Tu-95MS: Kwa nini ndege hizi ni muhimu kwa Urusi na kwa nini inazificha dhidi ya Ukraine

Russia

Chanzo cha picha, MIL.RU

Shambulio kwenye eneo la uwanja wa ndege huko Engels (mkoa wa Saratov) mnamo Desemba 26 lilisababisha uharibifu mkubwa ikiwemo ndege za kimkakati za Tu-95MS za Urusi. Hizi ni ndege za aina gani na Moscow itaweza kuzilinda kwa sasa?

Kituo cha kimkakati cha usafiri wa anga katika mji wa Engels sasa kinaweza kuuita mwezi Desemba kama mwezi "mweusi". Kwa sababu katika kipindi hiki kimeshambuliwa mara mbili kwa njia ya anga.

Kulingana na picha za satelaiti na waandishi wa habari wa Ukraine, mashambulizi ya tarehe 5 na 26 Disemba, ambayo pengine yalifanywa na ndege zisizo na rubani za Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine, yaliua angalau wanajeshi watatu wa Urusi na kuharibu ndege hizi kimkakati za Tu-95MS.

Ni ndege hizi ambazo jeshi la Urusi hutumia kwa mashambulizi makubwa ya makombora kwenye miji ya Ukraine. Sasa zinapaswa kufichwa kwa kadri inavyowezekana.

Tu-95MS ni ndege za aina gani na kwa nini zinapewa thamani sana?

Ndege hizi zenye uwezo mkubwa wa makombora mazito (kulingana na kanuni za NATO zimepewa jina "Bear") zilitengenezwa miaka 40 iliyopita katika Umoja wa Kisovyeti.

Tu-95MS ilikuwa maboresho ya ndege ya mashambulizi ya Tu-95 na iliundwa kwa lengo la kubeba makombora ya kimkakati ya masafa marefu. Inachukuliwa zinaweza kurusha kombora kwa kasi zaidi hadi kilometa 830 kwa saa, na pia ni moja wapo ya sehemu ya kinachojulikana kama 'triad' ya nyuklia ya Shirikisho la Urusi.

Mbali na Tu-95MS, Tu-22M3 na Tu-160 zinaweza kurusha makombora ya masafa marefu. Haya ndiyo yale mabomu mazito ambayo Ukraine iliipa Urusi mwishoni mwa miaka ya 1990 pamoja na makombora mingine wakibadilishana na gesi asilia.

Russia

Chanzo cha picha, MIL.RU

Tofauti na Tu-160, ambayo inaweza kubeba makombora 12, Tu-95MS inabeba nusu ya idadi hiyo chini ya mabawa yake. Pia, haibebi wafanyakazi wengi - ni watu saba (kamanda wa ndege, kamanda msaidizi, rubani, rubani saidizi, mtu wa mawasiliano, mhandisi wa ndege, na kamanda wa mitambo ya moto).

Tu-95MS ina injini nne za turboprop (sio injini za ndege) na inaweza kuruka kilomita 10,500, na ina uwezo wa kubeba uzani wa juu kabisa wa tani 20.

Ndege hii ina urefu wa 49.6 m, na kwenda juu ina urefu wa 13.3 m, na upana wa mabawa wa mita 50. Kulingana na Military Balance, hadi mwisho wa mwaka jana, Urusi ilikuwa na ndege 60 za Tu-95MS. Lakini chapisho maalumu la Ukraine la Defense Express linaamini kwamba Urusi ina nusu tu ya idadi hiyo zilizo tayari kwa mapambano.

Vyombo vya habari pia vilizingatia ukweli kwamba katika miezi ya hivi karibuni, Shirikisho la Urusi lilianza kutumia Tu-95MS kwa kasi zaidi, badala ya Tu-160 ambazo ni kubwa na nzito (ambayo, pia inaweza kubeba makombora mara mbili).

Defense Express linahitimisha kwa kusema: wakati wa vita, Tu-95MS zimethibitisha kuwa ni "za kuaminika zaidi" kuliko Tu-160. Hata hivyo mashambulizi ya rasilimali hiyo yenye thamani yaliwalazimisha Warusi kuficha ndege hizi.

Mchezo wa kujificha kama paka na panya

Inapaswa kusisitizwa kuwa Ukraine haikuwajibika moja kwa moja kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye viwanja vya kimkakati vya Urusi.

Yuriy Ignat, msemaji wa Jeshi la Anga la Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine, anasisitiza kuwa kulikuwa na "pamba" huko Engels, lakini ni nani haswa na jinsi gani imefanyika ilifanyika haijulikani.

"Kwa kweli, matukio haya ni matokeo ya uchokozi wa Urusi," alitoa maoni yake kwa ufupi juu ya milipuko katika vituo vya ndege vya Urusi.

Russia

Chanzo cha picha, MAXAR TECHNOLOGIES

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Pia ni vigumu kutaja athari za mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya ndege hizi. Baada ya shambulio la kwanza mnamo Disemba 5, picha za satelaiti zinazoonyesha uharibifu wa angalau ndege moja, lakini baada ya shambulio la Desemba 26, "habari za ndani" kuhusu ndege iliyoharibiwa zilianza kuenea kwenye vyombo vya habari.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba siku ya shambulio hilo kulikuwa na wingu zito, ambalo lilifanya athari zisionekane vizuri na picha za satelaiti.

Mwanablogu wa kijeshi wa Ukraine Volodymyr Zolkin anadai, akinukuu vyanzo vyake, kwamba Urusi ilipoteza ndege tano za Tu-95MS huko Engels. Pia, Warusi 17 walidaiwa kuuawa na 26 kujeruhiwa katika mlipuko huo.

Lakini Wizara ya Ulinzi ya Shirikisho la Urusi yenyewe ilitambua vifo vitatu na kujeruhiwa kwa askari 4. Vifaa vya anga, kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, havikuharibika hata kidogo.

"Siwezi (kuthibitisha), siamini kabisa ... Nilipoona habari hii, nilishangaa. Ndege 5 (ziharibiwe) kwa mara moja? Lakini haziko sehemu moja, au katika ukaribu fulani. Ndege kama vile Tu-95, ziko umbali wa mamia ya mita kutoka moja na nyingine nyingine...achana na matamanio ya kufikirika," alisema mseaji wa jeshi kwenye Radio NV.