Hili ndilo eneo lenye vifo vingi zaidi vya kigaidi' duniani

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeshi la Mali linajitahidi kupambana na waasi wa kiislamu katika eneo la Sahel
Muda wa kusoma: Dakika 5

Eneo la Sahel barani Afrika ndilo "kitovu cha ugaidi duniani" na sasa, kwa mara ya kwanza, linachangia "zaidi ya nusu ya vifo vyote vinavyohusiana na ugaidi", kulingana na Kielezo cha Kimataifa cha Ugaidi (GTI).

Ripoti yake mpya inasema kuwa katika eneo hili lenye ukame kusini mwa Jangwa la Sahara watu 3,885 kati ya jumla ya watu 7,555 duniani kote walikufa kutokana na ugaidi.

Ripoti ya GTI inaongeza kuwa wakati idadi ya kimataifa imepungua kutoka kilele cha vito 11,000 mnamo 2015 idadi ya vifo katika Sahel imeongezeka karibu mara kumi tangu 2019, kwani vikundi vya itikadi kali na waasi "vinaendelea kuelekeza umakini wao" kuelekea eneo hilo.

Kiwango hicho kimechapishwa na Taasisi ya Uchumi na Amani, taasisi ya fikra iliyojitolea kutafiti amani na migogoro duniani.

Inaufafanua ugaidi kama "kutishiwa au matumizi halisi ya nguvu haramu na vurugu zinazofanywa na mhusika asiye wa serikali kufikia lengo la kisiasa, kiuchumi, kidini, au kijamii kupitia uoga, shuruti, au vitisho".

Unaweza pia kusoma:

Sahel inaenea kutoka pwani ya magharibi ya Afrika kuelekea mashariki katika bara. Ufafanuzi wa GTI wa eneo hili unajumuisha sehemu za nchi 10: Burkina Faso, Mali, Niger, Cameroon, Guinea, Gambia, Senegal, Nigeria, Chad na Mauritania.

Sahel ina baadhi ya viwango vya juu zaidi vya idadi ya wawatu wanaozaliwa duniani, na karibu theluthi mbili ya idadi ya watu wanaoishi katika eneo hilo ni chini wenye umri wa chini ya miaka 25.

Tofauti na nchi za Magharibi ambako "ugaidi wa muhusika pekee unaongezeka", Sahel, imesjhuhudia upanuzi wa haraka wa vikundi vya wanamgambo wa jihadi, kulingana na ripoti hiyo.

Inasema mashambulizi mengi huko yalifanywa na mashirika mawili: kundi la Islamic State linaloshirikiana na Sahel na Jama'at Nusrat al-Islam wal Muslimeen (JNIM) - tawi la al-Qaeda.

"Wanajaribu kuweka amri mpya za kisheria," anaelezea Niagalé Bagayoko, mwenyekiti wa Mtandao wa Sekta ya Usalama Afrika. "Wanajaribu kusimamia haki hasa kwa kuzingatia Sharia."

Na katika mchakato huo, anasema "wanashindana" kwa ajili ya kupata ardhi na ushawishi.

h
Maelezo ya picha, Nchi za Sahel
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

IS-Sahel imeripotiwa kuongeza mara mbili ya eneo inalolidhibiti nchini Mali tangu mapinduzi ya nchi hiyo ya 2020 na 2021 husasan mashariki karibu na mipaka yake na Burkina Faso na Niger huku JNIM pia ikiendelea kupanua ufikiaji wake, kulingana na jopo la wataalam wa UN kuhusu Mali.

Ripoti ya GTI inabainisha kuwa makundi yote mawili yameajiri wapiganaji zaidi, ikiwa ni pamoja na askari watoto katika kesi ya IS.

"Katika baadhi ya matukio, watu hujipata wakiwa katika hali ya kutokuwa na chaguo wakati wanapoamua kujiunga na kundi la wanamgambo," anasema Beverly Ochieng, mchambuzi mkuu aliyebobea katika Francophone Africa at Control Risks, mshauri wa hatari za kijiografia. "Hizi ni jamii ambazo ziko hatarini sana."

Ripoti ya GTI inaeleza jinsi ukosefu wa uthabiti wa kisiasa na utawala dhaifu unavyounda mazingira bora kwa vikundi vya waasi kukua, ikiashiria mizozo kama "kichocheo kikuu cha ugaidi".

Sahel wakati mwingine inajulikana kama "ukanda wa mapinduzi" wa Afrika.

