Mashindano ya riadha na Wahadza - mbio za kusherehekea maisha ya asili

,

Wakati wa kupambazuko kaskazini mwa Tanzania, Jua linaanza kuchomoza kwenye Bonde la Yaeda na kuanza kwa siku mpya kunamaanisha jambo moja kwa kabila la Wahadza.

Ni wakati wa kuanza tambiko lao la kila siku la kutafuta chakula kitakachowaendeleza hadi jua litakapochomoza.

 Kwa wanawake, hii ina maana ya kutoka na vijiti virefu vya mbao kutafuta matunda na kuchimba mizizi ya chakula.

Kwa wanaume, ni wakati wa kuwinda. Kwa upinde na mishale iliyotengenezwa kwa mikono, watatembea hadi kilomita 40 kwa miguu hadi kufikia saa sita mchana.

Katika msimu wa joto wa mwaka 2023 kikundi cha wanariadha watawasili kwenye ardhi ya Hadza kwa mashindano ya mbio za kilomita 80. Washindani watatumia ujuzi wa kuishi wa Hadza ili kuishi eneo hilo.

 Hakutakuwa na chakula cha ziada au nishati.

Wakimbiaji hawataruhusiwa kuleta vifaa. Maji yatalazimika kukusanywa kutoka kwenye visima vya asili vya maji ya mvua kwenye miti ya mbuyu huku matunda ya miti yakiwa miongoni mwa vyanzo vyake vya nishati.

m

Kabila la Wahadza limekuwa likiishi hivi katika eneo hili kwa maelfu ya miaka.

Wao ni mojawapo ya makabila machache ya wawindaji-wanaoishi kiasili waliyosalia duniani.

 Wanaishi kwa uendelevu siku hadi siku mbali na ardhi yao ya asili katika Bonde la Yaeda, hawahifadhi chakula au rasilimali na hawana historia ya njaa.

 Lakini, idadi yao imepungua hadi 1,300 kwa sababu ya uvamizi kutoka katika makabila ya wafugaji na makazi ya wakulima. Wamepoteza 90% ya ardhi yao tangu miaka ya 1960.

m

"Nilipokuwa mtoto hakukuwa na makabila mengine katika eneo hilo hadi kilomita 80 kutoka hapa," mzee wa kabila bwana Maroba anasema akiwa ameketi kwenye jiwe linalotazama bonde.

 "Hifadhi ilikuwa hapa wakati huo - kila kitu kuanzia tembo, twiga, pundamilia, nyumbu - walikuwa wengi kwa ajili ya kuwinda. Polepole hilo lilibadilika na watu wakaanza kuhamia."

m

Mbio hizo zitafanyika wakati wa kiangazi, wakati mazingira yanaonekana kuwa mabaya na yasiyo vumilika.

 Lakini wanawake wa Kihadza wanasisitiza kuwa kuna chakula kingi kama unajua pa kuangalia.

 Wakati wa lishe ya asubuhi, Apooa inatuonyesha tawi lenye rangi ya kijivu ambalo linaashiria kuna mizizi inayoliwa chini yake. Anasema:

"Tunachimba makalitako na chakula hiki kitatusaidia hadi jioni hii

m

Mapema asubuhi inayofuata tunakaribia kujionea moja kwa moja baadhi ya kozi na watu wa makabila mawili tofauti, Moshi na Sindano.

 Wahadza ni jamii iliyo na usawa kabisa kuhusiana na jinsia na umri. Lakini, kuna safu dhahiri katika utaalam katika kikundi chetu kinachoendesha.

 Akiwa na upinde na mshale katika mkono mmoja na mwingine mfukoni, Moshi anatembea kwa kasi kwenye eneo lenye miamba, lisilo na usawa, lenye vilima pamoja na Sindano, ikijihadhari na fursa yoyote ya kuwinda. Inabidi ukimbie ili uendelee.

mm

Mapema asubuhi hiyo, njia ya mbio za mwaka ujao ilielezwa Moshi na Mika Peterson, muongozaji na mtafsiri wetu kutoka Mfuko wa Dorobo, shirika la uhifadhi la Dorobo Safaris ambalo linafanya kazi na Wahadza kuhifadhi haki za ardhi.

Atafanya kazi na mtaalamu wa riadha Josue Stephens na kampuni yake ya Barefoot Adventures kuandaa mbio hizo, ambazo bado hazina jina. 

m

Wahadza hawatumii kilomita au maili. Mika - akibadilisha kati ya Kiswahili na lugha ya Wahadza, - anaelezea njia ambazo wanatumia wahadza.

 "Watafiti wameweka vifuatiliaji kwa watu wa Hadza ni kawaida sana kwa Mhadza kwenda kuwinda na kukimbia kilomita 30 au 40 majira ya asubuhi," anasema Daudi Peterson, baba yake Mika, ambaye amekuwa akifanya kazi na Wahadza tangu miaka ya 1990.

mm

Mratibu wa mashindano ya riadha Stephens ametumia muda mwingi wa maisha yake kukimbia na kabila la Tarahuma nchini Mexico, kuandika kitabu kinachoitwa Born to Run cha Christopher McDougall. Alivutiwa kuandaa mbio na Wahadza kwa sehemu na uvumilivu wao kama wa mwanariadha.

