mwili wa Messenger uliitikia vyema.

"Nilikuwa tu nimeona aina hii ya rangi ya kahawia ikitokea kwenye kilima," anasema.

"Sikuwa na uhakika ni nini, lakini mshutuko uliingia mwilini mwangu. Kupumua kwangu kulikwenda mbio, macho yangu yalifungua zaidi, mapigo ya moyo yakaongezeka maradufu, na njia zangu za hewa zikafunguka.

Leo hii, karibu miaka 20 baadaye - na baada ya kusimulia aliyopitia katika kumbukumbu yake, Siku ya Ishirini na Tisa - Messenger bado anakumbuka wakati ubongo wake ulichukua kutambua ishara ambazo mwili wake ulikuwa ukitoa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Kulikuwa na majibu kutoka kwa mwili," anakumbuka.

“Kisha, baadaye, kulikuwa na mwitikio wangu wa kiakili na kihisia.

Mwanzoni alidhani "doa ya kahawia" alikuwa ni musk ox. Umbo lilipoonekana wazi ndipo alipogundua kuwa mwili wake tayari ulikuwa umejitayarisha kukabiliana na tishio la kutisha zaidi: mnyama hatari wa uzani wa pauni 600.

Dubu alisogea moja kwa moja kuelekea kwake, akamwangusha chini kwa pigo kali la kichwa. Akaliuma paja la Messenger, ambaye alizimia, kabla ya kumtelekeza.

Aliyopitia Messenger sio tu hadithi ya muujiza ya kuponea. Pia inatoa ufahamu juu ya hisia zetu za ndani ambazo mara nyingi hazizingatiwi.

Ingawa tunazifahamu hisia tano zikiwemo kuona, kunusa, kusikia, kuonja na kugusa - interoception ni uwezo wetu wa kutambua na kutafsiri ishara zinazotoka ndani ya miili yetu yenyewe.

Zaidi ya karne moja kabla ya makabiliano ya kutisha kati ya Messenger na dubu, mwanafalsafa na mwanasaikolojia Mmarekani William James alikuwa akichunguza jukumu ambalo ishara za mwili zingeweza kutekeleza katika kuunda hisia zetu.

Kulingana na yeye, kukutana na dubu hakufanyi moyo wetu kwenda mbio kwa sababu tunaogopa.

Badala yake, yaliyomkumba Messenger yanaonyesha kuwa miili yetu huitikia tishio tunalohisi kwa kutumia adrenaline, kuongeza mapigo ya moyo na kupumua, na kisha tunafasiri ishara hizi za mwili kama hofu. Kwa maneno mengine, hisia hutokea kutoka kwa mwili.

Wasiwasi na unyogovu

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sisi sote ni muhimu, kwa viwango tofauti, kwa ishara za ndani zinazotumwa kutoka kwa mwili wetu hadi kwa ubongo.

Hata hivyo, James aliweka msingi wa kwanza wa jinsi tunavyofikiri kuhusu uhusiano wa karibu kati ya ubongo na mwili. Kulingana na Antonio Damasio, profesa wa saikolojia, falsafa na mfumo wa neva katika Chuo Kikuu cha Southern California huko Marekani: “Mawazo na hisia zetu haziathiriwi tu na mwili wetu. Shughuli zetu zote za kiakili ni matokeo ya mwingiliano kati ya mwili na ubongo.

Katika kitabu chetu cha hivi majuzi, Je, Unafikiri Kwa Uwazi?, tunachunguza mambo mbalimbali yanayoathiri na kuendesha jinsi tunavyofikiri, kuanzia jeni, tabia hadi teknolojia, hali ya hewa na bakteria kwenye utumbo wetu . Na hisia hii ya ndani, ambayo ni utafiti unaopanuka kwa kasi, imeonekana kuwa mojawapo ya kuvutia zaidi.

"Interception ni uchakataji wa ishara za mwili zinazotoka ndani," anasema Jennifer Murphy, ambaye anafanya utafiti kuhusu uchakataji huu na athari zake katika utambuzi na afya ya akili katika Chuo Kikuu cha Royal Holloway huko London.

“Hii ni pamoja na kuhisi mapigo ya moyo wako, kupumua na kujua wakati unahitaji kwenda chooni au unapokuwa mgonjwa. Njaa na kushiba ni mifano mingine.

Baadhi ya ishara hizi za mwili, ambazo hupitishwa kutoka kwa viungo vyetu na sehemu nyingine za mwili hadi kwa ubongo wetu kupitia "mtandao wa ndani" wa viunganishi, ikiwa ni pamoja na mishipa ya uti wa mgongo na kemikali katika mkondo wa damu, ni ngumu sana kutambuliwa na akili yetu. Zingine, kama moyo unaoenda mbio, hofu kwenye tumbo kwa sababu ya woga au njaa sio ngumu.

