Wanafunzi sasa wageukia Akili Bandia kujifunza lugha mbali mbali

yyy

Chanzo cha picha, CHRISTINE RO

Maelezo ya picha, Christine Ro anatumia programu ya ChatGPT kujifunza Kihispania

Christine Ro mwanafunzi mmoja anamsimulia rafiki yake rai wa Argentina kwamba amekua akitumia programu ya ChatGPT ya akili bandia kufanya mazoezi ya ligha ili kuweza kufahamu vizuri Kihispania, na kukiri kwamba programu hiyo ina uwezo mkubwa.

Programu hii inaweza kunikosoa pale ninapo kosea na kunielekeza vizuri tofauti iliopo kati ya lugha ya kihsapnia kinachozungumzwa au kutumika katika maeneno tofauti kama Mexico, argentina na hata kile kispania kilichochanganyika na kingereza ambacho chenyewe kinaitwa Spanglish.anasema Christine

Rafiki yangu aliejitolea kinifundisha kihispania anauliza kama nimemsahau na kupata mbadala wake

Hata sijafanya hivyo, anaongeza kunatofauti kubwa ya kujifunza kupitia pogramu hii ya ChatGPT na ukiwa unafundishwa na mtu , kuna raha ya kufundishwa n binadamu kwa sasabu kuna mengi ya kukosoana na kisha kucheka na kuendelea na masomo.

Mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao wamengundua urahisi wa kujifunza lugha mbali mbali kupitia programu hii ya akili bandia siku za hivi karibuni’’ ,anaongeza .

Raia mmoja wa Kosta Rika anayefanya kazi katika tasnia ya ujenzi anasema kwamba matumizi yake ya misamiati hasa katika lugha ya kingereza yameongezeka maradufu tangu alipongundua programu hiyo , jambo analofurahia zaidi ni kwamba anapat msaada mkubwa likija kwenye suala la kutafuta neno mbadala au anapotaka kuelezea maana ya neno kiundani.

Mmiliki mmoja wa Mgahawa huko Afrika Kusini ameenda mbali zaidi katika kuboresha sarufi yake ya Kihispania kwa usaidizi wa AI. Alikuwa na wakati mgumu kupata njia mbadala ya kujifunza kihispiania hasa wakati wa kusoma lugha yenyewe kutokana na kukabiliwa na tatizo linaloathiri namna anavyo wasiliana na watu.Jambo hilo lilimlazimu kutumia programu ya hiyo ya ChatGPT .

Wabunifu wa programu hii ya akili bandia wamechangamkia hatua hii ya kuvutia, na sasa kuna programu nyingi ambazo zimetumia zinaunganishwa na programu ya Akili bandia ili kuweza kujifunza lugha ngeni na zimekua na msaada mkubwa kwa wanafunzi wengi wenye nia ya kujifunza lugha .

Blanka Klímová, profesa mshiriki wa isimu katika Chuo Kikuu cha Hradec Králové nchini Cheki, anasema kwamba programu ya Replika imekuwa muhimu kwa wanafunzi wake kutumia Kiingereza kisicho rasmi.

Kila kitu kizuri hakikosi kasoro, Blanka anasema licha ya kuwa chabbot ilikua nzuri lakini kuna vitu vingine vilikua vinakosekana , kwa mfano maongezi yana jirudia na hata ukikosea haukosolewi na kibaya zaidi wakati mwingine programu hiyo ilikua ikitoa maelekezo kwa wanafunzi kuweka picha zoa za kuvutia. "Hii ilikuwa kama ikiukwaji wa haki za binadamu.

yyy

Chanzo cha picha, CHRISTINE RO

Maelezo ya picha, Mazungumzo katika programu ya kujifunza lugha ya AI, Tutor Lily
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kinyume chake, mojawapo ya chatbots maalum za kujifunza lugha ni LangaI, iliyozinduliwa mwezi Machi na Federico Ruiz Cassarino. Bw Ruiz Cassarino alitumia tajriba yake mwenyewe ya kujifunza Kiingereza baada ya kuhama kutoka Uruguay hadi Uingereza. Ustadi wake wa Kiingereza uliimarika sana kutokana na kuongea kila siku, ikilinganishwa na mbinu nyingi za kitaaluma. Sasa anatumia programu yake mwenyewe kujifunza lugha ya kiitaliano .

Watu wengi hujisahau kuhusu kufanya makosa katika lugha ambayo hawazungumzi kwa shida, hata kwa mwalimu, Bw Ruiz Cassarino anabainisha. Lakini chatbot haitakukosoa. Na matumizi kwa kaisi kikubwa ya AI inayozalisha ni ya juu sana kwamba inaweza kuwaboresha watumiaji wa programu hiyo .

Baada ya matumizi ya akili bandia kuanza kushika kasi , sasa sio lazima usome au kutumia maandishi yanayoweza kukufanya uchukie kujifunza lugha mpya, badala yake unaweza kusema kile kinachokufurahisha jambo linalo rahisisha mno hatua nzima ya kujifunza lugha mpya na kuifanya kuoneka suala jepesi.

Ingawa wanafunzi wengi wanaojifunza lugha mpya wanatumia chatbots maarufu kama ChatGPT na Bard kufanya mazoezi, Bw Ruiz Cassarino anaamini kuwa programu mahususi za kupata lugha kama yake ni muhimu.

"Tulifanya kazi kwa bidii sana kufanya hii iwe maalum kwa mtu ambaye anataka kujifunza lugha," anasema. Wataalam wetu walirekebisha matumizi ya LangaI ili kuendana na viwango vya msamiati wa watumiaji, iliongeza uwezo wa kufanya masahihisho wakati wa mazungumzo, na kuwezesha ubadilishaji wa matamshi kuwa maandishi.

