Je Facebook na Twitter zinakabiliwa na tisho la uwepo wake?

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Facebook na Twitter zimekuwa zikiwafuta kazi wafanyakazi wake katika kipindi cha wiki chache zilizopita

Labda kama umekuwa ukiishi maeneo yasiyo na umeme, lakini vinginevyo bila shaka katika kipindi cha wiki chache zilizopita, ulipata habari kuhusu mtikisiko mkubwa uliyoyapata makampuni makubwa zaidi ya teknolojia duniani.

 Mwezi uliopita ilibainika kuwa baadhi ya makampuni makubwa zaidi ya teknolojia ya mawasiliano - Apple, Netflix, Amazon, Microsoft, Meta (wamiliki wa Facebook) na Alphabet (wamiliki wa Google) -walikapiliwa na pigo kubwa la hasara ya zaidi ya dola trilioni 3 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita katika soko la hisa la Marekani.

 Katika mwezi wa Novemba baadhi yao , ikiwemo kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni e-commerce - Amazon, ilitangaza kupunguza kazi kote duniani kwa idadi ya kazi 136,000 kufikia tarehe 21 Novemba, kulingana na wavuti wa Layoffs.fyi website, unaofuatilia kupunguzwa kwa kazi katika makampuni ya teknolojia.

 Baadhi ya waliopunguza idadi kubwa za wafanyakazi wake ni kampuni ya Facebook kamouni mama ya Meta, ambayo iliwafuta kazi wafanyakazi 11,000 na Twitter,ambayo imewaondoa kazini watu 3,700 hadi sasa (kiasi hicho ni nusu ya nguvu kazi yake yote).

Hii imeibua maswali kuhusu hali ya baadaye ya majukwaa ya makampuni hayo maarufu zaidi ya mitandao ya kijamii duniani: je tumechukulia uthabiti wa makampuni haya makubwa kama jambo la kawaida?

Ni kiasi gani cha matatizo Facebook na Twitter waliyomo?

Kama idadi ilivyonukuliwa hapo juu, majukwaa haya yanakabiliwa na kushuka kwa uchumiwa dunia sawa na sekta nyingine.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Facebook, inayomilikiwa na Zuckerberg, ilipoteza wafuasi kwa mara ya kwanza mwaka huu katika historia yake ya miaka 18

Hiyo inamaanisha kwamba ni kiasi kidogo cha pesa kinachoingizwa katika biashara – mapato ya muhimu ya matangazo ya biashara katika majukwaa ya mtandao huu wa kijamii yamepungua.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 "Yeyote anayejaribu kupata pesa katika teknolojia kwa sasa atabaini kuwa ni vigumu sana," anasema Professor Jonathan Knee, mtaalamu wa teknolojia ya habari katika Chuo kikuu cha biashara cha Colombia cha New York's Columbia , anasema.

Prof Knee sanasema kwamba majukwaa ya mitandao ya habari ya kijamii "kimsingi yamekuwa ya kutangaza matangazo ya biashara".

"Wakati unapotegemea katika aina hizo za mapato, mdororo wa uchumi utayafanya mazingira kuwa magumu kwako ," anasema.

Ripoti ya fedha ya mwaka huu ya kampuni ya Meta, iliyotolewa mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, ilitaja kupungua kwa mapato ya matangazo ya biashara kama sehemu ya matatizo yanayoikumba kampuni hiyo, lakini pia ilielezea kuongezeka kwa ushindani kutoka kwa majukwaa hasimu kama TikTok.

 Twitter, ambayo imeondolewa kwenye soko la hisa baada ya kununuliwa na bilionea Elon Musk, pia imeathiriwa pakubwa na huenda ikakabiliwa na changamoto zinazohusiana na mtindo wa uongozi wa Musk wa kuchukua maambuzi tata.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matatizo ya Twitter yalianza kabla ya kuwasili kwa mmiliki mpya

Lakini ishara za tahadhari zilikuwepo hata kabla ya kuwasili kwa Musk: nyaraka za ndani ya kampuni hiyo ambazo shirika la habari la Reuters zilizipata mwezi Oktoba zilionyesha kuwa "watumiaji wakuu wa Twitte " – baadhi yao ambao huingia mara sita au mara saba kwa wiki na kutuma jumbe matra tatu au mara nne kwa wiki – walikuwa wamepungua sana tangu mwanzoni mwa janga la Covid-19 pandemic.