 Uchunguzi umeonesha kuwa kabila la kawaida la Hadza hukamilisha muongozo wa mazoezi ya kila wiki ya- dakika 150 - kila siku. Pia wamegundua Wahadza hawana matatizo ya afya ya moyo , hata katika uzee.

 Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Hadza wanatuambia wangependa kufanya mbio hizo, huku Mika akiongeza: "Mtu kama Moshi, labda tutaomba kukaa karibu na mgongo ili kumsaidia yeyote anayetatizika."

mm

Itakuwa kozi ngumu kwa wanariadha 50 hadi 100 wanaotarajiwa kushindana.

Kilomita themanini katika halijoto zaidi ya 30C katika mwinuko wa 1,300m (sawa na mlima mrefu zaidi wa Uingereza Ben Nevis) itakuwa ngumu vya kutosha. Wakimbiaji hao pia watatafuta matunda ya porini, kuchimba mizizi, mishale ya kutengeneza kwa mikono, kuvuna asali na kupanda miti ya mbuyu kutafuta maji na matunda.

 "Kwa wanariadha, changamoto hizo zitachukua muda mrefu sana, lakini nitaweza kuzifanya haraka sana," Moshi anasema.

mm

Unaweza kuona miti ya mibuyu inayopatikana kila mahali katika mahali popote kwenye bonde.

Shina zao nene huwapa muonekano wa mifereji ya maji.

 Mbuyu unajulikana kote Afrika kama mti wa uzima na kwa sababu nzuri na inaweza kuhifadhi zaidi ya lita 100,000 za maji wakati wa msimu wa mvua.

 Tunda lake ni chakula cha juu kinachojulikana na vitamini C mara sita zaidi ya chungwa.

 Mika anasema: "Mbuyu utakuwa chakula kikuu cha kuendeleza mbio. Wakimbiaji hawawezi kuleta chakula chao chochote na watalazimika kupata chakula na vinywaji kwa ujuzi wanaojifunza kutoka kwa Wahadza."

mm

Katikati ya uwindaji wa asubuhi katika siku yetu ya mwisho bondeni tuliacha kufanya mazoezi ya ustadi wetu wa kuvuna ubuyu. Moshi tena yuko mbele, anacheka, anatabasamu na anatufundisha salamu ya jamii ya Wahadza.

'Am I yega' inatafsiriwa kama 'upo hai?'

mm

Hapo awali, Moshi alikuwa akiwaondoaa nyuki kutoka kwenye mzinga wao kutafuta asali.

Ilimchukua dakika chache kuwasha moto mdogo, kwa kutumia msuguano wa matawi kwa mbinu ya kuchimba visima kwa mkono na nyasi kavu kuwasha. Wakimbiaji pia watalazimika kujua hii kwa kuchoma mizizi na joto wakati wa usiku.

mm

Upande wa kulia kwetu kuna kipande cha mbao kilichopakwa rangi nyeupe upande mmoja na kijani upande mwingine. Ni kwa ajili ya urefu wa mita na ni alama ya mpaka.

Rangi inayowaka huchota mstari wa eneo la Wahadza na alama ambapo makabila ya wafugaji wa Datoga yanaruhusiwa kwenda kwenye ardhi ya Wahadza nyakati fulani za mwaka kwa malisho ya ng'ombe.

mm

Baadhi ya mapato ya mbio yatalipwa moja kwa moja kwa Wahadza, kwa matumizi ya ardhi yao na kugawana ujuzi wao wa kuishi. Wanatumia pesa katika huduma za afya, elimu na kutatua migogoro ya ardhi. Wameishi katika eneo hili kwa makumi ya maelfu ya miaka, lakini ni tangu mwaka wa 2003 eneo lao la jadi limepewa rasmi kwa sheria za Tanzania.

w

Katika mchana wetu wa mwisho na Wahadza, tulitumia muda fulani kukaa juu ya mwamba mkubwa unaoelekea Bonde la Yaeda pamoja na Maroba. Alipoulizwa jinsi bonde hilo lilivyobadilika katika maisha yake, Maroba alianza hadithi ndefu, mikono yake ikielekezwa pande mbalimbali huku akieleza maeneo tofauti ya upeo wa macho ambayo zamani yalikuwa ardhi ya Hadza.

Alipomaliza kuzungumza, tuliuliza kuhusu makabila hasimu yaliyovamia.

Alitabasamu na, kusema: "Imekuwa vigumu sana kuishi kwa kutegemea ardhi kuliko nilipokuwa mtoto.

"Ongezeko la watu na shinikizo, hata kama tuna maeneo haya yaliyotengwa ambayo yana ulinzi wa aina fulani, inafanya kuwa ngumu sana kuwinda. Tunakoelea sio kuzuri sana, lakini watu hao wanahitaji kujikimu kimaisha. vizuri."