Sisi sote huwa tunatambua ishara hizi za ndani kwa viwango tofauti, na sote tunaweza kuzitafsiri na kuzijibu kwa njia tofauti, kulingana na sisi ni nani na tunafanya nini. Kwa kweli, usumbufu katika hisia zetu na mtazamo wa ishara za mwili unaweza kuwa sababu ya anuwai ya patholojia.

Hii ni sayansi ya kisasa, na njia nyingi zinazohusika hubakia kuwa ngumu kufanyiwa majaribio.

"Marekebisho madogo"

Lakini utambuzi unawezaje kutumika katika maisha yetu ya kila siku?

Zingatia mapigo ya moyo wako - pengine ni mojawapo ya ishara za mwili ambazo unaona mara nyingi. Inajulikana sana kuwa wasiwasi unaweza kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha mapigo ya moyo.

Lakini vipi ikiwa, kama James na wengine wengi wamependekeza, hali hiyo inatokea kwa njia nyingine - na kuongezeka kwa mapigo ya moyo kunaweza kusababisha wasiwasi na kutufanya tusiwe na raha?

Ikiwa ndivyo, kiwango ambacho sisi ni tunaweza kutambua mapigo yetu ya moyo - na jinsi tunavyofasiri na kujibu ishara hizi - inaweza kuwa na athari muhimu kwa ustawi wetu na afya ya akili .

Lakini utafiti uliochapishwa mnamo 2023 na timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Stanford huko California ulienda mbali zaidi. Walijaribu ikiwa kuongezeka kwa mapigo ya moyo kunaweza kusababisha wasiwasi na hofu.

Watafiti walitumia non-invasive optogenetic stimulator (mbinu inayotumia mwanga kudhibiti seli) ili kuongeza kiwango cha mapigo ya moyo wa panya. Kisha walifuatilia panya hao ili kuona kama walikuwa tayari kuchunguza na kutafuta maji.

Matokeo yalikuwa ya kushawishi. Mapigo ya moyo yao yalipoongezeka, panya walipata wasiwasi zaidi – walikuwa na uwezekano mdogo wa kuchunguza sehemu zilizo wazi na kuamua kukaa katika maeneo yaliyohifadhiwa. Lakini muhimu, athari hii ilitokea tu katika "mazingira ya hatari" (kwa mfano, wakati kulikuwa na tishio la mshtuko mdogo).

Kwa maneno mengine, utafiti unapendekeza kwamba "tathmini" yetu au tafsiri ya ishara za mwili inaweza kuwa na jukumu muhimu katika jinsi zinavyoathiri hisia zetu.

Hali ambayo huturudisha kwenye umuhimu wa ishara za mwili - na jinsi tunavyozitambua na kuzijibu - kwa ustawi, afya ya akili na kufanya maamuzi. Mojawapo ya vizuizi vikubwa katika uwanja huu ni kubaini jinsi watu wanavyozingatia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutafakari kunaweza kutusaidia kusikiliza ujumbe ambao miili yetu inatutumia

Uchunguzi wa Garfinkel na watafiti wengine uligundua kuwa wafanyabiashara katika kituo cha soko la hisa la London ambao waligundua kwa usahihi mapigo yao ya moyo walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya maamuzi yenye faida na kuwa na taaluma ndefu.

Zaidi ya hayo, watu ambao wana ugumu wa kutambua hisia zao za mwili wana ugumu zaidi wa kueleza na kudhibiti hisia zao.

Lengo kuu la ubongo ni kuweka mwili, na kwa hiyo wenyewe kuwa hai.

Lakini ikiwa ni lazima ufanye kila uwezalo kudhibiti mazingira yake ya nje (ili kuepuka kuliwa na dubu, kwa mfano) na kudumisha hali nzuri katika mwili (kuzuia viwango vya glukosi kuongezeka sana au shinikizo la damu kushuka sana, kwa mfano), haiwezi kufikia moja kwa moja mazingira haya mawili.

Inazuiwa kufanya hivyo, hata kama hatupati uzoefu kwa njia hiyo, na lazima tutegemee ishara zisizo za moja kwa moja ambazo sababu yake haiwezi kuhakikishwa.

Badala yake, ubongo huunda kielelezo cha mwili kulingana na anuwai ya vigezo muhimu kwa kuishi. Kisha huendelea kufanya utabiri, ambayo hujaribu kwa makosa na kusahihisha kulingana na habari ya hisia inayopokea, na kuiruhusu kudhibiti mfumo.

"Unaweza kuwa mwangalifu kupita kiasi kwa kila jambo dogo linaloendelea katika mwili wako, na hilo linaweza pia kusababisha aina fulani ya wasiwasi," Seth anaonya.

Linapokuja suala la kuelewa kutambua, kuna siri nyingi. Lakini sayansi inapoendelea zaidi na zaidi, inafaa kutazama nafasi hii ya ndani.

Imetafsiriwa na Jason Nyakundi