Virusi vya corona: Ghadhabu baada ya Sri Lanka kuchoma kwa lazima maiti ya mtoto wa Kiislamu

Chanzo cha picha, AFP
Hatua ya kuchoma kwa lazima maiti ya mtoto wa Kiislamu wa siku 20-nchini Sri Lanka imezua mjadala mkali kuhusu agizo la serikali la kuchomwa kwa maiti za watu wote waliofariki kutokana na ugonjwa wa corona.
Wakosoaji wanasema agizo hilo haliambatani na msingi wa kisayansi na kuongeza kwamba linawalenga jamii ya wachache.
Mohamed Fahim na mke wake walifurahia sana Fathima Shafna wakati mtoto wao wa kiume Shaykh alipozaliwa Novemba 18 baada ya kusuburi kwa takriban mmiaka sita kupata mtoto.
Lakini furaha yao ilikatizwa ghafla.
Usiku wa Disemba tarehe 7, waligundua mtoto wao anakabiliwa na tatizo la kupumua. Walimkimbiza hopitali bora zaidi ya watoto katika mji mkuu wa Colombo, Lady Ridgeway.
"Walituambia kuwa hali ya mtoto ilikuwa mbaya sana kwasababu anaugua homa ya mapafu. Lakini, ilipofika karibu saa sita usiku, walimfanyia uchunguzi zaidi ambao ulibaini kuwa ana virusi vya corona," Mohamed Fahim, ambaye anaendesha gari la magurudumu tatu kujitafutia kipato aliambia BBC Sinhala.
Madaktari baadaye waliwafanyia vipimo vya corona Bw. Fahim na mke wake lakini hawakupatikana na virusi hivyo hatari.
"Niliuliza inawezekanaje mtoto awe na virusi na sote wawili hatukupatikana navyo, hata mama aliyekuwa akimnyonyesha?"
Licha ya vilio na kurai kwa muda, wazazi hao walilazimishwa kwenda nyumbani na maafisa ambao walisema wanahitaji kufanya uchunguzi zaidi. Waliambiwa wapige simu hospitali kupata maelezo.
Siku iliyofuata, walifahamishwa kuwa mtoto wao alifariki kutokana na corona. Bw. Fahim aliwaomba madaktari kumfanyia uchunguzi zaidi kubaini kama kweli mwanawe amefariki, lakini walikataa.
Baada ya hapo, madaktari walimuomba atie saini nyaraka za kuidhinisha mtoto wao achomwe, kwa mujibu wa sheria za Sri Lanka.
Bw.Fahim alikataa: kuchoma maiti ni kinyume na dini ya Kiislam.
Na sio yeyey peke yake. Baadhi ya familia za Kiislamu zimekataa kuidhinisha hatua ya kuchomwa kwa maiti za jamaa zao na kuacha serikali kugharamia uchomaji wa miiili hiyo, huku wengi wakikataa kuchukua majivu ya wapendwa wao.

Chanzo cha picha, AFP
Bwana Fahim anasema aliuliza mara kadhaa mwili wa mtoto wake arudishwe kwake, lakini maafisa walisema hapana. Siku iliyofuata, aliambiwa mwili wa mtoto wake unapelekwa kwenye chumba cha kuchoma maiti.
"Nilifika hapo lakini sikuingia katika ukumbi huo," anasema. "Unawezaje kumwangalia mtoto wako akichomwa?"
'Hakuna ushahidi'
Viongozi wa kisiasa, kidini na kijamii wanaoziwakilisha jamii za Kiislamu wameomba serikali mara kadhaa kubadili sera ya "kuchoma maiti", wakitoa mfano wa zaidi ya nchi 190 ambazo zinaruhusu kuzikwa kwa maiti za watu waliofariki kutokana na corona.
Wanaharakati, wamewasilisha kesi Mahakama Kuu, kupinga agiszo hilo lakini kesi hizo zilifutwa bila maelezo.
Serikali inasema kuzika miili kunaweza kuathiri maji ya ardhini, kwa msingi wa maoni ya kamati ya wataalam ambayo wakosoaji wanapinga.
Daktari bingwa wa magonjwa yanayotokana na virusi Prof Malik Peiris, hata hivyo, amehoji nadharia hiyo.
"Covid-19 sio ugonjwa unaosababishwa na maji, "Prof Peiris aliiambia BBC." Na sijaona ushahidi wowote unaosema unaenezwa kupitia miili iliyokufa. Virusi vinaweza kusabaa tu kwenye seli hai. Mara tu mtu anapokufa, uwezo wa virusi kuzaan hupungua. "."
Pia aliongeza kuwa: "Maiti hazizikwa ndani ya maji ya bomba. Mara tu unapozika mwili uliyofunikwa futi sita chini ya ardhi, kuna uwezekano mkubwa kwamba hauchafua maji ya bomba."

Chanzo cha picha, AFP
Hoja ya jamii ya Waislamu kupinga sheria ya kuchoma maiti haijatiliwa maanani kwa muda - lakini hatua ya kuchoma kwa lazima maiti ya mtoto Shaykh imebadilisha hilo.
Muda mfupi baada ya taarifa hiyo kuangaziwa, wanaume,wanawake na viongozi wa kidini kutoka madhebu tofauti walikusanyika nje ya aneo la kuchoma maiti na kufunga vitambaa vyeupenje ya lango kuu. Wengi walikuwa kutoka jamii ya Sinhala.
Watu pia wametumia mitandao ya kijamii kulaani kitendo hicho.
Mwanaharakati na wakili Thyagi Ruwanpathirana, ambaye alikuwa miongoni mwa walifunga vitambara vyeupe katika lango hilo, aliweka ujumbe katika mtandao wa Twitter akielezea kilichofanyika: "Nilikuwa nikijaribu tu, mara mama na binti yake wakavuka barabara na kuungana nami wakiwa na vitambaa vyao vyeupe. Kabla nifike hapo walihofia huenda kuna mtu anawaangalia.
Vitambara hivyo vilitoweka nyakati za usiku, lakini inasadikiwa huenda viliondolewa na mamlaka, lakini ghadhabu za watu ziliongezeka.

Hilmy Ahmed, naibu Rais wa Baraza la Waislamu nchini Sri Lanka, ameiambia BBC kwamba hatua hiyo ni ishara wazi ya najenda ya "ubaguzi" , unaowalenga Waislamu waliyo wachache.
"Serikali haijachukua hatua hiyo kwa misingi yoyote ya kisayansu," alisema. "Hawaonekani kufuata ushauri wa wataalamu wa magonjwa yanayotokana na virusi wala wanabaiolojia. Hii ni ajenda ya kibaguzi inayoendeshwa na baadhi ya watu waliyojumuishwa katika kamati ya wataalamu iliyobuniwa na serikali."
Aliongeza kusema: "Walifanya makosa sana kumchoma mtoto huyo bila wazazi wake kumuona."
Lakini serikali imekana madai hayo ikisema hatua hatua hiyohailengi jamii ya Waislamu, ikiashiria jamii ya Wabudha wa Sinhala wanachoma maiti ya wapendwa wao ndani ya saa 24, hali ambayo inaenda kinyume na utamaduni wao.
Waziri Mkuu Mahinda Rajapaksa, wakati huo huo, ameamuru mamlaka kupata ardhi kavu inayofaa kuzika wale wanaokufa kutokana na virusi vya corona, ilisema taarifa kutoka ofisi yake.

Chanzo cha picha, Getty Images














