Sri Lanka: Nyumba ya Waziri mkuu wa Ranil Wickremesinghe imechomwa moto

Chanzo cha picha, Getty Images
Nyumba ya Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe imechomwa moto katika ghasia za waandamanaji.
Kipindi cha saa moja iliyopita hali ya ghasia baina ya waandamanaji na polisi imekuwa ikiendela kuongezeka nje ya makazi ya Wickremesinghe katika mji mkuu Colombo.
Awali maelfu ya waandamanaji wamevamia kamazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa katika mji mkuu wa Sri Lanka.
BBC haijaweza kuthibitisha aliko rais, lakini chanzo kilichopo karibu na Waziri mkuu kimesema yuko ''mahala salama ".
Waandamanaji kutoka maeneo yote ya nchi waliandamana hadi mjini Colombo kudai kujiuzuru kwake baada ya maandamano ya miezi kadhaa kuhuusu kushindwa kudhibiti mzozo wa kiuchumi unaoikumba nchi hiyo.
Taarifa zaisema kuwa rais alikuwa ameondolewa tayari na kupelekwa katika eneo salama wakati waandamanaji waipoingia nyumbani kwake.
Nchi hiyo inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na inahangaika kuagiza chakula, mafuta na madawa.
Maelefu ya waandamanaji wanaoipinga serikali walisafiri hadi katika mji mkuu, huku maafisa wakiliambia shirika la habari la AFP kwamba wengine hata ‘’waliziamrisha’’ treni kufika pale.
Waliingia katika wilaya ya serikali ya Colombo, wakipaza sauti wakisema "Gota go home!" (lazima uende nyumbani) na kuvuka kwa nguhvu vizuizi kadhaa vya polisi kuifikia nyumba ya Rais Rajapaksa.
Polisi walifyatua risasi angani na kutumia gesi za kutoa machozi kuuzuwia umati wa watu kuingi.
"Rais alikuwa akisindikizwa kumepekwa mahali salama," afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi aliiambia AFP. "Bado ni rai, analindwa na kikosi cha jeshi ."
Maafisa walijaribu kuwazuia waandamanaji kwa amri ya kutoka nje lakini walilazimika kuiondoa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Picha za moja kwa moja za mtandao wa kijamii wa Facebook kujtoka ndani ya jengo la makazi ya rais zilionyesha waandamanaji wakiwa ndani ya vyumba na veranda, huku mamia pia wakizunguka kwenye mazingira yake na wengine wakiwa nje ya nyumba ya rais.
Picha za BBC zinaonyesha watu kadhaa wakiwa ndani ya kidimbwi cha kuogelea cha kasri ya rais.
Waandamanaji katika maeneo tofauti pia waliweza kuingia katika ofisi ya rais, ambayo imekuwa ikilengwa na waandamanaji kwa miezi kadhaa.
Takriban watu 33, wakiwemo wanajeshi wa usalama, wamejeruhiwa na wamekuwa wakipata matibabu katika hospitali ya taifa ya Sri Lanka mjini Colombo, msemaji wa hospitali hiyo ameiambia BBC Idhaa ya Sinhala.
Maafisa walikuwa wamejaribu kuzuia maandamano yasifanyike kwa kuweka mari yakutotoka nje usiku wa ijumaa. Lakini waandamanaji hawakukata tamaa, , na amri hiyo ikaondolewa baada ya makundi ya kiraia na vyama vya upinzani kuipinga vikali.
Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe ameitisha mkutano wa dharura wa viongozi wa vyama vya kisiasa vya Sri Lanka kujadili mzozo huo. Pia amemuomba Spika kikao cha bunge.
Wiki iliyopita, maafisa waliahirisha mauzo ya petroli na dizeli kwa magari yasio ya shughuli muhimu ili kujaribu kutunza akiba ya taifa ya mafuta iliyoendelea kupungua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali imekuwa ikijaribu kupata mafuta kwa mkopo kutoka nchi nyingine ikiwemo Urusi – lakini mpaka sasa haijafanikiwa
Iliomba msaada wa fedha za dharura na ililaumu janga la Covid-19, ambalo liliua biashara ya utalii ya sri lanka- moja ya sekta zilizoliingizia taifa hilo fedha za kigeni
Lakini wataalamu wengi wanasea kushindwa kuongoza vyema uchumi wan chi hiyo ndilo tatizo kuu.
Maandamano yamekuwa yakifanyika tangu mwezi machi huku waandamanaji wakimtaka Rais Rajapaksa aondoke madarakani.
Mzozo mbaya wa kiuchumi ulimsababishia kaka mkubwa wa Rais, Mahinda Rajapaksa, kulazimika kujiuzulu kama Waziri mkuu mwezi Mei.