Tangu 2020 kumekuwa na mapinduzi sita yaliyofaulu katika kanda kama ilivyofafanuliwa na ripoti ya GTI: mara mbili nchini Mali, mara mbili Burkina Faso, mara moja nchini Guinea na moja nchini Niger. Nchi hizi sasa zote zinaendeshwa na wanajeshi.

"Sahelimeshuhudia kuvunjika kwa serikali," anasema Dk Folahanmi Aina, mtaalam wa eneo hilo katika Chuo Kikuu cha SOAS huko London.

"Imefahamika kwa viongozi wa kisiasa ambao hawajatanguliza kipaumbele kwa utawala unaozingatia watu na malalamiko ya ndani yameongezeka, na kusababisha vikundi vya kigaidi kujaribu kukabiliana na haya."

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kapteni wa Burkina Faso Ibrahim Traoré (kushoto) na Jenerali wa Niger Abdourahamane Tiani (kulia) walichukua mamlaka katika mapinduzi, na kuahidi kupambana na waasi.

Kulikuwa na dhana kwamba serikali za kiraia hazikuweza kukabiliana na vitisho vya usalama kutoka kwa makundi ya waasi, "lakini licha ya wanaharakati hao kuchukua hatamu, ukweli ni kwamba ukosefu wa usalama umezidi," anasema Dk Aina. "Watawala wa kijeshi hawajajiandaa kitaaluma kukabiliana na ugumu wa utawala."

Mnamo mwaka 2024, Burkina Faso "ilibaki kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na ugaidi kwa mwaka wa pili mfululizo" kulingana na GTI.

Katika kipindi cha miaka 14 tangu ripoti hiyo kuanza, ni nchi pekee iliyoongoza orodha hiyo ambayo si Iraq au Afghanistan.

Makundi ya wanajihadi yanaendeleza shughuli zao katika Sahel na shughuli mbalimbali haramu za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi na wizi wa ng'ombe, kulingana na ripoti ya GTI.

Kanda hiyo pia imekuwa njia kuu ya walanguzi wa dawa za kulevya wanaoleta kokeini kutoka Amerika Kusini hadi Ulaya, na ripoti inabainisha kuwa "usafirishaji wa dawa za kulevya ni mojawapo ya shughuli haramu zenye faida kubwa kifedha zinazohusishwa na ugaidi katika Sahel".

Inabainisha kuwa baadhi ya vikundi huepuka kujihusisha moja kwa moja na uhalifu uliopangwa, hata hivyo, vikipendelea "kupata pesa kwa kutoza kodi au kutoa usalama na ulinzi kwa malipo".

Inaendelea kueleza: "Mtindo huu sio tu unazalisha mapato lakini pia husaidia vikundi hivi kuunganishwa katika jumuiya za mitaa, kuimarisha ushawishi wao."

Vikundi vya waasi pia vinapigania udhibiti wa maliasili tajiri za Sahel. Niger ni nchi ya saba kwa uzalishaji wa uranium duniani, na migodi ya dhahabu isiyodhibitiwa inayopatikana katika eneo lote mara nyingi hutumiwa na mashirika kama ya IS-Sahel na JNIM.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchimbaji madini usiodhibitiwa wa rasilimali kama vile dhahabu katika Sahel umesaidia ukosefu wa usalama wa mafuta

Kufuatia wimbi la mapinduzi ya hivi majuzi, serikali za Sahel zimejitenga na washirika wa Magharibi, kama vile Ufaransa na Marekani, kuelekea Uchina na Urusi kwa msaada katika kukabiliana na wanamgambo.

"Kwa sasa tunaona kwamba Urusi inachukua udhibiti kupitia wanamgambo wa Urusi katika eneo linalojulikana kama Africa Corps [zamani Wagner]," anasema Bi Ochieng. "Kazi yao ni kutoa mafunzo na kusaidia majeshi ya ndani ili kuweza kukabiliana na uasi katika eneo hilo, lakini hadi sasa haijafanikiwa."

Kutokana na hali hiyo, ripoti ya GTI inaonya kwamba sasa kuna hatari ya kuongezeka zaidi kwa kile kinachoitwa "kitovu cha ugaidi" kwa nchi jirani.

Inasema kuwa hii inaweza kuwa tayari kutokea - Togo ilirekodi mashambulio 10 na vifo 52 mnamo 2024, idadi kubwa zaidi tangu ripoti hiyo kuanza kutolewa. Mashambulio haya yalijikita zaidi kwenye mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.

Bi Ochieng anakubaliana na tathmini hii, akisema kuwa "upanuzi wa vikundi vya wapiganaji katika eneo hilo katika nchi kama Benin au Togo au mataifa mengine ya pwani ya Afrika Magharibi unaonekana karibu".

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi