Eneo ambalo lingejengwa jiji la Akon sasa ni malisho ya mbuzi

Chanzo cha picha, DAVE SIMPSON
Mwimbaji wa RnB Akon anasema mipango yake iliyocheleweshwa sana ya Jiji la Akon - jiji la Afrika kwenye pwani ya Senegal - "inasonga mbele kwa asilimia 100,000.
Ingawa mbuzi kwa sasa wanapata malisho eneo hilo, anasema kuwa wakosoaji wataonekana "wajinga sana" siku zijazo.
Katika mahojiano ya kipekee na BBC, mwimbaji hiyo wa wimbo wa Smack That pia aliwahakikishia mashabiki wanaosubiri kurejeshewa pesa kutoka kwa kampeni yake ya Token of Appreciation cryptocurrency kwamba watarejeshewa pesa zao, hata kama atalazimika kuzilipa kutoka mfukoni mwake.
Akon, ambaye alizaliwa Marekani lakini kwa kiasi fulani alilelewa nchini Senegal, alitangaza miradi miwili mikubwa mwaka 2018 ambayo ilipaswa kuwakilisha mustakabali wa jamii ya Kiafrika.
Jiji la kwanza l lililoripotiwa kuwa na thamani ya dola bilioni 6 lenye minara mirefu . Ilikuwa iambatane na mpango wa pili - sarafu mpya ya cryptocurrency inayoitwa Akoin.
Lakini miaka kadhaa baadayemiradi yote miwili imekabiliwa na matatizo na ucheleweshaji na eneo ambalo jiji linapendekezwa kujengwa linabaki wazi

Chanzo cha picha, 10 DESIGN ARCHITECTURE
Siku moja mnamo Septemba 2020, Akon, akiwa amevalia suti ya bluu, alitembea kwa ujasiri kwenye ardhi ya udongo mwekundu yenye vumbi isiyotumika. Kulikuwa na kundi la wanahabari kutoka kote ulimwenguni ambao walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya uzinduzi wa hivi punde zaidi wa msanii huyo ambao ni jiji kuu lililojaa usanifu wa kuvutia.
Watu wa eneo hilo walipiga makofi huku pazia likivutwa nyuma kwenye ubao wa kuashiria eneo la jengo la siku za usoni. Lakini miaka baadaye swali iwapo mipango hiyo itatimia linagawanya jamii katika eneo hilo.
"Tulifikiri tunaweza kulifanyia kazi lakini kwa kasi hii, labda watoto wetu watafanya hivyo," mkazi mmoja wa eneo hilo aliambia BBC. "Tunasalia na matumaini kwa mradi huo. Tunatumai kuwa watoto wetu watabakia hapa kufanya kazi."
Mkazi mwingine anasema hawaamini tena katika mradi huo kabla ya kuongeza "ikifika, ikitukuta hapa, tutaona jinsi ya kuchangia".
Hapo awali Akon City ililinganishwa kwenye vyombo vya habari na Wakanda, jiji kuu la ajabu la Kiafrika linaloonyeshwa kwenye filamu za Black Panther na vitabu vya katuni. Awamu ya kwanza ya jiji yenye barabara, chuo kikuu, maduka, makazi, hoteli, kituo cha polisi, shule, kituo cha taka na mtambo wa umeme wa jua ilipaswa kukamilika mwishoni mwa 2023. Lakini baada ya kuchelewa mara nyingi, mambo machache yanaonekana kubadilika tangu sherehe ya uzinduzi.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Siku moja mnamo Septemba 2020, Akon, akiwa amevalia suti ya bluu, alitembea kwa ujasiri kwenye ardhiya udongo mwekundu yenye vumbi isiyotumika. Kulikuwa na kundi la wanahabari kutoka kote ulimwenguni ambao walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya uzinduzi wa hivi punde zaidi wa msanii huyo ambao ni jiji kuu lililojaa usanifu wa kuvutia.
Watu wa eneo hilo walipiga makofi huku pazia likivutwa nyuma kwenye ubao wa kuashiria eneo la jengo la siku za usoni. Lakini miaka baadaye swali iwapo mipango hiyo itatimia linagawanya jamii katika eneo hilo.
"Tulifikiri tunaweza kulifanyia kazi lakini kwa kasi hii, labda watoto wetu watafanya hivyo," mkazi mmoja wa eneo hilo aliambia BBC. "Tunasalia na matumaini kwa mradi huo. Tunatumai kuwa watoto wetu watabakia hapa kufanya kazi."
Mkazi mwingine anasema hawaamini tena katika mradi huo kabla ya kuongeza "ikifika, ikitukuta hapa, tutaona jinsi ya kuchangia".
Hapo awali Akon City ililinganishwa kwenye vyombo vya habari na Wakanda, jiji kuu la ajabu la Kiafrika linaloonyeshwa kwenye filamu za Black Panther na vitabu vya katuni. Awamu ya kwanza ya jiji yenye barabara, chuo kikuu, maduka, makazi, hoteli, kituo cha polisi, shule, kituo cha taka na mtambo wa umeme wa jua ilipaswa kukamilika mwishoni mwa 2023. Lakini baada ya kuchelewa mara nyingi, mambo machache yanaonekana kubadilika tangu sherehe ya uzinduzi.

