Uvamizi wa hoteli Somalia: Zaidi ya 20 wafariki katika shambulio la al-Shabab

Vikosi vya usalama

Chanzo cha picha, Reuters

Vikosi vya usalama vya Somalia vimesema vimewaokoa watu 106 waliokuwa wamekwama ndani ya hoteli iliyokuwa imevamiwa na wanamgambo usiku wa kuamkia leo.

Watu 21 wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo wa saa 30, wizara ya afya ilisema. Mapambano ya kukomboa hoteli yalimalizika ndani ya usiku mmoja, maafisa walisema.

Washambuliaji walitumia vilipuzi kuingia kwenye Hoteli ya Hayat ya Mogadishu kabla ya kudhibiti kwa nguvu.

Kundi la al-Shabab limejitangaza kuhusika na shambulio hilo.

"Ningependa kuwafahamisha Wasomali wote kwamba operesheni katika hoteli hiyo ilihitimishwa usiku wa manane," Kamanda wa polisi Abdi Hassan Mohammed Hijra aliwaambia waandishi wa habari katika taarifa fupi iliyofanyika karibu na eneo la shambulio hilo.

"Inashangaza kwamba watu wasio na hatia walipoteza maisha hapa... Vikosi vya usalama vilikuwa vikihusika katika kuwaokoa watu mmoja baada ya mwingine na kwa vikundi."

Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwani kuna uwezekano kwamba wanafamilia walikusanya miili ya jamaa kabla ya kuhesabiwa rasmi, Waziri wa Afya Ali Haji Adan alisema.

Aliongeza kuwa watu 117 walijeruhiwa, huku 15 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Hoteli hiyo imeharibiwa kwa kiasi kikubwa kufuatia mapigano makali kati ya wanamgambo hao na vikosi vya usalama katika muda wote wa Ijumaa usiku na Jumamosi, huku video zikionyesha milipuko na moshi ukifuka kwenye paa la jengo hilo.

"Imekuwa ya kutisha, ya kutisha sana kuishi jirani na milio ya risasi, milipuko. Ilikuwa ni moja ya mambo ya kutisha ambayo nimewahi kuona huko Mogadishu," Abdisalam Guled, naibu mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi la Somalia, aliiambia BBC. .

Local residents came past the site of the hotel to see the destruciton for themselves

Chanzo cha picha, Reuters

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Afisa wa polisi aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu yametumiwa kufikia hoteli hiyo Ijumaa jioni - yakilenga kizuizi chake cha mbele na lango.

Baada ya shambulio la awali, tovuti yenye uhusiano na al-Shabab ilisema kundi la wanamgambo walikuwa "wakiendesha risasi bila mpangilio" baada ya "kuingia kwa lazima" katika hoteli hiyo - inayoelezwa kuwa eneo maarufu kwa wafanyakazi wa serikali ya shirikisho kukutana.

Vikosi vya usalama vilitatizika kuingia kwenye orofa za juu za hoteli hiyo kwa saa nyingi kwa sababu watu wenye silaha, ambao walikuwa wameshikilia idadi isiyojulikana ya watu, waliripotiwa kufyatua kwa mabomu ngazi zinazohitajika ili kuingia. Washirika wa al-Qaeda, al-Shabab wamehusika katika mzozo wa muda mrefu na serikali ya shirikisho.

Kundi hilo linadhibiti sehemu kubwa ya kusini na kati mwa Somalia, lakini limeweza kuimarisha ushawishi wake katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali yenye makao yake makuu mjini Mogadishu.

Somalia

Chanzo cha picha, Reuters

Katika wiki za hivi karibuni, wapiganaji walio na uhusiano na kundi hilo pia wameshambulia walengwa kwenye mpaka wa Somalia na Ethiopia, jambo ambalo limezua wasiwasi kuhusu uwezekano wa mkakati mpya wa al-Shabab.

Shambulio hilo la Ijumaa ni la kwanza kufanywa na kundi hilo katika mji mkuu tangu Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, kuchaguliwa mwezi Mei.

Hoteli na mikahawa zimekuwa zikilengwa mara kwa mara, lakini Mogadishu ilishuhudia shambulio baya zaidi mnamo Oktoba 2017, wakati zaidi ya watu 500 waliuawa wakati lori lililojaa vilipuzi lilipolipuliwa kwenye moja ya makutano ya jiji hilo.

Hakuna kundi lililojitangaza kuhusika na shambulio hilo, ingawa waandishi wa habari wanasema dalili zote zinaonyesha kuwa al-Shabab ilihusika.

UCHAMBUZI

Kwa nini ilichukuwa muda mrefu kudhibiti usalama?

Hili ni swali ambalo limeibua maswali mengi ndani ya na nje ya Somalia.

Mchambuzi wa masuala ya usalama wa Somalia Ahmed Kaboole, ambaye, ameambia BBC Idhaa ya Kisomali kwamba kundi lililoshambulia hoteli hiyo huenda lilichunguza eneo hilo kwa muda kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo.

"Muda uliochukuliwa na majeshi ya serikali kukomesha uvamizi huo unaashiria kuwa kundi lililoingia kwenye hoteli hiyo lilikuwa limejipanga vyema na huenda kuna uwezekano tayari lilikuwa limemeingiza vilipuzi ndani ya jengo la hoteli kabla ya kuanza mashambulizi," alisema.

"Walikuwa wakifanya kazi na wakazi wa eneo hilo au watu wa ngazi za chini waliokuwa pale kwa sababu hawakuweza kupata mahali pa kujificha kutokana na milio ya risasi ya jeshi, ambayo sauti yake ilisikika mjini."

Aliongeza kuwa kulingana na eneo la hoteli hiyo, ilikuwa rahisi kwa watu wengi kuingia humo bila kupitia vizuizi vya usalama.

"Eneo la Hayat liko nje kidogo ya eneo la udhibiti wa uwanja wa ndege. Liko wazi kwa jiji zima. Ilikuwa rahisi kwa watu kuingia na kuifikia jengo hilo kwa miguu bila kupitia sehemu zilizo na vizuizi vya usalama."

Hoteli hiyo iliharibiwa vibaya baada ya vikosi vya usalama kukabilia vikali na wavamizi ho Ijumaa na Jumamosi usiku, huku picha zikionyesha moto na moshi ukifuka kwenye paa la hoteli hiyo.

“Makundi haya huwa yanatafuta mwanya wa kuvuruga jamii iwe maeneo ya biashara au mikusanyiko wanatafuta mwanya wa kuwanyanyasa wananchi walipata fursa hiyo mahali hapo kwa sababu serikali ilikuwa katika kipindi cha mpito,” alisema Bw Ahmed Kaboole,