Mwisho Wetu: Je! Ugonjwa wa fangasi unaweza kutugeuza sote kuwa mazombi?

By James Gallagher, BBC Radio 4

fungus

Chanzo cha picha, HBO/WARNER MEDIA/LIANE HENTSCHER

Acha nikufahamishe jambo la kutisha sana - kuna fangasi ambao husababisha wale walioathirika kugeuka mazombi. Huzalisha seli ambazo huingia ndani ya mwili. Kisha fangasi hao hukua na kuanza kuhodhi na kuteka akili ya kiumbe mwenye fangasi (mwenyeji wake).

Fangasi wa vimelea hula mwathirika wake kutoka ndani, na kunyonya kila kirutubisho cha mwisho, zinapojitayarisha kwa mwisho wake. Kisha - katika tukio la kutatanisha zaidi kuliko filamu ya kutisha zaidi - mwelekeo wa kifo hutokea kuanzia kwenye kichwa.

Mwili huu ulio na fangasi husambaza seli kwenye kila kitu kinachoizunguka - kuwaangamiza wengine kama inavyokuwa kwa mazombi. Inaonekana kama hadithi. Lakini ufalme wa fangasi - tofauti na mimea na wanyama - ni wa kipekee.

Aina za vimelea vya fangasi vya Cordyceps na Ophiocordyceps ni halisi. Ipo video game na tamthilia ya "The Last of Us" inayoonyesha nguvu ya mazombi, Lakini katika ulimwengu wa kweli, je, janga la Cordyceps - au linalosababishwa na fangasi mwingine - linaweza kutokea?

"Nadhani tunapuuza maambukizi ya fangasi kama kitu cha hatari kwetu," Dk Neil Stone, mtaalamu mkuu wa fangasi katika Hospitali ya Magonjwa ya Tropiki huko London, ananiambia.

"Tayari tumefanya hivyo kwa muda mrefu sana na hatuko tayari kabisa kukabiliana na janga la fangasi."

Mwishoni mwa Oktoba mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa orodha yake ya kwanza ya fangasi hatari kwa maisha. Kuna mpaka wanaobebwa na mende, lakini utafarijika kujua kuwa Zombifying-Cordyceps hawajajumuishwa. Kwa nini isiwe hivyo?

Fungus

Chanzo cha picha, Getty Images

Dk Charissa de Bekker, mwanabiolojia katika Chuo Kikuu cha Utrecht, amechunguza jinsi fangasi hutengeneza mchwa na anasema haoni kama hilo linaweza kutokea kwa watu.

"Joto la mwili wetu ni la juu sana kwa fangasi wengi kuweza kuishi vizuri na kukua. "Mfumo wao wa fahamu ni rahisi kuliko wetu, kwa hivyo ni rahisi kuvamia ubongo wa wadudu kuliko ubongo wetu, pia mifumo yao ya kinga ni tofauti sana na yetu."

Spishi nyingi za fangasi 'Cordyceps' zilizo na vimelea zimebadilika kwa mamilioni ya miaka , hivyo utaalam katika kuambukiza aina moja tu ya wadudu ina mashaka. Wengi hawaruki kutoka kwa wadudu mmoja hadi mwingine.

"Kwa fangasi huyu kuweza kuruka kutoka kwa wadudu kuja kwetu na kusababisha maambukizi ni hatua kubwa sana," anasema Dk de Bekker.

Dk Stone

Chanzo cha picha, JAMES GALLAGHER

Maelezo ya picha, Dk. Stone

Vitisho vinavyotokana na fangasi vimetupiliwa mbali kwa muda mrefu. "Watu hufikiria kama jambo dogo, la juujuu au lisilo muhimu," asema Dk Stone. Ni wachache tu kati ya mamilioni ya spishi za fangasi husababisha ugonjwa, lakini baadhi yao wanaweza kuwa na athari mbaya zaidi ya kuwasha mguu au ukucha ulioambukizwa. Fangasi huua karibu watu milioni 1.7 kwa mwaka - idadi hiyo ni takriban mara tatu ya malaria.

Je, tunapaswa kuwachukulia kwa uzito zaidi fangasi?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Maambukizi yatokanayo na fangasi yana utofauti na maambukizi ya bakteria au virusi. Fangasi inapotufanya tuwe wagonjwa, karibu kila mara huchukuliwa kutoka kwa mazingira badala ya kuenea kupitia kikohozi na kupiga chafya.

Sisi sote tunakabiliwa na matatizo ya fangasi ya mara kwa mara, lakini mara nyingi wanahitaji mfumo dhaifu wa kinga ili kukudhuru. Kwa vile dawa inatuweka hai zaidi - lakini wapo baadhi yetu wenye kinga dhaifu.

Dr Neil Stone kutoka maabara ya (HSL) London, Dk Stone anasema ugonjwa wa fangasi una utofauti kimaambukizi na Covid - kwa jinsi unavyoenea na aina ya watu unaoambukiza.

Anadhani tishio liko kwa sababu ya "kiwango cha fangasi katika mazingira... mabadiliko ya hali ya hewa, usafiri wa kimataifa, kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa na kupuuzwa kwao kwa kina katika suala la matibabu tuliyo nayo".

Fangasi huenda wasitugeuze sote kuwa mazombi, lakini wanaweza kusababisha matatizo mengi zaidi kuliko tunayodhani ya mguu wa Mwanamichezo.