Ni nini huwafanya mashabiki kuwarushia vitu wasanii jukwaani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Fikiria kuwa unacheza jukwaani mbele ya maelfu ya watu, na unashangaa mtu fulani katika hadhira anapokutupia kitu.
Ni kama vile kumekuwa na video inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii kila wikendi, inayomuonesha mdau akiwarushia wasanii vitu ya ajabu na tofauti wakati wanatumbuiza.
Cardi B alikua nyota wa hivi karibuni zaidi kuvuma wakati mtazamaji alipommwagia kinywaji chake wakati wa tamasha lake la Las Vegas.
Lakini rapper huyo alichukua hatua mikononi akajibu kwa kumtupa
kuwarushia maikrofoni yake kutoka stejini.
Mwanaume anayetuhumiwa kwa tukio hilo alisema alidhani kitakuwa kitendo cha kuchekesha, lakini sivyo ilivyo kwa wasanii wengi.
Harry Styles alipigwa jichoni na kipande cha peremende kwenye tamasha mnamo Novemba mwaka jana, na Pink alikasirika wakati mtazamaji alipotupa mfuko wa majivu ya binadamu kwenye jukwaa.
Mwimbaji mzuri Ava Max alipigwa kofi stejini, na mtu akamtupia bangili mwimbaji Kelsey Ballerini.
Tukio la Kelsey lilimfanya mwimbaji Charlie Puth kuwasihi mashabiki kwenye Twitter, "Mtindo huu lazima ukome, ni ukosefu wa heshima na hatari sana."
Hivi kwanini baadhi ya mashabiki wanalipa pesa kwenda kuwaona wasanii, na kuwarushia vitu?!

Chanzo cha picha, BEBE REXHA / INSTAGRAM
Dkt. Lucy Bennett ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Cardiff akiangalia uhusiano kati ya mashabiki na waimbaji wanaowapenda.
Anasema kuwa mshikamano wa mashabiki unaweza kujenga hisia ya "mali" ndani ya jumuiya yao na kuwaruhusu "kujieleza wao ni nani".
"Lakini, nadhani kuna kitu kimeanza kubadilika hivi karibuni," aliiambia BBC Newsbeat. "Tunaona vitendo vya mashambulizi vinavyosumbua na kuharibu zaidi na zaidi kama vile kuwarushia wasanii vitu."
Anasema pia kwamba mitazamo ya watu inaweza kuwa imebadilika tangu janga la Covid "kwamba hatuwezi kuwa kwenye matamasha".
Naye Bennett anaamini kuwa baadhi ya watu hufanya hivyo kwa sababu ni vigumu kwa wasanii kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo cha picha, SYMPHORIEN DEMORES
Kurusha vitu kwenye jukwaa sio jambo pekee ambalo hadhira hufanya ili kuwaudhi wasanii.
Lucy May Walker ni mwimbaji ambaye nyimbo zake zilionekana katika mfululizo wa filamu za kuvutia, lakini kwenye matamasha yake anaona kuwa mashabiki hawajali vya kutosha.
Anasema, "Nilichukia kucheza muziki, kwani niliweka hisia zangu zote ndani yake, na ninasikia tu sauti za watu wakizungumza ninapocheza."
"Unapaswa kuwaambia kwa upole sana bila wao kukuchukia."
"Ikiwa watazamaji wote walikuwa wanazungumza ni afadhali nicheze kwenye chumba kisicho na kitu."
Kulingana na Dk. Bennett, baadhi ya mashabiki huchukua hatua mikononi mwao ili "kuhakikisha tabia njema inakuwepo wakati wa tamasha".
Hivi karibuni tuliona mafunzo ya adabu ya tamasha yaliyoundwa na mashabiki wa Taylor Swift.
"Labda tutaona juhudi zaidi za mashabiki wenyewe kuhakikisha heshima kubwa kwa wasanii wanapokuwa wakicheza jukwaani."












