Wanawake wanavyonyanyaswa kingono mashariki mwa DR-Congo
Zaidi ya wanawake 150 wananyanyaswa kingono kila mwezi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, haya ni kwa mujibu wa rekodi za kulazwa kwa wagonjwa katika hospitali ya Panzi huko Bukavu pekee.
Mamia ya wanawake wamelazwa katika kituo hicho, wakiwa wamekata tamaa, na kuvunjika moyo kwa kudhalilishwa na wanamgambo wenye silaha katika eneo hilo.
Vita kati ya waasi wenye silaha huko mashariki mwa DRC na majeshi ya serikali vikizidi, viongozi wa eneo hilo, wanawake, wasichana na madaktari katika kituo hiki kinachosimamiwa na Dkt Denis Mukwege, wanahofia huenda kituo hicho kikazidiwa na wingi wa idadi ya wahanga wa vitendo vya unyanyasaji kingono na wagonjwa wanaolazwa.
Mwandishi wa BBC Caro Robi ametembelea kituo hicho Bukavu, DRC.









