Hivi ndivyo diplomasia ya Urusi ilivyokufa chini ya Putin

Putin

Chanzo cha picha, Getty Image

Kuna wanadiplomasia wa Urusi waliwahi kuwa sehemu muhimu ya mkakati wa sera za kigeni za Rais Putin. Lakini hayo yote yamebadilika.

Katika miaka kuelekea uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, wanadiplomasia walipoteza mamlaka yao, majukumu yao yalipungua hadi kuanza kuimba pamoja maneno ya kichokozi ya Kremlin.

BBC inawauliza wanadiplomasia wa zamani, pamoja na maafisa wa zamani wa Kremlin na White House, jinsi diplomasia ya Urusi ilivyopotea ama kufa.

Mnamo Oktoba 2021, Ofisa mwandamizi wa Marekani Victoria Nuland alienda Moscow kwenye mkutano wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi. Aliyempokea alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Ryabkov, ambaye Bi Nuland alikuwa amemfahamu kwa miongo mingi na alishirikiana naye kila mara.

Wamarekani walimwona Bw Rybakov kama msuluhishi kwa vitendo na mtu mtulivu - ambaye wangeweza kuzungumza naye hata kama uhusiano wa nchi hizo mbili ulipoyumba.

Wakati huu, mambo yalikuwa tofauti.

Nuland

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, MwanadiplomasiaVictoria Nuland

Bw Ryabkov alisoma msimamo rasmi wa Moscow kutoka kwenye kipande cha karatasi na akapinga majaribio ya Bi Nuland ya kuanzisha mjadala. Bi Nuland alishtuka, kwa mujibu wa watu wawili waliokuwa wakijadili kisa hicho na yeye.

Alimtaja Bw Ryabkov na mmoja wa wafanyakazi wenzake kama "roboti" zilizo na karatasi", watu hao walisema (haya hivyo Marekani ilikataa kutoa maoni juu ya tukio hilo).

Na nje ya chumba cha mazungumzo, wanadiplomasia wa Kirusi walikuwa wakitumia lugha isiyo ya kidiplomasia.

"Tunatemea vikwazo vya Magharibi."

"Wacha niongee. Vinginevyo, utasikia kweli makombora ya Grad ya Kirusi yana uwezo?."

Haya yote ni nukuu kutoka kwa watu walio katika nyadhifa za mamlaka katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi katika miaka ya hivi karibuni.

Tumefikaje hapa?

Vita mpya baridi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Inaweza kuwa vigumu kufikiria kwa sasa, lakini Bw Putin mwenyewe aliwahi kuiambia BBC mwaka wa 2000 kwamba "Urusi iko tayari kushirikiana na Nato... ikiwemo hata kujiunga na muungano huo".

"Siwezi kufikiria nchi yangu kutengwa na Ulaya," aliongeza.

Mapema katika kipindi cha mwanzo mwanzo cha urais wake, Bw Putin alikuwa na hamu ya kujenga uhusiano na nchi za Magharibi, afisa wa zamani wa Kremlin aliambia BBC.

Wanadiplomasia wa Urusi walikuwa sehemu muhimu ya timu ya Bw Putin, wakisaidia kutatua mizozo ya eneo na China na Norway, wakiongoza mazungumzo ya ushirikiano wa kina na nchi za Ulaya, na kuhakikisha mabadiliko ya amani baada ya mapinduzi nchini Georgia.

Lakini kadri Bw Putin alivyozidi kuwa na nguvu na uzoefu, alizidi kusadiki kuwa alikuwa na majibu yote na kwamba wanadiplomasia hawakuwa wa lazima, anasema Alexander Gabuev, mkurugenzi wa Kituo cha Carnegie Russia Eurasia, ambaye anaishi uhamishoni Berlin.

Ishara ya kwanza kwamba Vita Baridi vinaanza ilikuja mnamo 2007 kupitia hotuba ambayo Bw Putin aliitoa kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich.

Obama

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Ben Rhodes (kushoto), mshauri msaidizi wa zamani wa rais Obama wa masuala ya Usalama anasema Putin ameendela kupuuza wizara yake ya mambo ya nje.

Katika hotuba hiyo ya dakika 30, alishutumu nchi za Magharibi kwa kujaribu kujenga ulimwengu wenye muelekeo mmoja. Wanadiplomasia wa Urusi walifuata mwongozo wake. Mwaka mmoja baadaye, wakati Urusi ilipoivamia Georgia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Moscow, Sergei Lavrov, aliripotiwa akiapa mbele ya mwenzake wa Uingereza, David Miliband, akimuhoji: "Wewe ni nani wa kunifundisha?

Lakini hivi karibuni ikawa dhahiri kwa maafisa wa Marekani kwamba wenzao wa Urusi walikuwa wakifuata maoni ya Bw Putin yanayoongezeka dhidi ya Magharibi, anasema Ben Rhodes, naibu mshauri wa usalama wa taifa wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.

Bw Rhodes anamkumbuka Rais Obama akipata kifungua kinywa na Bw Putin mwaka wa 2009, akiandamana na timu yake. Anasema Bw Putin alipenda zaidi kuwasilisha maoni yake kuhusu ulimwengu kuliko kujadili ushirikiano na kwamba kiongozi huyo wa Urusi alimlaumu mtangulizi wa Bw Obama, George W Bush, kwa kuisaliti Urusi.

"Katika masuala fulani fula- hasa kuhusu Ukraine - sikuelewa kwamba [wanadiplomasia] walikuwa na ushawishi wowote," anasema Bw Rhodes.

Obama

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Putin akizungumza na Obama mwaka 2009, alionekana kueleza zaidi maoni yake kuliko mazungumzo ya kushirikiana

Andrei Kelin, balozi wa Moscow nchini Uingereza, anapinga maoni kwamba wanadiplomasia wa Urusi wamepoteza ushawishi wao. Amefanya kazi katika uhusiano na nchi za Magharibi katika maisha yake yote ya kidiplomasia.

Katika mahojiano na BBC, alikataa kukiri kwamba ama Moscow au wanadiplomasia binafsi watawajibika kwa kuporomoka kwa uhusiano na nchi za Magharibi.

"Sisi sio tunaharibu," alisema. "Tuna matatizo na utawala wa Kyiv. Hakuna tunachoweza kufanya kuhusu hilo."

Anasema vita nchini Ukraine ni "mwendelezo wa diplomasia kwa njia nyingine".

Boris Bondarev

Chanzo cha picha, Boris Bondarev

Maelezo ya picha, Boris Bondarev

Urusi inaonekana kutegemea zaidi mifumo yake ya kijeshi, huduma za kijasusi na uwezo wa kiuchumi wa kijiografia kufanya ushawishi - badala ya diplomasia.

Katika mazingira haya ya kukatisha tamaa, kwa nini wanadiplomasia wa Urusi hawapigi kura kwa miguu yao na kujiuzulu kabisa kutoka kwa utumishi wa kigeni?

"Ni tatizo kwa kila mtu ambaye amekaa katika nyadhifa zao kwa miaka 10 hadi 20," mfanyakazi wa zamani wa Kremlin aliambia BBC. "Hakuna maisha mengine kwako. Yanatisha."

Bw Bondarev, mwanadiplomasia wa zamani, anaweza kuhusishwa na hilo. "Kama isingekuwa vita, labda ningebaki na kuvumilia," anasema.

"Kazi sio mbaya sana. Unakaa, unateseka kidogo na jioni unatoka."