Tetesi za Soka Jumanne: Man Utd na Man City wanamtaka Olmo

Chanzo cha picha, Getty Images
Jaribio la Barcelona lililoshindwa la kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Dani Olmo kwa kipindi cha pili cha msimu limefungua milango kwa Manchester United na Manchester City kumsajili mchezaji huyo wa miaka 26 bila malipo.(Mundo Deportivo - in Spanish)
Real Madrid wangependelea kumsajili beki wa kulia wa England Trent Alexander-Arnold mwezi Januari, lakini wako tayari kusubiri hadi msimu wa majira ya kiangazi wakati mkataba wake utakapomalizika ikiwa Liverpool hawataki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwezi ujao.(Marca - in Spanish)
Mshambulizi wa Newcastle raia wa Uswidi Alexander Isak yuko tayari kusalia katika klabu hiyo iwapo watamaliza katika nafasi nne za juu za Ligi ya Primia msimu huu, na kutoa pigo kwa Arsenal ambao wana nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (JSun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa Ipswich Muingereza Liam Delap, 21, na mshambuliaji wa Brighton wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, wakati wanatazamia kutoa ushindani kwa mshambuliaji ambaye ni chaguo la kwanza Nicolas Jackson. (Talksport)
Meneja wa West Ham Julen Lopetegui atapewa muda zaidi licha ya kiwango kibovu cha wagonga nyundo hao msimu huu. (Telegraph - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Cristiano Ronaldo amekataa kudhibitisha kuwa hataondoka Al-Nassr msimu wa kiangazi, huku mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 39 akiwa huru kufanya mazungumzo na vilabu vingine kuanzia Januari 1. (Marca- in Spanish)
Newcastle wanapanga kumnunua kipa wa Burnley mwenye umri wa miaka 22, James Trafford kwa kitita cha pauni milioni 20. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wolves wamelemnga kumhamisha mlinzi wa Lens wa Austria, Kevin Danso, 26, kati mwezi Januari. (Sky Sports)
Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomtazama kwa karibu kiungo wa kati wa Manchester City Mwuingereza mwenye umri wa miaka 22, James McAtee. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham hawana uwezekano wa kubadilisha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 28, kuwa mkataba wa kudumu, kumaanisha kwamba atarejea RB Leipzig msimu wa kiangazi (Bild - in Germany)
Athletic Bilbao wamemtambua kiungo wa kati wa Norwich Mhispania Borja Sainz, 23, kama kiungo mbadala bora wa Nico Williams, iwapo winga huyo wa Uhispania, 22, ataondoka katika klabu hiyo msimu wa jkiangazi. (Sport - In Spanish)
AC Milan na Napoli ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinaweza kumnunua mshambuliaji wa Nottingham Forest Chris Wood, 33 , iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa New Zealand atashindwa kukubaliana na klabu hiyo kandarasi mpya. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Juventus zimeonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili beki wa Barcelona mwenye umri wa miaka 28 kutoka Denmark Andreas Christensen mwezi Januari. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Newcastle wako katika nafasi nzuri ya kufanikisha usajili wa beki wa England Fikayo Tomori, 27, kutoka AC Milan mwezi Januari. (Caught Offside)
Manchester United wanaendelea kufuatilia maendeleo ya beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 21 kutoka Hungary, Milos Kerkez. (Fabrizio Romano)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