Kulingana na Bw Ruiz Cassarino, wanaona idadi ya watu ikiongezeka kila uchao na idadi hiyo ni ya kuvutia hasa kwenye programu zinazojihusiha na elimu. Kati ya watumiaji wanaojaribu programu kwa takriban dakika 10, takriban asilimia 45 bado watakuwa wakiitumia mwezi mmoja baadaye. Sasa zinalenga katika kujenga msingi wa wasajili wa watu walio tayari kulipia matumizi bila kikomo.

Assoc Prof Klímová, ambaye pia ni mwanachama wa mradi wa utafiti wa Lugha hasa karne hii ambayo watu wanageukia matumiazi ya akili bandia , ametathmini matumizi na manufaa ya programu ya chatbots za AI kwa wanafunzi wa lugha za kigeni. Utafiti huu unapendekeza kuwa chatbots za AI ni muhimu kwa ukuzaji wa msamiati, sarufi na ujuzi mwingine wa lugha, haswa zinapotoa maoni ya kusahihisha.

yyy

Chanzo cha picha, CHRISTINE RO

Maelezo ya picha, Baadhi ya programu nyingi za AI ya kujifunza lugha

Ili kuwa mbele na kuelewa zaidi, programu zilizoboreshwa za kujifunza lugha zimekuwa zikiunganisha AI kwenye mifumo yao wenyewe.programu ya lugha zaidi ya moja maarufu kama Duolingo alianza kushirikiana na OpenAI mnamo mwezi Septemba 2022, kwa kutumia GPT-4 ya kampuni hiyo.

Haiwezekani kwamba chatbot za AI zitachukua nafasi ya Duolingo kabisa. Joy Ehonwa, mhariri na mwandishi huko Lagos, hutumia sana programu ya Lunga1 zaidi ya moja Duolingo kujifunza Kifaransa.

Lakini hivi majuzi pia amekuwa akitumia chatbot ya AI iliyotengenezwa Nigeria kumsaidia boresha Namana anavyozungumza na kuandika Kifaransa.

Joy anaongeza kuwa namna anavyotumia programu ya Kainene vos Savant haina tofauti na jinsi ambavyo anavyoongea au kuwa na maongezi ya kawaida na binadamu.

Lakini kuna wale ambao wanakumbana na changamo kama Bi Ehonwa ya kujieleza , anasema mimi kila nikipata tatizo huwa nakimbilia programu ya chatbot kuuliza kwa nini programu hiyo muda mwengine huwa inashindwa kufanya mazoezi kwenye programu ya Duolingo, na haina uwezo wa kumsaidia kuelewa ni kwa nini jambo ambalo halikuwa sahihi lilikuwa sahihi. Anaenda mbali na kusema huwa yupo huru kutoa mawazo yake hasa anapofikiria kwamba jambo linapaswa kufanywa tofauti, na kwa matumaini makubwa Kainene anatoa maelezo kwa nini haiwezi kuwa jinsi ninavyotarajia kuwa, kama mzungumzaji wa Kiingereza."

yyy

Chanzo cha picha, AMAJU ADOM

Maelezo ya picha, Joy Ehonwa anasema chatbots ni nzuri katika kueleza nukta za lugha

Ikiwa majukwaa ya zamani ya kujifunzia lugha yana udhaifu, vivyo hivyo na ujifunzaji wa lugha unaoendeshwa na AI. Watumiaji wanaripoti kuwa chatbots wanafahamu vyema lugha za Ulaya zinazozungumzwa na watu wengi, lakini ubora unashusha hadhi kwa lugha ambazo haziwakilishwi mtandaoni au ambazo zina mifumo tofauti ya uandishi. Programu nyingi za kujifunza lugha za AI zinapatikana kwa seti chache za lugha.

Hata katika lugha za kawaida, chatbots hufanya makosa wakati mwingine hata kubuni maneno. Shida moja ni kwamba wanawasilisha maandishi kwa ujasiri sana, itakuwa rahisi kwa mwanafunzi mpya kuchukua kile wanachosema kuwa sahihi.

Emily M Bender, profesa wa isimu komputa katika Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani, ana wasiwasi, "Ni aina gani ya upendeleo na njia zisizofaa za kuzungumza kuhusu watu wengine wanaweza kuwa wanajifunza kutoka kwenye chatbot?" Masuala mengine ya kimaadili, kama vile faragha ya data, yanaweza pia kupuuzwa.

Bado, Assoc Prof Klímová anaamini kuwa kutakuwa na soko kubwa la teknolojia kama hizo. Na kama idadi ya wanafunzi wanaojifunza lugha, anadokeza kuwa GPT-4, inayopatikana kwa usajili unaolipishwa kwa ChatGPT, imepiga hatua za kushangaza kwenye usahihi.

Ingawa walimu wengi hawakubaliani, anaamini, "Ni suala la wakati ambapo akili bandia itachukua nafasi yetu kama walimu wa lugha za kigeni."

Ingawa hilo linaweza kusikika kuwa la kukithiri, "walimu bado watakuwa na jukumu muhimu kama washauri na wawezeshaji, hasa kwa wanaoanza kujifunza na wazee kwa vile walimu wana uelewa mkubwa wa mitindo ya kujifunza, mahitaji ya lugha na malengo ya kila mwanafunzi."

Itakuwa muhimu kwa walimu wa lugha kutathmini thamani iliyoongezwa ya AI na jukumu lao kuhusiana nayo, kadiri ujifunzaji wa hali ya juu zaidi wa kujielekeza unavyowezekana. Assoc Prof Klím