Ni kwanini Uingereza inawaonya marubani wake wa zamani wasitoe mafunzo kwa Wachina?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Madai yameibuka kwamba marubani wa zamani wa jeshi la Uingereza wanavuka kuingia China kwa njia ya kuwatambua na kuwafuata kwa ajili ya kazi ya kutoa mafunzo kwa jeshi la China

Uingereza imetoa tahadhari ikiwaonya wanajeshi wake wa zamani wasivutiwe na mikataba mizuri ya kufanya mafunzo na vikosi vya nchi hiyo, ikielezea hofu kwamba shughuli za aina hiyo zinaipatia Beijing fursa ya kupata siri za usalama na uwezo wa wa kiusalama wa Uingereza.

“China ni mshindani ambaye anatishia maslahi ya Uingereza katika maeneo mbali mbali duniani ,”Waziri wa ulinzi wa Uingereza James Heappey aliiambia televisheni ya Sky News katika mahojiano Jumanne . “Kumekuwa na hofu ndani MOD kwa miaka mingi,”aliongeza akimaanisha Wizara ya ulinzi ya Uingereza.

 Marubani hadi 30 wa zamani wa kikosi cha anga cha Uingereza - Royal Air Force huenda walikwenda Uchina kuwapatia mafunzo wanajeshi wa Uchina - People’s Liberation Army of China. BBC iliripoti kuwa baadhi ya walilipwa hadi dola $270,000.

Hii imeifanya Uingereza iangalie uwezekano wa kubadili sheria zake kwa ajili ya kuwatia katika hatia ya uhalifu wanajeshi wake wanaokubali mikataba ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa majeshi ya nchi fulani za kigeni.

G

Chanzo cha picha, UK POOL VIA ITN

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa ujasusi wa Uingereza-MI5, Ken McCallum (kushoto) na Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani FBI Christopher Wray (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari mjini London

Tumewasiliana na watu ambao wanahusika na tumekuwa wazi kwao kwamba ni matarajio yetu kwamba hawataendelea kuwa sehemu ya mpango ule, na tutaiweka katika sheria , kwamba mara watu wanapopewa onyo lile, itakuwa ni kosa kuendelea na mafunzo hayo,” Heappey aliongeza.

Alisema kuwa kwamba Beijing ni mshirika “muhimu” wa Uingereza lakini akasema China “haifichi katika jaribio lake la kupata siri zetu, na kuwaajiri kwao marubani wetu ili kuelewa uwezo wa vikosi vyetu ni hofu ya wazi kwetu”

Msemaji wa Waziri wa mambo ya nje Wang Wenbin Jumamne alisema haelewi lolote kuhusu juhudi za kuwaajiri wanajeshi wa zamani wa Uingereza.

 Katika taarifa yake kwa gazeti la The Washington Post,msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Uongereza aliita ajira ya aina hiyo changamoto ya “kisasa”, akielezea kwamba “wanajeshi wa zamani na wale wanaohudumu kwa pamoja wanawajibika kulinda sheria ya siri rasmi, na tunatathmini matumizi ya mikataba ya sirina makubaliano ya kutoifichua katika huduma zote za ulinzi .”

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Sheria ya siri rasmi inaweka adhabuzinazotolewa kutokana na hujuma na kufichua taarifa rasmi kinyume cha sheria kwa baadhi ya wafanyanyazi walioajiriwa na serikali.

“Tunachukua hatua kusitisha mifumo ya uajiri ya Kichina inayojaribu kuwawinda marubani wanajeshi wanaohudumu sasa na wa zamani kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa jeshi la Uchina - People’s Liberation Army ,” Taarifa ya Wizara ya ulinzi ya Uingereza iliongeza.

Uhusiano baina ya Beijing na London ume umeingia dosari katika miaka ya hivi karibuni juu ya biashara, hofu kuhusu uhuru katika Hongkong

Koloni la zamani la Uingereza, na jinsi Uchina inavyowatendea Waislamu wa Uighur katika jimbo la China la Xinjiang.

Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss awali alisema China ni tisho kwa sheria za kimataifa na aliishutumu Beijing kwa “kujenga haraka uwezo wa kijeshi na kuimarisha nguvu zake katika maeneo ya ndani zaidi ya bahari ya maslahi ya kimkakati ya Ulaya .”

 Wiki iliyopita, mkuu wa ngazi ya juu zaidi wa ujasusi nchini Uingereza alitoa hotuba ya nadra kwa umma, akionya kuhusu azma ya uchina ya kupanua eneo lake la ushawishi kwa kutumia sayansi na teknolojia.

Akiuita “Wakati wa milango inayoteleza katika historia ” Jeremy Fleming, mkuu wa GCHQ — Shirika la ujasusi, mtandao na usalama — alishutumu onyo la China la “gharama iliyojificha” utegemezi wa kupindukia wa teknolojia ya Kichina.

Sio uingereza pekee ambayo ina hofu juu ya China

Wiki iliyopita, ikulu ya Marekani White House, ilisema katika mkakati wake wa uslama wa taifa kwamba China imeendelea kuwa changamoto kubwa zaidi yenye athari ya siasa za kieneo kwa Marekani, licha ya vita vya Urusi vinavyoendelea nchijni Ukraine. Beijing katika jibu lake iliishutumu Washington kwa “fikra za Vita Baridi” na ikatoa wito wa juhudi bora za kurejesha mahusiano magumu.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Xi Jinping anataka kubadilisha jeshi la Uchina kuwa jeshi la kisasa zaidi duniani kufikia mwaka 2049, kulingana na pentagon

Uhusiano baina ya Beijing na London ume umeingia dosari katika miaka ya hivi karibuni juu ya biashara, hofu kuhusu uhuru katika Hongkong

Koloni la zamani la Uingereza, na jinsi Uchina inavyowatendea Waislamu wa Uighur katika jimbo la China la Xinjiang.

Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss awali alisema China ni tisho kwa sheria za kimataifa na aliishutumu Beijing kwa “kujenga haraka uwezo wa kijeshi na kuimarisha nguvu zake katika maeneo ya ndani zaidi ya bahari ya maslahi ya kimkakati ya Ulaya .”

 Wiki iliyopita, mkuu wa ngazi ya juu zaidi wa ujasusi nchini Uingereza alitoa hotuba ya nadra kwa umma, akionya kuhusu azma ya uchina ya kupanua eneo lake la ushawishi kwa kutumia sayansi na teknolojia.

Akiuita “Wakati wa milango inayoteleza katika historia ” Jeremy Fleming, mkuu wa GCHQ — Shirika la ujasusi, mtandao na usalama — alishutumu onyo la China la “gharama iliyojificha” utegemezi wa kupindukia wa teknolojia ya Kichina. 

Kwa sasa sheria haijavunjwa

Kwa sasa, marubani wa zamani wa jeshi hawavunji sheria ya sasa ya Uingereza kwa kukubali kufanya kazi, lakini Uingereza na mataifa mengine ya Magharibi yanapanga kuchukua hatua za ziada za kukabiliana na mafunzo hayo, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza.