Kwanini Waafrika Kusini hawawezi kuwasha umeme

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Afrika Kusini imekabiliwa na msimu wa baridi kali huku ikikabiliwa na ukosefu mkubwa wa umeme kuwahi kushuhudiwa.

Watu wanakabiliwa na ukosefu wa umeme unaoendelea hadi saa sita kwa siku na kulazimiak akukabilaina na baridi mbaya kutokana na umeme usambazaji wa umeme usioaminika.

Katika siku halisi ya kampuni ya taifa ya umeme nchini humo Eskom inayoiita " hatua ya sita ya kupunguza mzigo " ni pamoja na kutokuwa na umeme asubuhi, kuendesha gari kwenda kazini kupitia barabara zeney msongamano wa magari kwasababu taa za barabarani hazifanyi kazi, kukumbwa na kelele za milio ya jenereta katika maeneo ya kazi, na halafu unabaini kuwa umeme umekatika tena wakati unaporejea tena nyumbani.

Inatosha kumfanya George Landon, mkazi wa mji mkuu wa Afrika Kusini Johannesburg, anataka kuihama nchi. "Nilikuwa na mtihani wa kazi mjini London. Ninatafuta ndege ya kesho kwasababu ya hali tuliyonayo. Kwa bahati mbaya ninaipenda nchi yangu, lakini nchi inapaswa kutupenda pia," anasema.

Utawala duni na ufisadi katika kampuni ya Eskom vimeifanya Afrika Kusini ikabiliwe na kukatika kwa umeme kwa miaka mingi lakini hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Nchi hiyo inakaribia haraka kufikia kiwango cha mwaka jana cha kukatwa kwa umeme kiasi cha gigawatt 2,521 za umeme. Hadi sasa, Eskom hukata umeme kwa kiwango cha saa za gigawatt 2,276 , na ni kwa mwezi Julai pekee.

Kuzuia ukosefu kabisa wa umeme, Eskom hukata umeme katika maeneo tofauti yan chi kwa wakati mmoja.

Wiki iliyopita Eskom iliingia hatua ya sita kwa mara ya kwanza tangu Disemba mwaka 2019, ikimaanisha kuwa ililazimika kukata kiwango cha saa zinazolingana na megawatt 6,000 ili kuzuia ukatwaji wa umeme wa nchi nzima.

Kuna hatua nane za kukata umeme- kila hatua inamaanisha saa za megawatt 1000 lazima zikatwe.

Wakazi wengi wanalazimika kukaa hadi saa sita kwa siku bila umeme .

Eskom inawaambia watu wakati umeme utakapokatwa katika eneo lao, lakini sio kila mara inafuata mpangilio wake. Mara nyingine, umeme unaweza kukatwa mapema au baadaye.

umeme

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sehemu kubwa ya umeme wa Afrika Kusini unatoka kwenye vituo vya makaa ya mawe.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sehemu kubwa ya umeme wa Afrika Kusini unatoka kwenye vituo vya makaa ya mawe.

Ukatwaji wa umeme umekuwa ukizidishwa na mgombo wa wafanyakazi wa Eskom ambao walifanya mgomo wiki iliyopita.

Mazungumzo ya mshahara baina ya Eskom na wafanyakazi kutoka vyama vutatu vya wafanyakazi yalivunjika, na kuwafanya wagome kufanya kazi, jambo lililoathiri utendaji vibaya na kazi muhimu ya ukarabati wa mitambo ya umeme.

Mkuu wa Eskom Andre de Ruyter aliwakemea wafanyakazi wanaogoma, akiuita mgomo "haramu" ana kuwashutumu kwa‘’kuiteka‘’ nchi.

Wafanyakazi wa Eskom wanatambuliwa kama wafanyakazi muhimu katika Afrika Kusini na hawaruhusiwi kugoma.

 Msemaji wa Muungano wa wafanyakazi wa vyma nchini Afrika Kusini (Numsa) Phakamile Hlubi, hatahivyo alisema serikali haitaki kukubali kuwa "kushindwa kwake vibaya kutekeleza majukumu yake" ndiko kulikosababisha mzozo wa ukosefu wa umeme.

Mkataba wa malipo kwa sasa umefikiwa lakini Eskom haimaanishi kuwa ndio mwisho wa kukatwa kwa umeme kwani ityachukua muda kumaliza shughuli zilizokwama za ukarabati.

Zaidi ya hayo, Eskom inakabiliwa na deni kubwa la dola bilioni $26 (£22bn), kutokana na kwamba inatumia vituo visivyo na ufanisi vya umeme ambavyo vinahitaji kukarabatiwa kila mara ili kuviwezesha kuendelea kufanya kazi.

Vituo viwili vya umeme ambavyo imevijenga vimekumbwa na matumizi ya kupita kiasi ya gharama, na kucheleweshwa kuanza utendaji. Matokeo yake havitengenezi umeme wa kutosha.

Mwezi Mei mwaka huu, Waziri wa raslimali za madini na nishati Gwede Mantashe alisaini mikataba mitatu ya kununua nishati kutoka kwa wazalishaji binafsi, ilionekana kama hatua ya kumaliza ukiritimba wa Eskom katika sekta ya umeme.

Inachukuliwa kama miradi mikubwa zaidi ya nishati mbadala ya jua na betri kwa pamoja duniani.

Huku kukiwa na mafanikio katika kuongeza kiwango cha umeme, rai awa Afrika Kusini wamekuwa wakitahadharishwa kuwa wategemee mgawo zaidi wa umeme kwa miaka mingine mwili hadi mitatu.

Maeneo masikini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika maeneo masikini zaidi ya Afrika Kusini, watu wengi huwasha mioto ili kujikinga na baridi

Kukatwa kwa umeme kuna athari mbaya kwa uchumi na kunaweza kuzorotesha ukuaji wa uchumi na kuufanya mzozo wa ukosefu wa ajira kuwa mbaya zaidi ambapo kwa sasa watu wasio na ajira nchini humo ni 34.5%.

Boitumelo Mokoena, ambaye anaendesha kampuni ya kutengeneza samani za nyumba mjini Alexandra, kitongoji cha mji wa Johannesburg ambacho ukosefu wa umeme unaua biashara yake, hususan ukosefu huu unapokuja baada ya masharti ya Covid.

"Wakati hakuna umeme machine kubwa lazima zizimwe. Imeathiri kazi yetu. Kuna nyakati ambapo wateja wetu wameshindwa kupata bidhaa zetu kwa wakati uiopangwa ."Biashara ndogo tayari zinahangaika katika soko, na kama usipofanya kazi iliyotarajiwa inakuwa hata vibaya zaidi ," Anasema Mokoena.

Biashara ndogo na za kati ndio msingi wa uchumi wa Afrika Kusini ulioathirika.