Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mizizi ya Urusi barani Afrika inavyokuzwa kwa safari ya Lavrov nchini Mali
- Author, Beverly Ochieng
- Nafasi, BBC News
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameahidi kuendelea kuiunga mkono kijeshi Mali, ambayo imekuwa ikipambana na waasi wa kijihadi tangu mwaka 2012.
Mwaka jana, Mali iliwageuka watawala wake wa zamani na kuonesha kupendelea kupata usaidizi kutoka kwa Urusi badala ya Ufaransa.
Hii ni ziara ya pili ya waziri huyo wa mambo ya nje barani Afrika katika kipindi cha wiki mbili.
Urusi inalenga kuimarisha washirika huku vita vya Ukraine vikiendelea, lakini ushiriki wake katika nchjini Afrika Magharibi ulionza hata kabla ya vita umekuwa ukiongezeka kwa muda sasa.
Bw Lavrov, ambaye yuko katika safari ya siku mbili nchini Mali, alielezea nia ya Moscow ya kutoa msaada wa kijeshi kwa serikali kote Afrika Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu.
Serikali ya kijeshi ya Mali imepuuzia ukosoaji wa kuhamia kwa Urusi.
"Hatutahalalisha tena uchaguzi wetu wa mshirika. Urusi iko hapa kwa mahitaji ya Mali na inajibu kwa ufanisi mahitaji yetu ya kimkakati," Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Urusi.
Sasa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu wapiganaji wa Wagner Group waanze kufanya kazi nchini Mali, ingawa mamlaka haijawahi kuthibitisha rasmi hili.
Lakini ushahidi unaonyesha kwamba hawajafanikiwa zaidi kuliko vikosi vingine katika kukabiliana na tishio la muongo wa wanajihadi na ukosefu wa usalama unaweza kuwa mbaya zaidi.
Majeruhi wa kiraia kutokana na ghasia waliongezeka zaidi ya mara mbili mwaka jana, kulingana na data kutoka kwa shirika la Acled Info.
Mbeleko kwa Moscow
Hata hivyo, utawala wa kijeshi wa Mali umepuuzilia mbali ripoti kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama wa nchi hiyo ikisema ni "habari za uwongo".
Badala yake imeitaka Moscow kwa kuwapa uwezo wanajeshi wa Mali baada ya kupeleka vifaa vizito vya kijeshi huko Bamako mara kadhaa tangu jeshi lilipochukua mamlaka mnamo Agosti 2020.
Hizi ni pamoja na ndege za kivita za Sukhoi, pamoja na helikopta za kupambana na waasi.
"Mafanikio ya kijeshi tuliyopata katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yanapita yote yalifanywa katika miongo iliyopita. Silaha zetu ni fahari ya taifa zima," Rais wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goïta alisema katika hotuba yake katika siku ya jeshi mwezi uliopita.
Alisema kuwa watu wameweza kurejea majumbani mwao lakini hakutoa mifano mahususi.
Hata hivyo, uwepo wa mamluki wa Urusi ulisimamisha ghafla muongo mmoja wa juhudi za Ufaransa na washirika wake wa Ulaya kuimarisha majaribio ya Mali ya kukabiliana na wanajihadi.
Kutumwa kwa kundi la Wagner kulitokana na kupungua kwa vikosi vya Ufaransa ambavyo vilikuwa vimepiga hatua kubwa dhidi ya wanamgambo tangu vimetumwa kwa mara ya kwanza mnamo 2013.
Takribani watu 700 waliuawa katika visa vilivyohusisha mamluki hao, hasa katika maeneo ya katikati ya nchi ya Mali.
Moja ya idadi kubwa zaidi ya vifo ilikuja mnamo Machi 2022 wakati takriban watu 300 waliripotiwa kuuawa katika operesheni za kukabiliana na waasi katika mji wa kati wa Moura.
Walionusurika waliambia Human Rights Watch kwamba wanajeshi wa Mali na "askari weupe waliokuwa wakizungumza kwa lugha ngeni" waliwaua kwa ufupi makumi ya askari.
Mafanikio ya mitandao ya kijamii
Ikiwa imetiwa moyo na kazi zao nchini Mali pamoja na mafanikio yake katika kushawishi maoni ya umma, Wagner imefanya mapinduzi kwa Burkina Faso - ambayo ilikumbwa na mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka 2022 - na pengine Ivory Coast.
Lakini wasiwasi umeibuliwa kuhusu jinsi wapiganaji wa kundi la Wagner wanavyofanya kazi na Umoja wa Mataifa umetaka uchunguzi ufanyike kuhusu uhalifu wa kivita unaoweza kufanywa na wanajeshi wa Mali na mamluki, jambo ambalo mamlaka ya Mali inakanusha mara kwa mara.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yameandika ripoti za mateso, mauaji na unyanyasaji wa kingono wakati wa operesheni za pamoja za kukabiliana na waasi zinazoitwa Keletigui zilizoanza Desemba 2021.
Uchambuzi wa data kutoka Acled unaonyesha kuwa raia walikufa kwa idadi kubwa kuliko wapiganaji katika operesheni kama hizo mnamo 2022.
Urafiki wa Urusi unaochanua Afrika
Katika ziara yake nchini Mali, Bw Lavrov alieleza jinsi "vifaa vya anga vya Urusi" vilitumiwa "kutekeleza operesheni zilizofanikiwa dhidi ya magaidi katika siku za hivi majuzi".
Lakini pengine kikubwa zaidi, alidokeza kwamba Urusi inaweza kuwasaidia wengine katika eneo hilo wanaokabiliana na tishio sawa la wanajihadi akisema kwamba "hili linahusu Guinea, Burkina Faso na Chad na eneo la Sahel kwa ujumla na hata mataifa ya pwani kwenye Ghuba ya Guinea".
Katikati ya kutengwa kwa Urusi kimataifa kufuatia uvamizi wake wa Ukraine, kwa hatua hii kwa nchi za Afrika ni kama ni urafiki ambao unaweza kuchanua tu.