Sudan: Kikosi cha kukabiliana na dharura RSF ni kikosi cha aina gani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa kikosi cha kukabiliana na dharura nchini Sudan

Kiliundwa mwaka wa 2013 kwa misingi ya wanamgambo wenye kuchukiza wa Janjaweed, ambao walipigana na waasi huko Darfur kwa mbinu za kishenzi.

Tangu wakati huo, Jenerali Dagalo ameunda kundi lenye nguvu la kijeshi ambalo limeshiriki katika migogoro ya Yemen na Libya na kudhibiti baadhi ya migodi ya dhahabu nchini Sudan.

Sababu kuu ya mzozo huo ni uhasama kati ya Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo (pichani) na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Wanachama wa kundi hilo pia wameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya Juni 2019 ya zaidi ya waandamanaji 120.

Kundi hilo lenye nguvu za kijeshi ambalo haliko chini ya jeshi ni tishio kwa utulivu wa nchi.

Jenerali Hamdan anahusishwa vipi na Urusi?

Kuanzia kama mfanyabiashara wa ngamia, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo amekusanya ushawishi na utajiri kwa kasi nchini Sudan katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, na kupanda hadi kufikia kilele cha mamlaka.

Jenerali Hamdan alikuwa kamanda wa wanamgambo wa Janjaweed, ambao wanatuhumiwa kwa uhalifu mkubwa wakati wa vita vya Darfur vilivyoanza mwaka 2003 na kusababisha vifo vya hadi watu 300,000. Mamilioni ya watu walilazimika kuacha nyumba zao.

Utendaji wa Hamdan katika jukumu hili ulivuta hisia za Rais Omar al-Bashir, ambaye alimteua mnamo 2013 kuongoza Kikosi kipya cha kukabiliana na dharura cha Janjaweed.

Hata hivyo, baada ya maandamano mwaka 2019 kumtaka al-Bashir ajiuzulu, Jenerali Hamdan alimgeuka kiongozi huyo wa zamani na kusaidia kumuondoa madarakani.

Mnamo 2019, Vikosi vya RSF vilikandamiza maandamano ya kidemokrasia nchini Sudan kudai serikali ya kiraia.

Kulingana na baadhi ya ripoti, wanapigana pia kama mamluki nchini Yemen kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.

Nchini Sudan, maslahi ya Hemeti ni katika uchimbaji wa dhahabu na ujenzi. Pia anahusika na siasa za kikanda na kuendeleza uhusiano na Urusi.

Mnamo Machi 2022, maafisa wa Sudan walisema walipanga kufanya upya makubaliano, yaliyositishwa mnamo 2020, ambayo Moscow ingepokea ukodishaji wa miaka 25 kwenye kambi ya jeshi la majini huko Port Sudan kwenye Bahari Nyekundu.

Wakati huo huo, Hamdan alisafiri hadi Moscow, ambapo alikutana na maafisa wa Urusi, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov na Nikolai Patrushev, katibu wa Baraza la Usalama la Urusi

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sababu kuu ya mzozo huo ni uhasama kati ya Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo (pichani) na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Shirika la habari la serikali ya Sudan SUNA kisha liliripoti kuwa pande hizo zilikubali kufanya upya mikataba yote ya awali ya kiuchumi, kidiplomasia na kiusalama.

Mwezi Machi mwaka huu, baada ya ziara ya Sergey Lavrov, utawala wa kijeshi nchini Sudan uliidhinisha ujenzi wa kituo cha jeshi la wanamaji la Urusi. Itawahifadhi wachezaji 300 na meli nneza kijeshi . Kwa kubadilishana, Moscow itaipatia Khartoum silaha na zana za kijeshi.

Mnamo Machi 16, kituo cha telegram Prigozhin's Press Service kilichapisha jibu kwa mwandishi wa New York Times, kwa njia yake ya kawaida, ambayo ilisema hasa: "Sisi ... hatuna chochote cha kufanya ... na Mheshimiwa Khamedti."

Kwa nini Sudan inaongozwa na jeshi?

Mapigano ya mwishoni mwa juma ni mzozo wa hivi punde zaidi nchini humo kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir mwaka wa 2019.

Al-Bashir alikuwa madarakani kwa takriban miongo mitatu. Baada ya maandamano makubwa ya mitaani ya kutaka aondolewe madarakani, wanajeshi walifanya mapinduzi na kuchukua uongozi wa nchi.

Kutokana na hatua hiyo, serikali ya pamoja ya kijeshi na kiraia iliundwa, lakini kutokana na mapinduzi mengine mnamo Oktoba 2021, serikali ilipinduliwa.

Tangu wakati huo, ushindani kati ya Jenerali Burkhan na Jenerali Dagalo umeongezeka.

Mnamo Desemba mwaka jana, mpango wa mfumo ulikubaliwa kuhamishia mamlaka kwa raia, lakini mazungumzo ambapo pande hizo mbili zingekubaliana juu ya undani wa mabadiliko haya yalishindikana.

.

Chanzo cha picha, Anadolu

Maelezo ya picha, Makubaliano ya mfumo wa uhamishaji madaraka, uliotiwa saini na wanajeshi na wawakilishi wa vyama vya kiraia, yalizua maandamano nchini humo hata kabla ya mazungumzo hayo kufikia mwisho

Nini kinaweza kutokea baadaye?

Ikiwa mapigano yataendelea, yanaweza kusambaratisha nchi hiyo Zaidi na kuzidisha hali ya sintofahamu ya kisiasa.

Wanadiplomasia hao ambao walichukua nafasi kubwa katika kujaribu kuwashawishi wananchi kurejea katika utawala wa kiraia, watakuwa wakijaribu kutafuta njia ya kuwafanya majenerali hao wawili kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Wakati huo huo, raia wa kawaida wa Sudan wanakabiliwa na kipindi kingine cha hofu