Je ni kweli mawe haya yanaweza kuwasha taa?

Reality Check

Rocks

Chanzo cha picha, video

Video zinazosemekana kuonyesha kwamba mawe ama miamba inayopatikana Afrika inaweza kuzalisha umeme imetazamwa mara milioni mtandaoni. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanadai kuwa mawe ama miamba hiyo inaweza kuwa jibu la matatizo ya nishati barani humo.

Hilo ni dai kubwa, kwa hivyo tumeonyesha video kwa wataalamu ambao wametufafanulia kwa nini sifa kama hizo haziwezekani sana.

Video iliyosambaa sana

Ilikuwa moja ya video zilizosambaa sana ikionyesha cheche za umeme zikiruka kati ya mawe mawili yalipogusanishwa.

rocks

Chanzo cha picha, video

Maelezo ya picha, Taa inawaka, lakini kwanini?

Ilisambazwa sana na miongoni mwa walioisambaza, ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Daniel Marven, ambaye ana wafuasi zaidi ya 800,000.

Tweet yake sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni mbili. Mtumiaji mwingine wa Twitter alitoa maoni kuhusu chapisho la Bw Marven na video tofauti ikimuonyesha mtu anayewasha taa (balbu) aina ya LED kwa kugusanisha waya zinazoiunganishwa na kipande kidogo cha mwamba au jiwe.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Marven pia alichapisha video hii saa chache baadaye, na kupata maoni zaidi ya milioni. Video zote mbili zilichukuliwa na kutumika katika kurasa maarufu ya Twitter, African Archives. Hii ilienea sana, na maoni zaidi ya milioni 35. Je, video zimerekodiwa wapi?

Video hizi zimerekodiwa wapi?

Katika video inayoonyesha akiwasha taa ya umeme akionekana kutumia mawe, sauti inaweza kusikika ikizungumza kwa Kiswahili kwa lafudhi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa video ya mawe hayo mawili yanayowasha taa, inaonyesha kuwa hii ilionekana hapo awali kwenye ukurasa wa Facebook wa Chuo Kikuu cha Mohamed First, huko Oujda, Morocco mnamo Novemba mwaka jana - ingawa video yenyewe inaweza kuwa ilipakiwa mapema.

Maelezo yanasema tu: "Lithium!!?" lakini bila maelezo zaidi. BBC imewasiliana na chuo kikuu hicho lakini bado haijapata jibu. Chapisho moja lililofuata la Twitter linadai miamba hii ya kuto cheche ilipatikana nchini Zimbabwe, ikisema ugunduzi huu "ungesaidia nchi yetu kuwa na...nishati endelevu."

Zimbabwe ni mzalishaji mkubwa zaidi barani Afrika wa lithiamu, madini yanayotumika sana katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme na vifaa vya simu.

Je, umeme unaweza kuzalishwa kutoka kwa mawe?

"Nina shaka sana kwamba video hizi zinaonyesha nishati ya umeme wa bure," anasema Prof Stuart Haszeldine wa Shule ya Sayansi ya Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.

"Sijawahi kuona chochote kijiolojia kitu kama hiki kwamba mwe yameunganishwa kwenye vyanzo vya nguvu vya umeme ambavyo havijajumuishwa kwenye picha za video zilizowekwa vizuri."

Anasema kuwapo kwa kile kinachoonekana kama mkono uliovaa glavu katika sehemu ya chini ya video inayoonyesha mashaka.

Rocks

Chanzo cha picha, Video

Maelezo ya picha, Mkono uliovaa glovu ukionekana katika video hii

Hii inaonyesha kwamba "nguvu ya umeme inatiririka kutoka kweye mawe yaliyoshikiliwa kwa glavu (ili kujikinga na mkondo wa umeme)". Akirejea video inayoonyesha taa ya LED ikiwaka, Prof Haszeldine anasema inatia shaka "kwa sababu kuna mikono mitatu (watu wawili)".

"Inaonekana kwangu kwamba kuna udanganyifu". Picha ya mnapo iliyopigwa kutoka kwenye kwenye video inaonyesha kwamba wakati taa inasalia kuwaka ingawa waya mmoja umetenganishwa na jiwe, jambo linaloonyesha kuwa mwamba huo hauhusiani na saketi ama kuwaka kwa taa hiyo.

Rocks

Chanzo cha picha, Video

Nguvu halisi iliyoko nyuma juu ya madini ya Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina utajiri wa madini ya thamani, ikiwa ni pamoja na coltan (columbite-tantalite). Inaposafishwa, coltan hutoa tantalum ya metali, poda inayostahimili joto ambayo inaweza kushikilia kiwango cha juu cha umeme, hiyo ni kwa ujibu na Dk Munira Raji wa Chuo Kikuu cha Plymouth nchini Uingereza.

Rasilimali hizi hufanya kuwa muhimu sana katika utengenezaji wa vifaa vinavyotumiwa katika simu za mkononi, kompyuta mpakato na vifaa vingine vya elektroniki.

Dk Raji anasema haiwezekani kuthibitisha kama mawe yoyote yanayoonyeshwa kwenye video ni coltan bila ya kuyafanyia majaribio katika maabara ya jiolojia, lakini hata kama yalifanyika, hayawezi kuzalisha umeme yenyewe. Kwa maana hiyo, anasema, madai kwamba miamba hii inaweza kuzalisha umeme ni uongo.

Rocks

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hapa inaonekana taa inawaka wakati waya ukiwa haujaunganishwa na jiwe

Dkt Ikenna Okonkwo, mhadhiri wa jiolojia katika Chuo Kikuu cha Nigeria, pia ameangalia video kutupa tathmini. Anasema mawe hayo yanayoonekana kama madini ya zinki au madini ya risasi.

Na madini haya, anasema, hakika hayana uwezo wa kuwasha taa (balbu). "Labda [wangeweza kushikilia]." Video hizo, anasema Dk Okonkwo, zinaonekana kuwa "ujanja fulani".