Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muswada wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda kuwa sheria baada ya miezi kadhaa ya mvutano
Na Jennifer McKiernan
Mwandishi wa habari za siasa
Mswada mkuu wa Rishi Sunak wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda unatarajiwa kuwa sheria baada ya miezi mitano ya mzozo wa ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza na bunge katika Westminster.
Unaielezea Rwanda kuwa nchi salama na sehemu muhimu ya mipango ya serikali ya kuwapeleka baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi Uingereza.
Mswada huo umekosolewa vikali na vyama vya upinzani lakini baada ya mijadala kadhaa wabunge wa Uingereza (the Lords) walitupilia mbali pingamizi zao dhidi yake Jumatatu jioni.
Bw Sunak amesema safari za ndege za kuelekea Rwanda zitaanza ndani ya wiki 10 hadi 12, baada ya kushindwa lengo lake la awali ambapo safari hizo zilitarajiwa kuanza kati ya mwezi wa Septemba na Disemba mwaka jana.
Lakini safari za kuondoka bado zinaweza kusimamishwa na mahakama au kucheleweshwa kwa ajili ya kupata ndege ambazo zitatumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao hadi Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Ndani James Cleverly alisema kupitisha mswada huo ni "wakati wa kihistoria katika mpango wetu wa kuzuwia mashua."[za wahamiaji kuingia Uingereza].
Katika video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, alisema: "Niliahidi kufanya kile kilichohitajika ili kuruhusu safari ya kwanza ya ndege. Hilo ndilo tumefanya."Sasa tunafanya kazi siku baada ya siku ili kuhakikisha ndege zinaweza kuondoka ."
Lakini waziri kivuli wa mambo ya ndani Yvette Cooper aliuita mpango wa Rwanda "ujanja wa gharama kubwa’’.
Mipango ya serikali imekwama tangu Novemba 2023, wakati Mahakama ya Juu ya Uingereza ilipoamua kwa kauli moja kwamba mpango huo wa kuwapeleka wahamiaji wanaotafuta hifadhi Uingereza nchini Rwanda haukuwa halali .
Mapema Jumatatu, waziri mkuu alisema safari za ndege zimepangwa zimepangwa kuanza tu sheria hiyo itakapopitishwa na wafanyakazi 500 wako tayari kuwasindikiza wahamiaji "njia yote hadi Rwanda".
"Mipango iko tayari. Na safari hizi za ndege zitafanyika , hata iweje," alisema, akiongeza kuwa alitaka " safari nyingi za ndege zifanyike kwa mwezi ... kwa sababu ndio njia ya kuweka kizuizi cha kimfumo na ndivyo utakavyozuia mashua kuingia".
Bw Sunak alikuwa ameapa kuwazuia wabunge kufanya kazi usiku kucha ikibidi ili kupitisha mswada wake na kuhakikisha safari za ndege za kuondoka Uingereza kuelekea Rwanda zinaanza.
Mwishowe, baada ya mswada huo kukwamishwa mara kadhaa na wabunge na pia maafisa wenzake kuupinga mara tano waliamua kutompinga tena , huku mjadala wa mwisho ukikamilika muda mfupi baada ya saa sita usiku.
Hii inamaanisha kuwa serikali iliweza kufanikiwa katika azma yake , licha ya ukosoaji mkali kutoka kwa vyama vya upinzani na wabunge kutoka pande zote za kisiasa.
Baada ya pingamizi nyingi, kupitishwa kwa mswada huo kulikuwa ni ushindi wa kisiasa kwa Rishi Sunak.
Huku uchaguzi mkuu ukikaribia, waziri mkuu hana muda mrefu wa kuthibitisha iwapo mpango wake utafanya kazi kwa ufanisi.
Mwanzoni mwa siku, wwabunge walikuwa wakishikilia marekebisho mawili – la kwanza, kutoka kwa mbunge Lord Anderson, kuhusu suala la uhakiki huru na unaoendelea wa hali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki iwapo ni salama.
Lord Anderson aliungwa mkono na mbunge Lord Carlile ambaye alisema: "Hili ni jambo ambalo halijachukuliwa vibaya, limeandaliwa vibaya, lisilofaa, kinyume cha sheria katika sheria za sasa za Uingereza na za kimataifa, na Baraza la bunge ni sawa kabisa kusema kwamba tunataka kudumisha viwango vyetu vya kisheria nchi hii, na kuna njia bora zaidi za kushughulikia tatizo hili hata hivyo."
End of Unaweza pia kusoma:
'Mkataba muhimu sana'
Marekebisho mengine, kutoka kwa mbunge Lord Browne wa Ladyton, yalikuwa juu ya kuwaachilia wanajeshi wa zamani wa Afghanistan ambao walikuwa wamelisaidia jeshi la Uingereza lisiondolewe Afghanistan.
Mbunge huyo wa chama cha Labour alikosoa mtazamo wa serikali na kumtaka msemaji wa serikali Lord Sharpe kurudia ahadi yake ya hapo awali, ambapo alisema wanajeshi hao wa Afghanistan ambao wana "uhusiano wa kuaminika" na vikosi maalumu vya Afghanistan watatathiminiwa upya madai yao na chombo huru na kusema wale walio na madai yaliyothibitishwa hawatarejeshwa makwao.
Mbunge Lord Browne alisema haya yalikuwa "makubaliano muhimu sana", ingawa ilimbidi "kuwaamini kwa neno lao" kwani ahadi hiyo haikufanikiwa katika maneno ya kisheria, na aliamua kuachana na mapendekezo yake ya marekebisho.
Huko nyuma katika Bunge la Commons, waziri kivuli wa uhamiaji Stephen Kinnock alisifu "ustahimilivu" wa wenzake katika bunge kwa kushikilia kile alichokiita "makubaliano makuu".
Lakini serikali ilishikilia msimamo wake kwa kukataa moja kwa moja marekebisho ya mwisho.
Kwa kuwa muswada huo ulirejeshwa tena katika Ikulu ya Westminster, mbunge Lord Anderson aliamua kusitisha madai yake kuhusu marekebisho.
Akizungumza katika kile kilichoitwa "mazishi" ya marekebisho ya mwisho, alisema: "Madhumuni ya mjadala wa vuta ni kuvute ni kuishawishi serikali, kwa nguvu ya hoja, kuja meza na kukubaliana maelewano.
"Wamekataa moja kwa moja kufanya hivyo... Wakati umefika sasa wa kukiri ukuu wa baraza lililochaguliwa na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho."
Akitetea mswada huo, waziri wa Mambo ya Ndani mbunge Lord Sharpe wa Epsom alisema unafuata sheria za kimataifa na kwamba "ni maadili mema na uzalendo kutetea uadilifu wa mipaka yetu".
Mswada huo unatarajiwa kuidhinishwa na Mfalme Charles katika siku chache zijazo, na kuupitisha rasmi kuwa sheria.
Sio tu vyama vya upinzani ambavyo vimepinga mpango wa serikali ya Rwanda, mashirika ya haki za binadamu yanasema mpango huo unaleta "tisho kubwa kwa utawala wa sheria" kwa kudhoofisha kile kinacholinda watu dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka na serikali.