Chanzo cha picha, 10 DESIGN ARCHITECTURE
Lakini Akon bado anashikilia kuwa mipango yake kabambe bado itatimizwa.
Tunapokutana katikati mwa London, anakubali kwamba "ningepata vitu zaidi kabla ya kuitangaza."
Pia analaumu Covid, ambayo anasema ilimaanisha "kila kitu kingerudishwa nyuma miaka miwili".
Lakini, ulimwengu ulikuwa tayari katika janga hili wakati alifanya sherehe ya kutangaza jiji la Akon kwa vyombo vya habari vya kimataifa mnamo Agosti 2020.
"Ninapanga kustaafu katika jiji hilo," anasema kwa ujasiri. "Sipendi kutumia neno mfalme wa jiji. Lakini ndivyo itakavyokuwa."
"Tunajaribu kujenga jiji haraka iwezekanavyo," anasema, akiongeza kwamba ana ukodishaji wa ardhi kwa miaka 50 ijayo na kwamba mradi wake "umetiwa saini na rais wa sasa".
Bodi ya utalii ya serikali ya Senegal SAPCO hivi karibuni ilithibitisha kujitolea kwao kwa mradi huo.
"Tunaamini katika jiji la Akon na sote tunamuunga mkono Akon kwa hivyo jiji la Akon litakuwa hai," alisema Me Aliou Sow, Mkurugenzi Mtendaji wa SAPCO. "Itawavutia watalii na wawekezaji katika ukanda huu na SAPCO imejitolea kikamilifu katika kufanikisha mradi huu."
Akon anasema amebadilisha makampuni ya ujenzi na wasanifu anaofanya nao kazi katika mradi huo, akiongeza kuwa washirika wake wapya wanaelewa Afrika, ardhi na wana "uaminifu wa kweli duniani". Malengo yake kwa ujumla yanabaki kuwa makubwa.
"Tunataka majumba makubwa makubwa. Lengo langu ni kujaribu kujenga kitu ambacho watu wanaona hakiwezekani katika Afrika."
Tovuti kadhaa za watu mashuhuri za kifedha zinakadiria thamani ya Akon kuwa kati ya $60-80m, na kuchanga wengine kuhoji pesa zitatoka wapi kwa mradi wa ukubwa huu. Timu yake inadai wana mashirika ya kimataifa ambayo yatafadhili kwa uwekezaji binafsi.
Akon alisema kuwa kazi ya uchimbaji kwenye eneo hilo hatimaye itaanza kabla ya mwisho wa mwaka, akiongeza kuwa matangazo zaidi yatatolewa katika kituo cha vijana ambacho amejenga kwa wakazi katika kijiji eneo holo. Kazi ya ujenzi katika Jiji la Akon anasema "bado haijakaririwa kikamilifu".
Mipango ya awali ya Jiji la Akon, iliyoipa jina la "Crypto City" na mnamo Agosti 2020 Akon alisema miundombinu ya kifedha ya jiji hilo "itajengwa" kutokana na sarafu yake ya Akoin. Lakini sarafu hiyo imekuwa ikikumbwa na ucheleweshaji na changamoto zingine.
"Haikuwa ikisimamiwa ipasavyo," anakubali. "Ninachukua jukumu kamili kwa hilo."
Kabla ya kuzindua Akoin cryptocurrency, tovuti ya Akoin ilitangaza fursa ya kuuza, kampeni iliyoitwa Token of Appreciation (TOA).
Kampeni ilitangazwa zaidi ya miaka miwili kabla ya Akoin cryptocurrency yenyewe kupatikana. Ilikuwa ni uchangishaji ili kufidia gharama za kuzindua Sarafu ya Akoin baadaye.
Pesa zilizotumwa kwa TOAs ziliitajwa kama "mchango" kwenye ukurasa wa tovuti wa Akoin TOA lakini kulikuwa na motisha maalum ya kuweka pesa katika kipindi hiki. Wachangiaji waliambiwa kwamba kwa kila $1 watakayoweka wangepokea hadi TOA nne ambazo baadaye zingebadilishwa kuwa sarafu Akoin sahihi.
"Niliamini kwa dhati katika mfumo wa ikolojia ambao walikuwa wakitafuta kujenga," anasema Marcus (si jina lake halisi) anayeishi Uingereza. "Kila wakati ningeweka pauni elfu chache."
Kampeni ya Token of Appreciation ilikamilika mnamo Oktoba 2019. Akaunti rasmi Twitter ya Akoin ilidai kuchangisha $290,000. Zaidi ya miaka miwili baadaye wafadhili wa TOA walipewa chaguo katika kundi rasmi la Akoin kwenye mtandao Telegram.

