'Watu hutaka kufanya ngono nami kama njia ya kunionyesha ukarimu kwa sababu mimi ni mlemavu'
Gemma Dunstan
BBC Wales Live

Chanzo cha picha, BBC NEWS
Holly alikuwa na umri wa miaka 16 tu mtu mmoja alipomuuliza ikiwa angeweza kufanya ngono naye kwa sababu alikuwa mlemavu.
Ameulizwa maswali mengine mengi kwa miaka mingi, kama vile "anaweza kufanya ngono kwa nguvu" au ikiwa inahitajika kuwa kwenye kiti cha magurudumu akifanya ngono.
"Watu wanadhani wanakufanyia ukarimu, au hata wamejitoa mhanga kukusaidia. Jambo baya zaidi sishangai wala siudhiki tena siku hizi ninapokumbana na maswali kama hayo."
Holly, ambaye sasa ana umri wa miaka 26, ana maumivu ya muda mrefu na ugonjwa wa hypermobility na ni mmoja wa wanawake walemavu ambao wamezungumza kupinga mawazo mabaya na unyanyapaa linapokuja suala la uchumba na mahusiano.
Holly Greader alisema ni muhimu kwamba mahusiano ya furaha kwa wale ambao walikuwa walemavu yanawakilishwa.
Alianza kuchumbiana na mume wake wa sasa James alipokuwa kijana, na amekuwa naye kwa miaka tisa, na kufunga ndoa mapema mwaka huu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Mara nyingi katika vyombo vya habari walemavu wana maisha duni, sisi ni hadithi ya kusikitisha," alisema.
Aliongeza kuwa amekuwa akihisi kuungwa mkono naye kila wakati, lakini alihisi ubaguzi na wengine.
"Niliambiwa na watu tulipoanza kuishi pamoja mara ya kwanza, kwamba ikiwa afya yangu itadorora ataniacha.
"Kwa kuwa mzigo au kuhitaji kushughulikiwa'.
Alisema kulikuwa na mawazo ambayo watu walikuwa nayo shuleni, ambayo wengine walimuuliza hadharani.
"Inapokuja kwa watumiaji wa viti vya magurudumu, daima bila shaka ni karibu swali la kwanza, mtu huyo anaweza kufanya ngono?"
Alisema wavulana katika darasa lake shuleni wangeuliza maswali ya kibinafsi na ya kumuudhi.
"Niliulizwa kama, unaweza tu kufanya mapenzi kwenye kiti cha magurudumu? Je, viungo vyako vitatengana? Ikiwa ningetaka kufanya ngono kwa 'nguvu' na wewe, itawezekana pia?"
Holly alisema watu pia wamemtumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ngono, ofa ambayo mara nyingi alipewa na kutoa taswira kana kwamba alipaswa kujiona mwenye bahati'
Holly angependa kuona uwakilishi mzuri zaidi katika vyombo vya habari, akitaja kwamba mhusika Isaac Goodwin katika kipindi cha 'Sex Education' ndiye mfano pekee mzuri ambao amekuwa akifahamu hivi karibuni.

Chanzo cha picha, RAM Photography & Film
Nicola Thomas, 38, kutoka Caerphilly ana ulemavu wa kuona.
Alisema: "Moja ya mambo ya kawaida ambayo watu watauliza ni, unafanyaje ngono? inakushangaza , ni swali la kibinafsi sana'
Nicola ana ugonjwa wa kinga mwilini - Neuromyelitis Optica - alipoteza uwezo wa kuona katika jicho moja miaka 15 iliyopita na jingine miaka mitano iliyopita.
"Watu wengi huona vizuizi vilivyo na upofu na hakika mimi ndiye wa kuvivunja."
Shughuli anazofanya kujivinjari Nicola ni pamoja na kusafiri,kusafiri kwa mashua majini na safari yake inayofuata ni kwenda Hong Kong.

Chanzo cha picha, Nicola Thomas
Nicola alikuwa na mpenzi alipopoteza uwezo wa kuona lakini uhusiano huo ulivunjika.
"Nilichukuliwa kama mzigo, watu wangesema huwezi kuwa mlezi wake, lakini sikuhitaji mlezi."
Sasa ana mpenzi ambaye pia hana uwezo wa kuona
"Ingawa sisi sote ni vipofu, tutazunguka jiji, au kwenda kwa shughuli zetu peke yetu. Hakuna kinachotuzuia."
Nicola pia alisema anahisi ubaguzi watu wanapoonyesha kupendezwa naye.
"Watu hutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wakiuliza twende mkahawani kama safari ya kuanza uchumba, umakini wao hubadilika au mambo kubadiliska kabisa ninapowaambia mimi ni kipofu."
"Hakika unatendewa kama wanakufanyia ukarimu. Inakuweka mbali mara moja."
Nicola aliongeza: "Watu wanatubagua. Nataka kuvunja dhana hiyo, nina maisha kamili na yenye furaha."

Kat Watkins alisema walemavu wana haki ya kuchunguza utambulisho wao wa kijinsia na kuendeleza mahusiano kama mtu mwingine yeyote.
Yeye ndiye afisa wa mradi wa siasa wa Disability Wales.
"Kwa nini ngono na mahusiano ni mwiko kwa watu wenye ulemavu? Kuna mengi zaidi kwetu kuliko tu kuwa na uwezo wa kula na kuwa na paa juu ya vichwa vyetu."
"Kuishi maisha yako na kujifurahisha hiyo ni sehemu tu ya maisha, na haiangaziwI vya kutosha kwa watu wenye ulemavu."
Kat alisema mifano ya kusikia jinsi watu hutuma ujumbe kwa wanawake walemavu kama jabo la kawaida ni hatua ya kusikitisha.
Alisema vinyago vya ngono vinavyoweza kubadilika na vifaa vingine vya usaidizi vinaweza kusaidia kuwapa watu kujiamini na angependa kuviona kwenye tovuti na maduka makubwa zaidi ya ngono.
"Unapaswa kujistarehesha na kuelewa mwili wako, ili uweze kuwaambia wengine jinsi unavyofanya kazi. Kujipenda pia ni muhimu sana."












