Kombe la Dunia 2022: Nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia inamchanganya Mbeumo

Bryan Mbeumo on the ball for Cameroon

Chanzo cha picha, Getty Images

Bryan Mbeumo anasema kwamba 'atachanganyikiwa' iwapo atapata heshima ya kuanzisha mchezo kwa Cameroon kwenye Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliitwa kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika Qatar, ambapo Indomitable Lions itamenyana na Brazil, Serbia na Uswizi, licha ya kucheza mechi yake ya kwanza Septemba mosi.

Baada ya kuitaja ndoto yake kuwa kweli kuwa kwenye michuano mikubwa zaidi ya kandanda, Mbeumo angefurahi zaidi akijiona yupo miongoni mwa timu uwanjani nyimbo za taifa zitakapokuwa zinachezwa.

"Siku zote nilitaka kucheza Kombe la Dunia tangu nilipokuwa mdogo," Mbeumo aliiambia BBC Sport Africa.

"Kutembea tu kwenye uwanja na umati mkubwa na mambo mengine itakuwa jambo la kupendeza zaidi. Nitahisi kuchanganyikiwa."

Cameron itacheza katika Uwanja wa Al Janoub wenye uwezo wa kuchukua watu 40,000, mara mbili, na Uwanja wa Lusail Iconic wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000, ambao utaandaa fainali yenyewe tarehe 18 Desemba.

Mbeumo hivi majuzi tu alichagua kuwawakilisha Waafrika wa kati baada ya kucheza katika viwango mbalimbali vya vijana Ufaransa alikozaliwa, na kubadili kwake kurasimishwa miezi mitatu tu iliyopita.

Baba yake anatoka Douala, ambako Mbeumo bado ana "familia zake", pamoja na jamaa wengine katika mji mkuu Yaounde.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Douala pia ni jiji la nyumbani kwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne Samuel Eto'o, ambaye ameongoza bodi ya mpira ya Cameroon tangu mwishoni mwa 2021 na ambaye alichukua jukumu muhimu katika kumsajili Mbeumo.

Kabla ya Mbeumo mzaliwa wa Avalon kuweka mustakabali wake kwa mabingwa hao mara tano wa Afrika, wawili hao walitoka kwenda kula chakula cha jioni katika jiji la nyumbani la Brentford, London.

“Ilikuwa heshima kwangu kukutana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa sababu alikuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani,” alieleza.

"Aliniambia kuhusulengo hilo, tunachoweza kufanya na nilifurahia wakati huu. Ni jambo kubwa kwa mtu kama yeye kukutaka katika timu yake."

Eto'o alinyakua mataji manne ya Ligi ya Mabingwa na mawili ya Afrika wakati wa uchezaji wake mashuhuri, na Mbeumo anasema nyota huyo wa zamani wa Barcelona analenga mbali zaidi baada ya Cameroon kupoteza nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nyumbani dhidi ya Misri mwezi Februari.

Mahusiano ya familia

France's forward Bryan Mbeumo controls the ball during the UEFA Under 21 Euro 2021 qualifying football match between Switzerland and France on November 19, 2019 at La Maladiere stadium in Neuchatel.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbeumo, ambaye alichipuka kupitia akademi ya vijana ya Troyes, aliwakilisha Ufaransa katika ngazi ya U17, U20 na U21.

Mbeumo anaelezea uamuzi wa kutupilia mbali nchi ya mama yake kwa ajili ya Cameroon kuwa "mgumu na mrefu".

Alikua akitazama mechi za Kombe la Mataifa na anasema anaifahamu Cameroon vyema, tofauti na baadhi ya raia wa nchi mbili ambao wanaweza kuwa na ufahamu mdogo wa mataifa waliyoasili.

"Nilipoichezea Ufaransa katika timu ya vijana na kukulia Ufaransa pia, ilikuwa ngumu lakini nimesafiri hadi Cameroon mara nyingi," alisema mchezaji huyo wa Indomitable Lion.

"Baba yangu ana Fahari sana, na ana furaha sana kwangu. Ninashukuru kuwa sehemu ya hili kwake, na kwa familia yangu, na ana furaha sana."

Mechi ya kwanza ya Mbeumo ya Cameroon ilichapwa 2-0 na Uzbekistan kabla ya kupoteza 1-0 dhidi ya Korea Kusini, na michezo yote miwili mjini Seoul.

"Hii ilikuwa michezo yangu ya kwanza katika soka [ya juu] ya kimataifa, kwa hivyo nilijifunza mengi. Ni aina tofauti ya mchezo."

Pia ni chumba tofauti cha kubadilishia nguo kwa Mbeumo, ambaye alikuwa akicheza soka la daraja la pili la Ufaransa hivi majuzi kama 2019 kwa Troyes.

