Arshad Sharif:Tunayojua hadi sasa kuhusu mauaji ya mwanahabari maarufu wa Pakistan nchini Kenya

th

Chanzo cha picha, Javeria Siddique

Mwanahabari maarufu wa Pakistan, Bw Arshad Sharif, aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi Jumapili usiku katika hali isiyoeleweka.

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa Bw Sharif alikuwa akisafiri kurejea Nairobi kutoka Magadi akiwa na dereva wake alipokumbana na kifo kwenye kizuizi cha barabara cha polisi.

Habari za kifo chake zilitangazwa kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii na mkewe Javeria Siddique, na kusababisha kizaazaa huku watumiaji wa mtiandao wa Pakistan wakijaribu kufahamu kifo hali inayozingira kifo chake.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitoa rambirambi zake kwa familia ya mwandishi huyo.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Huku familia yake na watu wengi wanaofutilia tukio hilo wakitaka kujua kilichotokea usiku wa Jumapili tarehe 23 Oktoba,kuna maswali mengi kuliko majibu lakini haya ndio yanayofahamika hadi sasa kuhusu kifo cha mwanahabari huyo

Waliagizwa kusimamisha gari lao kwenye kizuizi

Katika usiku huo wa maafa, polisi wanadai kwamba mara baada ya kuingia katika barabara ya Kiserian-Magadi kutoka kwenye barabara ya vumbi, walitakiwa kusimama lakini wakakaidi. Kisha polisi walifyatua risasi.Hayo ni kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo vinavyodai kuiona taarifa ya polisi kuhusu tukio hilo

Polisi kuanza uchunguzi

Baada ya habari kuhusu kifo cha Sharif ,polisi nchini Kenya wamethibitisha kuanza uchunguzi kuhusu kifo chake .

Msemaji wa polisi Bruno Shioso anasema wanachunguza hali iliyosababisha kifo cha Bw Sharif.

IPOA pia yatangaza kuanza uchunguzi

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi nchini Kenya (Ipoa) inasema imeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanahabari mashuhuri wa Pakistani Arshad Sharif.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba kuuawa kwa Bw Sharif na polisi ni kisa cha utambulisho usio sahihi.

Ipoa, chombo cha kiraia, kiliundwa kufuatilia kazi ya polisi.

Mkuu wake, Ann Makori, amewaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Nairobi, kwamba timu maalum ya kutafuta majibu ya haraka imetumwa kuchunguza mauaji ya mwandishi huyo.

Kituo cha runinga cha Citizen kimechapisha kwenye ukurasa wa twitter video ya matamshi ya Bi Makori:

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 3

Kifo chake kimewashtua wengi hasa nchini mwake Pakistan

Mwanahabari huyo aliyeshinda tuzo alipinga vikali maendeleo ya kisiasa yanayoendelea nchini Pakistan. Sharif alibobea katika uandishi wa habari za uchunguzi na alishughulikia matukio mengi ya kisiasa nchini mwake kwa mashirika ya habari ya kitaifa na kimataifa.

Sharif, mkosoaji mkali wa serikali ya Pakistan, aliondoka nchini mapema mwaka huu baada ya msururu wa kesi za uchochezi kuwasilishwa dhidi yake.

Chama cha waandishi wa habari nchini Pakistan kinataka uchunguzi kuhusu kifo chake. Watu wengi nchini humo kupitia mitandao ya kijamii wameelezea kushangazwa na hali iliyosababisha kifo chake na kutaka uchunguzi kufanyika