Chanzo cha picha, 10 DESIGN ARCHITECTURE
"Sasa tunaweza kuwapa wamiliki wa TOA chaguo," aliandika msimamizi. "wapate kurejeshewa pesa za mchango wao wa awali au wapokee Akoin MasterCard ambayo itakuwa na thamani ya mchango wao wa awali."
Baadhi ya wafadhili wa TOA wameamua kusubiri zawadi zao walizoahidiwa. Kwa sasa wana taarifa ya Ishara ya Kushukuru lakini haina matokreo yoyote. Wengine wamejaribu kudai kurudishiwa pesa zao.
"Sikuomba kurejeshewa pesa, walinirudisha pesa," anabainisha Marcus, ambaye imani yake katika mradi huo ilikuwa inaanza kufifia. "Urejeshaji wa pesa ulikusudiwa kuja wiki chache baadaye. Sasa tuna zaidi ya mwaka mmoja. Na tumerejea katika hali ile ile na kila mtu analalamika."
Marcus hayuko peke yake. Katika vikundi vya Akoin Telegram nimezungumza na watu wengine kadhaa kote ulimwenguni ambao walisema kwamba wameomba kurejeshewa pesa zao lakini bado wanasubiri kurejeshewa pesa hizo.
"Inafadhaisha sana," anasema Reggie, Mmarekani anayeishi Asia ambaye pia alichangia kampeni hiyo. "Ndio, nimekuwa na hasira kuhusu hili, mara kadhaa."
Nililalamika kama za Marcus' na Reggie kwa Akon, ambaye alikana kujua kwamba wafadhili wa kampeni ya Akoin walikuwa bado wanasubiri kurejeshewa pesa. Anadai atashiriki katika kurekebisha hali hiyo hadi wafadhili wa TOA watakapofurahi.
"Hata kama nitaingia mfukoni mwangu,". Nitfanya ziara ya dunia ili tu kuwalipa wote."

Chanzo cha picha, SEMER INVESTMENT
Sarafu ya Akoin yenyewe ilizinduliwa kwenye Bitmart mnamo Septemba 2021. Thamani yake wakati huo ilikuwa $0.28 lakini imeshuka kwa kiasi kikubwa tangua kuporomoka kw soko la cryptocurrency. Leo bei ya Akoin ni £0.01 tu.
Pia kumekuwa na maswali kuhusu kama itakuwa halali kwa Akoin kufanya kazi kama njia ya msingi ya malipo katika Jiji la Akon .
Sarafu ya sasa nchini Senegal ni faranga ya CFA, ambayo inadhibitiwa na kutolewa na Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO), ambayo hugawana pesa hizo. Yahoo Finance iliripoti mwaka jana kwamba "taasisi hiyo ilionya juu ya hatari ya kutumia cryptocurrency na kuiita kuwa ni haramu". Tuliwasiliana na BCEAO ili kutoa maoni kuhusu uhalali wa jiji linalotumia cryptocurrency lakini hawakujibu.
"Hayo ni mashaka mengi hata mimi ninayo," anakubali Akon. "Ninataka kuhakikisha kwamba kwa njia yoyote tunahusisha na crypto ndani ya jiji ni kwa njia ambayo inaambatana na sheria na kanuni zote."
Kwa hivyo, je, shughuli za kawaida katika "Jiji la Crypto " iliyopendekezwa na Akon bado zitafanyika na crypto yake mwenyewe? Inaonekana haijulikani. "Tutaelewa wakati jiji litakapomalizika, hiyo ni hakika," anaahidi.
Lakini baada ya miaka miwili ya kusubiri, si kila mtu ana hakika.
"Nadhani wengi wetu tumefanya utafiti wetu lakini iliibuka kana kwamba hakuna kinachoendelea," anasema Reggie. "Ningependa kurudishiwa pesa zangu na niondoke".