"Akiwa amezoea chumba cha kubadilishia nguo, anafurahia muda wake na kikosi cha Cameroon, ambao mara nyingi huimba na kucheza wakielekea kwenye mechi.

"Katika chumba chetu cha kubadilishia nguo, tunapenda muziki na kucheza dansi, huwezi kuamini! Inafurahisha sana."

Japo kuwa, kuna kazi ngumu ya kukabiliwa huko Qatar.

Licha ya kufanya vyema katika Fainali zao mbili za kwanza za Kombe la Dunia - bila kushindwa 1982, kabla ya kuwa Waafrika wa kwanza kufika robo fainali mwaka wa 1990 - rekodi ya hivi majuzi ya Cameroon ni mbaya.

Katika mechi 15 za fainali za 1994, wameshinda mara moja tu - ushindi mnono wa 1-0 dhidi ya Saudi Arabia (na Eto'o akifunga) mnamo 2002 - na kupoteza 10, huku wakifungwa zaidi ya mabao 30.

Kuanza na kasi

Cameroon striker Bryan Mbeumo in action for his national team

Chanzo cha picha, Getty Images

Ili Mbeumo kuongeza matumaini yao, mshambuliaji huyo mwenye mchezo mzuri, lazima ajifunze kwa kasi soka la kimataifa na uchezaji wa wachezaji wenzake wapya.

Cameroon wana mechi moja ya mwisho ya kujiandaa, dhidi ya Panama mnamo 18 Novemba huko Abu Dhabi, kabla ya mechi yao ya kwanza ya Kundi G dhidi ya Uswizi mnamo Novemba 24, na michuano dhidi ya Serbia (Novemba 28) na Brazil (Desemba 2) itafuata.

Kikosi kilichotangazwa na mlinzi wa zamani wa Liverpool, Rigobert Song kilimshuhudia Nicolas Nkoulou akiitwa tena baada ya kukosekana kwa miaka mitano na Mbeumo kati ya wachezaji 11 waliocheza mechi tano au pungufu.

"Ni vigumu kwa sababu unakutana na wachezaji wapya, bado unahitaji kujenga uhusiano kwa kila mmoja," alisema Mbeumo, ambaye mara kwa mara hutoa nafasi katika ngazi ya klabu.

"Inachukua muda na bila shaka itakuwa ngumu. Nataka mahusiano mazuri na wachezaji wenzangu."

Amejiunga na kundi la WhatsApp la Cameroon ili kujua kikosi kilichosalia zaidi, hasa kwa vile mchezaji pekee wa Indomitable Lion - Olivier Ntcham wa Swansea City – ndiye mwenye makao yake Uingereza.

Bryan Mbeumo of Brentford celebrates his goal, alongside teammate Ivan Toney, in the 5-2 home win over Leeds United in September 02022.

Chanzo cha picha, Getty Images

Huku akitarajia mechi ngumu kutoka kwa Uswizi – yenye "kazi nzuri sana katika Ulaya," - na Serbia - "nzuri sana na thabiti" - Mbeumo haamini kuwa Cameroon inahitaji kukusanya pointi zao zote kabla ya mchuano wao wa mwisho na Brazil.

"Sidhani hilo ndilo lengo. Tunapaswa kulenga makubwa, ndoto kubwa kwani hatutaki tu kuwa sehemu ya shindano hili - tunataka kufanya kitu."

Maneno yake yanazidisha malengo ya Eto'o, ambaye uwezo wake mkubwa ulirejesha mabao 205 katika mechi 336 alizochezea Barcelona na Inter Milan.

Kinyume chake, umaliziaji wa Mbeumo unaweza kuwa mbaya, kama ilivyosisitizwa na yeye kugonga nguzo mara nane msimu uliopita, na anakiri kumuuliza Eto'o vidokezo.

Wote watatumai hawa hili watalifanyia kazi huku rekodi ya Afrika ya kufuzu mara nane ya Kombe la Dunia ikijaribu kutinga hatua ya mtoano kwa mara ya pili pekee.

Nafasi ya kweli zaidi ya kupata medali ya fedha inakuja 2024 wakati Ivory Coast watakapoandaa Kombe lijalo la Mataifa, mashindano ambayo Mbeumo pia hawezi kusubiri kuyafurahia.

"Kucheza Kombe la Mataifa ni kitu kikubwa sana barani Afrika, kwa hivyo kitakuwa kitu kizuri sana - nina furaha."

Huku fainali mbili kuu zikikaribia katika miezi 14 ijayo, ni mwanzo kabisa kwa Indomitable Lion ya hivi sasa katika soka ya Afrika.