Nyumba gani kati ya nyingi za kifalme atakayoishi Mfalme Charles wa Uingereza?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna marupurupu mengi unapata ukiwa mfalme. Moja wapo ni ondoa hofu kuhusu utalala na kuishi wapi.
Pamoja na majumba mengi yanayojulikana sana, nyumba zilizoko kwye himaya ya Mfalme Charles III ni pamoja na baadhi ya nyumba za kawaida - za kawaida kwa viwango vya kifalme.
Baadhi ni kwa sababu ya kazi ama cheo chake na nyingine zinamilikiwa binafsi na mfalme mwenyewe. Pia kuna majengo ya Duchy ya Cornwall, mali binafsi ya Mwanamfalme wa Wales, ambayo alifanya nyumba yake wakati wa jukumu hilo.
Kwa vitendo, bila shaka, hataweza kuishi kote. Na waangalizi wa Kifalme wanasema Mfalme mwenyewe hana nia ya kujaribu kufanya hivyo.
"Mfalme kuwa kuishi Kifalme katika makazi mengi wakati Uingereza inakabiliwa na gharama ya maisha ni ngumu," anasema Anna Whitelock, profesa wa historia ya ufalme katika Chuo Kikuu cha London. Mfalme anasemekana analijua hilo na anatarajiwa kuyarejesha mengi kwa matumizi ya wageni wa ziada.
Kwa hivyo ni wapi Mfalme anaweza kuchagua kuishi?
Kasri la Buckingham

Chanzo cha picha, Getty Images
Jengo kubwa lililoko katikati mwa jiji la London lenye vyumba 775 ni mojawapo ya alama maarufu za Familia ya Kifalme. Pia ni makao makuu ya utawala wa ufalme wa Uingereza tangu 1837, ambapo wageni wapatao 50,000 hualikwa kwenye hafla rasmi za kifalme kila mwaka na kwa sasa linafanyiwa ukarabati mkubwa.
Windsor Castle

Chanzo cha picha, Getty Images
Inasemekana kuwa ngome kubwa na kongwe zaidi duniani, Windsor ilikuwa nyumba aliyopenda kuitembelea Malkia Elizabeth II mwishoni mwa wiki na ikawa makazi yake makuu mara tu janga la Covid lilipoanza. Ni muda gani Mfalme mpya atatumia kukaa huko, hata hivyo, ni jambo la kusubiri kuona.
Kasri la Holyroodhouse

Chanzo cha picha, Getty Images
Malkia Elizabeth alitumia wiki moja kwenye jumba hili kila mwaka kuandaa hafla rasmi na za serikali, kama alivyofanya Mfalme Charles alipokuwa Mwanamfalme wa Wales. Ina vyumba 289, kati hivyo 17 viko wazi kwa ajili ya umma.
Ngome ya Hillsborough

Chanzo cha picha, Alamy
Ni jumba linaloweza kuwa limeangaziwa kwa sababau ya tukio la hivi karibuni wakati Mfalme alipotumia kalamu iinayovuja wakati wa ziara. Ngome ya Hillsborough ni makazi yake rasmi huko Ireland Kaskazini - pia ni mahali pa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland kaskazini.
Kwa hivyo, mazungumzo muhimu kuhusu mchakato wa amani wa Ireland ya Kaskazini yalifanyika huko. Nyumba ya kabla ya karne ya 18 iko katika ekari 100 za bustani na ni kivutio maarufu cha wageni.
Jumba la Highgrove

Chanzo cha picha, Getty Images
Charles alihamia kwenye jumba hili la Gloucestershire mwaka 1980 na kulifanyia marekebisho. Mkewe marehemu Diana alisemekana hakuwa analipenda, lakini kulingana na Prof Whitelock, jumba hili na lile la Clarence - palionekana mahali ambapo mfalme huo alipofurahia zaidi.
Jumba la Sandringham

Chanzo cha picha, Getty Images
Tofauti na makazi mengine mengi ya kifalme, jumba hilo la Norfolk linamilikiwa binafsi na mfalme, baada ya awali kununuliwa na Mfalme Edward VII na kurithishwa kwa warithi wake. Marehemu Malkia alitumia majira yake ya baridi katika jumba hili na Siku ya Krismasi ya Familia ya Kifalme inatembelea huko. Charles alichukua uendeshaji wa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 20,000 mwaka 2017.
Balmoral

Chanzo cha picha, Getty Images
Balmoral Estate pia inamilikiwa binafsi na familia ya mfalme. Ilitengenezwa na Malkia Victoria na Mwanamfalme Albert, Mnara Mkuu wa ngome hiyo unakaribia kufikia futi 100 (30.5m) kaskazini mashariki mwa Scotland.
Malkia Elizabeth, ambaye alifariki huko tarehe 8 Septemba, alikuwa akitumia mara kwa mara miezi ya majira ya joto kwenye jumba hilo.
Jumba la Clarence

Chanzo cha picha, Getty Images
"Jumba la Clarence ni jumba lililonakshiwa zaidi kuliko makazi yote huko London," anasema Lacey. Lakini Mfalme anasemekana kuipenda sana. "Ina mgusa sana kwa sababu bibi yake mpendwa aliishi huko," anasema Lacey. Ilikuwa pia makazi yake rasmi ya London kati ya 2003 na 2022.
Llwynywermod

Chanzo cha picha, Alamy
Jumba hili , ambalo liko nje kidogo ya Hifadhi ya Kitaifa ya Brecon Beacons huko Carmarthenshire, ilinunuliwa na Duchy ya Cornwall mnamo 2006. Nyumba ya vyumba vitatu ilibadilishwa kwa matumizi ya Mfalme Charles na Camilla, Malkia Consort. Wanandoa hao hukaa huko wakati wa ziara zao katika nchi ya Wales na Mfalme amekuwa akitembelea eneo hilo.
Jumba la Dumfries

Chanzo cha picha, Getty Images
Nyumba sio makazi rasmi makazi ya Kifalme, lakini Mfalme alikuwa akiishi hapa alipoambiwa mama yake alikuwa mgonjwa sana kabla ya kusafirishwa kwa helikopta hadi Balmoral.
Ukiacha haya yapo mengine mawili Castle of Mey na Tamarisk House ambayo Mfalme Charles anaweza kuchagua kuishi pia.












