Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Bayern inamfukuzia Marc Guehi Crystal Palace
Bayern Munich imejiunga kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Crystal Palace Marc Guehi, Palace wanapanga kumpa Adam Wharton mkataba mpya nao Napoli wa Italia wanamwinda Kobbie Mainoo kwa mkopo kutoka United.
Miamba ya Ujerumani Bayern Munich wamejiunga kwenye msururu wa timu kadhaa Ulaya zinazoitaka saini ya beki wa kati wa Crystal Palace Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25 .Mkataba wake Guehi raia wa England unatamatika mwisho wa msimu huu na ikumbukwe kuwa nusra ahamie Liverpool katika siku ya mwisho ya uhamisho mwezi uliopita. (Sky Germany)
Napoli ya Italia inaongoza msafara wa timu zinazomtaka kiungo wa Manchester Unite Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 20 kwa mkopo mwezi Januari. Napoli wameendeleza mazungumzo ya karibu na United tangu msimu wa uhamisho ya majira ya joto ulipoisha. (Sky Switzeland)
Meneja wa Fulham Marco Silva analengwa pakubwa na klabu ya Nottingham Forest iwapo watampiga kalamu Ange Postecoglou kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo. Hata hivyo itakuwa vigumu kwa Forest kumpata kabla mwisho wa msimu huu.(Mail)
Mancheser United wana imani kuwa Lisandro Martinez mwenye umri wa miaka 27 atapona jeraha la goti alilopata msimu huu kabla ya mwisho wa mwaka. Beki huyo wa Argentina hajacheza hata mechi moja kwa United katika mudabwa miezi nane. (Mail)
Vigogo wa Uhispania Barcelona huenda wakajaribu kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya Ujerumani Karim Adeyemi mwenye umri wa miaka 23 ajiunge nao kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka 2027 (Sky Switzerland)
Manchester City wa England hawana azma yoyote ya kumuuza kiungo wao wakati Rodri mwenye umri wa miaka 29. City wamepuuza taarifa za kutaka kumpiga bei kwa Real Madrid ya Uhispania. (Teamtalk)
Manchester United inamtazama kwa jicho la tatu Unai Emry kuwa mtu sahihi kabisa kuchukuwa nafasi ya Ruben Amorin iwapo italazimika kumfuta kazi Kocha huyo kutoka Ureno. (Fichajes)
Real Madrid hawana nia ya kuanzisha biashara ya kiungo wa kati kutoka Uturuki Arda Guler ,20, licha ya Arsenal na Newcastle kuonyesha azma ya kumsajili.(Football Insider)
Barcelona na Juventus wana azma za uhakika kumsajili kiungo wa Mancheser City Bernado Silva ,31, huku vilabu vya Saudia kama Al Ahli,Al Qadsiah na Al Nassr vyote vikijipanga kuvunja akaunti zao za benki ili wamsajili mkataba wake utakapoisha mwaka 2026. (Caught offside)
Imetafsiriwa na Ahmed Bahajj na kuhaririwa na Ambia Hirsi