Mabaki ya Titan: Baadhi ya sehemu za nje za nyambizi iliyotoweka zapatikana

.

Chanzo cha picha, Triton Submarine

Mabaki ya nyambizi ya kitalii Titan yaliopatikana wakati wa utafutaji wa meli hiyo ni Pamoja nae neo lake la nje.

Mpiga mbizi mtalaamu David Mearns aliambia BBC rais wa klabu ya wagunduzi ambayo inahusishwa na jamii ya wapigaji mbizi na waokoaji inasema kwamba mabaki ni Pamoja na "fremu ya kutua na kifuniko cha nyuma kutoka kwa chini ya maji".

Walinzi wa pwani wa Marekani walithibitisha kuhusu mabaki ambayo yamepatikana katika eneo la utafutaji.

Mabaki hayo yalipatikana na roboti ya chini ya maji inayodhibitiwa na rimoti ROV karibu na mabaki ya meli ya Titanic.

Kikao cha walinzi hao wa pwani na wanahabari kinatarajiwa kufanyika mwendo was aa nne kamili siku ya Alhamisi.

Nyambizi hiyo ya Titan ilitoweka katika eneo la mashambani kaskazini mwa Atlatinci siku ya Jumapili ikiwa na oksijeni ya siku nne kwa abiria wake watano.

Baadhi ya wataalamu wamedai kwamba huenda nyambizi hiyo ilipasuka kutokana kufeli kwa mitambo. Nyambizi hiyo ndogo ilikuwa ikimilikiwa na kuendeshwa na kampuni ya kibinafsi OceanGate Expeditions.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo, Guillermo Söhnlein, aliiambia BBC kwamba anaamini kuwa huenda kulikuwa na "mlipuko wa mara moja" kwa nyambizi hiyo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

“Kama ndivyo ilivyokuwa, ndivyo ingekuwa hivyo siku nne zilizopita,” alisema.

Bw Söhnlein aliongeza kuwa "hofu yake kubwa" wakati wa msako ni kwamba Titan ilijitokeza baada ya mawasiliano kupotea - jambo ambalo alisema lingekuwa hatua ya kawaida.

"Tangu mwanzo siku zote nilifikiri kwamba labda ndivyo Stockton [Rush, nahodha wa nyambizi] angefanya," aliongeza. "Katika hali ambayo inakuwa viguku sana kupata nyambizi, kwa sababu meli ya juu haingejua ilikuwa inakuja na haingejua pa kuangalia."

Iwapo sehemu ndogo itapatikana chini ya bahari, itahitaji kufikiwa na vifaa maalum vya uokoaji na kisha kuletwa juu ya bahari uso katika operesheni ambayo inaweza kuchukua saa nyingi.

Mapema katika wiki, ndege za utafutaji za Kanada ziliripoti kusikia kelele za chini ya bahari. Bado haijulikani kelele hizi zilikuwa nini, na viongozi wameonya kuwa huenda hazikuwa na uhusiano na Titan.

Tangazo la Alhamisi kwamba mabaki yalipatikana hadi sasa ndio kidokezo pekee kinachoweza kugunduliwa na vifaa vya kutafuta chini yam aji au ROVs ambazo zimetumwa kwenye eneo hilo.

Moja ya ROVs, iliyotumwa kutoka meli ya Canada Horizon Arctic, ilifika kwenye sakafu ya bahari mapema Alhamisi asubuhi. Nyingine kadhaa zilitarajiwa kuwasili baadaye mchana.

Meli ya utafiti ya Ufaransa, Atalante, pia iliwasili katika eneo hilo Alhamisi asubuhi na kupeleka ROV yake, Walinzi wa Pwani wa Marekani walisema. Roboti hiyo ina uwezo wa kufikia kina chini ya ajali ya Titanic, ambayo iko karibu 12,500 ft (3,810m) chini ya bahari, na ina uzoefu wa kuchunguza Titanic.

Eneo la jumla la bahari inayosakwa ni takriban kilomita za mraba 26,000 (maili za mraba 10,000), mara mbili ya ukubwa wa jimbo la Connecticut la Marekani. Eneo hilo hukabiliwa na hali ya dhoruba na kutoonekana vizuri jambo ambalo hufanya shughuli za utafutaji kuwa ngumu zaidi, wataalam wanasema.