Tazama Rais Biden alivyoanguka kutoka kwa baiskeli baada ya safari ya Delaware

Rais wa Marekani Joe Biden mwishoni mwa alianguka kutoka kwa baiskeli yake alipokuwa akijaribu kusimama, baada ya safari karibu na nyumbani kwake ufukweni katika jimbo la Delaware nchini Marekani.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79 alisimama na kuanza kuzungumza na wananchi.

Alisema hakujeruhiwa , kulingana na Associated Press. Alisema mguu wake ulikuwa umenaswa kwenye kamba ya kanyagio.