 Kuwasili kwa Musk , hata hivyo, kunaonekana kusababisha tatizo jingine : utafiti uliochapishwa tarehe 3 Novemba , wiki moja tu baada ya kuchukua umiliki wa kampuni hiyo , tathmini ya watafiti kutoka taasisi ya teknolojia ya Massachusetts (MIT) ilikadiria kwamba Twitter ilikuwa imepoteza watumiaji milioni kwa kipindi hicho.

 Mizunguko wa maisha

Lakini je mzozo huu ni kile tu baadhi ya watalaamu wanachokiona kama mwisho wa mzonguko wa maisha wa kawaida wa kampuni ya mtandao wa kijamii?

"kila jukwaa lina matarajio yake ya ukuaji na kukua/ kushuka . Kushuka kwa kiasi kikubwa kutokana na majukwaa mapya yanayochukua nafasi yake ," Dkt Natalie Pang, mtaalamu wa mawasiliano na vyombo vipya vya habari katika chuo kikuu cha Singapore, anasema.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Je tumechukulia muda mrefu wa mitandao ya kijamii kama jambo la kawaida?

Dr Natalie pang anasema:"Wakati wa janga majukwaa ya teknolojia yalikua haraka kwasababu ya digitali ilikuwa muhimu katika kuwawezesha watu kuwasiliana wakati huo."

Sasa, anasema, ni muda wa kubadilisha utendaji wake.

Mtaalamu mwingine anayeona dalili za kuanguka kwa Facebook na Twitter na Dkt Lianrui Jia, mtaalamu wa habari za kidigitali katika chuo kikuu cha Sheffield, nchini Uingereza.

"Huenda tulichukulia kudumu kwa majukwaa hayo kama jambo la kawaida," anasema Dkt Jia.

"Watumiaji wanaweza kuanza kutambua baadhi ya matatizo kwa kuondoka kwa baadhi ya majukwaa haya."

 Makampuni haya makubwa yanaweza kutegemea misingi yake, hatahivyo: Facebook ilikuwa na watumiaji halisi bilioni moja kwa mwezi kufikia robo ya mwaka wa 2022, kulingaa na Meta, jambo ambalo linaifanya kuwa jukwaa la mtando wa kijamii maarufu zaidi duniani.

Lakini Februari, Meta ilitangaza kwamba jukwaa hilo lilipoteza watumiaji kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 18, jambo lililopelekea kuporomoka kwa hisa zake.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kupanda kwa umaarufu wa Tik Tok kuliongeza ushindani kwa majukwaa ya zamani

Renaud Foucard, Mhadhiri wa ngazi ya juu wa masuala ya Uchumi katika Chuo kikuu cha Lancaster , nchini Uingereza anasema kuwa kuongezeka kwa sheria za udhibiti za serikali mbali mbali pia kumekuwa kikwazo kwa makampuni ya teknolojia kwasababu imesababisha ushindani kwa watumiaji kuwa mkali zaid.i

 "katika miaka ya hivi karibuni, Marekani na Umoja wa Ulaya kwa pamoja wameweka sheria ambazo zimeyafanya makampuni ya teknolojia kupata ugumu kuyanunua makampuni hasimu, kama Facebook ilivyofanya kwa Instagram na WhatsApp awali ," Foucard anasema.

"Makampuni zaidi sasa yanashindania watumiaji na mapato."

Kusahaulika

Majukwaa wakati mwingine hutoweka au kufifia na kuwa yasiyokuwa ya maana.

Moja ya kisa maarufu zaidi ni cha MySpace.com: mtandao mkubwa wa kwanza wa kijamii kuwafikia watu kote duniani katika miaka ya 2000, ulikuwa na watumiaji milioni 300 katika mwaka 2007.

 Lakini ilipoteza umaarufu kwa kushindana na Facebook na sasa umebakia kama mchanganyiko wa watumiaji wa mtandao na huduma ya muziki wa moja kwa moja, ukiwa na watumiaji elfu sita tu duniani.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, MySpace ni mfano wa kupanda na kuanguka kwa mtandao mkubwa wa kijamii

Ushindani

Iwe hii ni kuruka tuta katika barabara ya Facebook na Twitter au iwe ni mwisho wake, baadhi wanaamini kuwa kukabiliwa na matatizo kwa majukwaa marufu ni dalili nzuri.

 "Ni jambo zuri kwamba sababu moja ya makujukwaa haya kuwa mashakani ni kwasababu ya ongezeko la ushindani ," anasema Renaud Foucard.

 "Ni soko lisilo na upendeleo, makampuni mapya yanaweza kutoa chaguo kwa watumiaji na fursa zaidi za kutoa hutoa uzoefu bora kwao ."